A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

hatujawahi kufikiria kufanya ukatili na unyama kwa viumbe ambavyo ni mfano wa watu weusi kasoro rangi.
Mkuu hakuna kitu kinaitwa UKATILI katika dunia ya ushindani. It's survival of the fittest. Mbona tulifahamu ya kuwa vita ya Kagera ingetugharimu lakini still tukaenda kupigana na Idd Amin? Huo unaouita ukatili ndio umewafikisha wazungu hapa walipo kiasi kwamba ukishindwa kuzungumza lugha yao kwa ufasaha unaitwa msamba/mbumbumbu
 
Historia inasema watu weusi kabila ya Moors toka kaskazini mwa Afrika walienda Ulaya hasa Spain na kuwatwala wazungu.
Waliwakuta wazungu hawana ustaarabu wa kutumia vyoo vya kisasa, sauna na swimming pools, kisha hawa weusi wakapeleka ustaarabu huo huko Spain na kujenga majengo ya kisasa ambayo mengine hata sasa yapo kama alama.
 
Historia inasema watu weusi kabila ya Moors toka kaskazini mwa Afrika walienda Ulaya hasa Spain na kuwatwala wazungu.
@Then, what happened next? It looks like things have been turned upside down
 
Ina maana hatukuwa hata na sababu ya kwenda kwao kiunguzi tu !
Majibu mengi humu hayalidhishi. Hata vitabu vya Historia vinaanzia karne ya kumi na tano lakini bado mfano wetu na wa Wazungu haukuwa sawa na haukulingana. nafkiri tuendelee kufikirisha fikra mbona waarabu walifika katika kipindi cha nyuma zaidi kabla ya Wazungu kwa nini sisi tulikuwa nyuma ya jamii hizo kwenda kwao na kufanya kama wao walivyofanya? Vitabu vinasema walivyokuja ndiyo wameleta utegemezi kwetu mpaka leo na utajiri kwao mpaka leo kwa hiyo kwa namna zozote hata sisi tungekuwa na maarifa ya ku wawai kwenda kwao na kufanya walivyofanya kwa wakatu ule Africa ingekuwa tofauti( Kwa mawazo yangu).
Kuna methali ya Kiingereza inasema "Necessity is the mother of invention".

Ikimaanisha kwamba, uhitaji wa kitu ndio unamfanya mtu agundue vitu. Kama mtu hana uhitaji, kugundua vitu vipya kunakuwa haba sana.

Kwenye hii habari ya Waafrica kuna mengi.

Africa ina land mass kubwa sana inland. Watu wengi walipotaka kupanua wigo wa makazi yao, walipanua wigo huo ndani ya Afrika bila kuhitaji kwenda nje. Hawakuhitaji kwenda nje kwa sababu walipata wanyama wa kuwinda, mifugo na mazao ya kilimo kwa urahisi ndani ya Afrika. Ukiangalia Bantu migration, na hata migration za watu wa Afrika kabla, utaona hili.

Bara la Ulaya licha ya kuwa halina hali nzuri sana ya hewa kwa maana ya kwamba lina baridi na vitu havioti mwaka mzima, na vinavyoota ni vichache, pia lina tabia ya kijiograpfia ya kutokuwa na hinterland kubwa sana, sehemu nyingi zipo karibu na pwani.Hili linachangia kuwafanya watu wajipanue makazi kwa kusafiri baharini, zaidi ya kujipanua makazi kwa kujikita bara.

Kuna hilo. Pia kuna la utashi. Wenzetu wana utashi. Wakiona mlima wanataka kuupanda.Sisi tukiona mlima tunausema ni makazi ya Mungu. Ukimueleza Muafrika wa asili habari ya wazungu kupanda milima, atashangaa sana, atauliza, kupanda mlima kunamsaidiaje? Wenzetu wanaona ni changamoto ya kuikabili na kuishinda. Wenzetu wanaishi kwa kutaka kuyapinda mazingira yaendane na wanavyotaka wao. Sisi tunaishi kwa kukubali kwamba inabidi tukubali mazingira yalivyo. Hili jambo linatakiwa kwa kuangalia pande zote mbili. Jamii inayosema inakubali mazingira tu inaweza kupata ugonjwa isitafute dawa, kwa sababu ugonjwa nao si sehemu ya mazingira? Unakubali tu. Lakini, jamii inayotaka kuyapinda sana mazingira kama dunia ya sasa ndiyo inatuletea mfumuko wa ma pandemic (kwa kupitia kirahisi utandawazi nasafari za ndege za watu wengi kimataifa), ma global warming na vitisho vya kumalizana pakubwa vita vya nyukilia.

