Tetesi: 90% ya Waandamanaji kutoka Mikoani wamewasili Dar es Salaam, Waliosalia ambao wengi wataingia Jumamosi wameombwa kutokuvaa sare za CHADEMA safarini

Waambieni watajuwa jiji.

Kuna FFU na mbwa zao wametoka mafunzoni wanasubiri kuwalinda mitaani Dar. Wengine wamesambazwa mikoani.

Wanajeshi pia watakuwa na zoezi la kuwasafishia mitaa ili waandamane vizuri.
Kwahiyo nyinyi ccm hamna tena uwezo wa kujibu hoja, mnategemea FFU tu!
 
Wamewahi kufanya Ubaya gani, Wapi?
 
Umeongea kwa Hekima kubwa!Mwenye Akili na Asikie maneno hayo.
 
Waambieni watajuwa jiji.

Kuna FFU na mbwa zao wametoka mafunzoni wanasubiri kuwalinda mitaani Dar. Wengine wamesambazwa mikoani.

Wanajeshi pia watakuwa na zoezi la kuwasafishia mitaa ili waandamane vizuri.
Acheni kuwatisha watu mara kifo ni kifo km kuua kwenu sio ajabu mara mbwa mara ffu acheni kutisha watu acheni watu waandamane kudai haki zao
 
Kwahiyo wanadasalama hawatoshi

Kweli chagadema kimeisha
 
TUSAIDIE SERIKALI KUWE NA UTULIVU:-
1. Wanadai nini?
2. Wamewaomba mazungumzo hao wanao wadai wakakataliwa?
3. Kwanini tuingie kwenye maandamano wakati tuna mawaziri, wakuu wa mikoa, waziri mkuu na Rais ambaye anaweza kuombwa venue ya mdahalo na mambo yakawekwa sawa?

USHAURI:
Vyama vikae mezani, kuwe na muafaka wa kitaifa, tuendelee kutunza tunu yetu ya amani.
 
Maandamano ya transformation huwa hayatangazwi kajifunzeni kwa wamasai na kwingineko! Watanzania bado hawajawa tayari kwa mabadiliko wakifikia stage hiyo hawatasubiri waitwe na wanasiasa! Kwa sasa hv ni njia zingine zinafaa kwa sababu hawatakuja
 
Na nyinyi fanyeni kama Tunisia, mtaijuwa hii ni Tunisia au Tanzania.

Usimdanganye yule Mzanzibar.
Hakuna jeshi litakalokubali kuua ndugu zake kwa sababu ya mtu asiyekuwa na dira .

Tanganyika hatutaki kuuana kwa sababu ya Mzanzibar .

Hatujazoa kubaguana sisi ndio maana huku Tanganyika kuna watu wa dini tofauti waliooana na kila mmoja anakaa na dini yake mpaka wanakufa lakini kule kwao ni wabaguzi hawana uvumilivu .
Hatutaki atuletee hasira na ubaya wake huku.
Eti kifo ni kifo tu.
Nimekereka sana.
 
Tunu ipi ya amani unayoitunza hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…