Halafu pia, nafikiri, Waafrika wa asili walikuwa wanapenda jamii na familia zao sana, kiasi kwamba, kuondoka nyumbani kulichukuliwa kama utoro na kukosa mapenzi kwa familia au jamii yako.Wajibu kwenye jamii ulikuwa mkubwa sana, kiasi, kwenda mbali ilikuwa tatizo.

Kuna mfano wa Mfalme mmoja wa Mali ya kale, Mansa Aboubakar. Mansa Aboubakar (abdication 1311) alikuwa mfalme wa Mali kabla ya Mansa Musa. Na tunajua habari zake, kwa sababu, Mansa Musa - mtu anayehesabika kuwa tajiri kuliko wote waliowahi kutokea duniani- alivyokuja kuchukua ufalme baada ya Mansa Aboubakar, Mansa Musa alienda kuhiji Mecca. Kwenye safari hiyo, akiwa Cairo - ambapo alitoa sadaka ya dhahabu mpaka dhahabu ikashuka bei Cairo kwa miaka kadhaa - aliulizwa.Mansa Musa, ulipataje kuwa Mfalme wa Mali?

Mansa Musa akajibu. Akasema kabla yangu alikuwapo Mansa Aboubakar. Na Mansa Aboubakar kwa utashi wake mkubwa, alisema kwamba, kama unavyoona mto huu (Niger) una ng'ambo ya mbili upande huu na ule, hata ile bahari kubwa nayo (Atlantic) ukiivuka, kuna nchi upande wa pili vile vile. Akapakia mashua nyingi chakula, maji na dhahabu, akaenda safari, akaacha ufalme.Walipofika katikati ya bahari wakakutana na mawimbi makubwa sana, jahazi la mwisho likaamua kurudi kutoa habari kwamba Mansa Aboubakar amekwenda mbali sana mpaka bahari ya mawimbi makubwa.

Kuna habari kwamba Mansa Aboubakar alifika America kabla ya Christopher Columbus.

Lakini unajua nchini kwake Mali Mansa Aboubakar alichukuliwaje?

Alichukuliwa kama msaliti aliyekimbia kwao, akajiuzulu ufalme huku kawaacha watu wake. Kuna kitabu kinaandika majina ya Wafalme wa Mali.Kuna kipindi Mansa Aboubakar alifutwa, kwa sababu ya usaliti.

Sasa huyo mvumbuzi mwenye utashi wa kutaka kujua nchi nyingine zikoje, kaonwa msaliti!

Soma zaidi kuhusu Mansa Aboubakar hapa Abu Bakr II - Wikipedia

Tukiongelea falme, hapo tutaona uvumbuzi wa kwenda nchi za mbali unahitaji mitaji mikubwa inayoweza kukusanywa katika jamii zinazoishi katika nchi zenye serikali/ falme kubwa. Ndiyo maana wavumbuzi walioanza kuvumbua nchi za mbali za dunia, hata huko Ulaya, walitoka Uhispania, Ureno, Uingereza na Italy. Ni vigumu kusikia mvumbuzi wa kutoka Croatia.

Sisi hatukuwa na city states kubwa nyingi, na chache zilizokuwepo, zilifanya biashara na watu wa nje na kuanza kuvumbua kama huo mfano wa Mansa Aboubakar. Tatizo hatukuwa na moyo wa kuvumbua.Tuvumbue wapi na sisi tuliona dunia iko kwetu?

Kitu kingine, ikumbukwe kwamba Africa haikuwa na watu wengi sana mpaka miaka ya karibuni. Inakadirikwa kwamba, kufikia mwaka 1600, Africa nzima ilikuwa na watu milioni kama 55 tu. Hii ni sawa na idadi ya Watanzania tu leo.Ulaya, ambayo ni ndogo kulinganisha na Africa na haina maliasili nyingi, inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 1600 ilikuwa na watu milioni 78. Msongamano wa watu ni moja ya sababu zinazofanya watu waende kutafuta maisha pengine, Bila msongamano wa watu, ni vigumu watu kutafuta maisha sehemu nyingine.

Zaidi, ukisoma historia, ukatafuta utafiti wa kibaiolojia wa DNA diversity, utaona kwamba, watu karibu wote wa dunia hii, wametokea Africa. Sasa labda tulishafanya misafara ya mbali, tukaja kuona madhila yake, tukaamua kujisogetza polepole.

Mpaka leo kuna watu wengi tu Africa wana falsafa za "tutabanana hapa hapa".
 
@absolutely right
 
Nafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'. Huwezi kumlaumu mzungu ambaye alikuwa na utashi wa kutoka kwake kuja Africa kwa ground kuwa kwanini walikuja. Hapa ndiyo huo utashi unaouzungumzia unapoingia. Nafkiri utashi wa wazungu wa tangu1480's ndiyo unaoamua mambo mengi katika dunia hata leo. Kwa mfano hiyo entourage Mansa Musa kwenda Mecca na utajiri aliokuwa ungeweza kufanya maeneo yanayopatikana Mali (nchi) ya leo isiwe na matatizo iliyonayo leo. lakini yeye Mansa Musa utashi wake ulikuwa ni kwenda kuhiji akiwa na watu zaidi ya 1000 tena kwa kuzungukia Maurtania-Morroco-Tunisia mpaka Misri. Hapa inatupa pich ya utifauti wa utashi wa waafrica na wazungu tangu zamani.
 
Nafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'.
Well said
 
Nafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'. Huwezi kumlaumu mzungu ambaye alikuwa na utashi wa kutoka kwake kuja Africa kwa ground kuwa kwanini walikuja. Hapa ndiyo huo utashi unaouzungumzia unapoingia. Nafkiri utashi wa wazungu wa tangu1480's ndiyo unaoamua mambo mengi katika dunia hata leo. Kwa mfano hiyo entourage Mansa Musa kwenda Mecca na utajiri aliokuwa ungeweza kufanya maeneo yanayopatikana Mali (nchi) ya leo isiwe na matatizo iliyonayo leo. lakini yeye Mansa Musa utashi wake ulikuwa ni kwenda kuhiji akiwa na watu zaidi ya 1000 tena kwa kuzungukia Maurtania-Morroco-Tunisia mpaka Misri. Hapa inatupa pich ya utifauti wa utashi wa waafrica na wazungu tangu zamani.
Mansa Musa kasafiri unamlaumu, asingesafiri ungemlaumu kwa nini Waafrika hawajasafiri!

Utashi unaenda na vipaumbele vya jamii.

Waafrika kipaumbele chao tangu awali ni kuishi kwa amani na utulivu, Ndiyo maana Waafrika original walikuwa watu peaceful sana. Sasa, ukiwa mtu peaceful habari za maendeleo ya kumfanya mwenzako awe mtumwa huwezi, mambo ya kwenda nchi za watu utaona mwiko, utaona unawaingilia sehemu zao.

Hizi sheria hata wanyama wanazo, wana kojolea sehemu zao kuzi mark, akija mnyama mwingine ajue hapa ni eneo la mnyama tofauti na mimi.

Wazungu waliondoa habari za kutaka kuishi kwa amani, wao kipaumbele chao kikawa kupata utajiri.Na ukiwa na mawazo hayo ndiyo unapata habari za kuafanya wenzako watumwa na makoloni.

Swali la muhimu hapa ni, je, ingewezekana dunia kupata maendeleo ya kiuchumi bila amani kuvunjwa? Bila watu kufanywa watumwa na vita kubwa kufanyika?

Na kama iliwezekana, hao mnaosema wazungu, walikosea kutafuta maendeleo kwa vita na utumwa na ukoloni? Hiyo ni akili nzuri au mbaya?

Na kama haikuwezekana, tukipata maendeleo sana, halafu dunia ifike mwisho wa uwezo wake wa ku support maisha, kwa sababu ya ma global warming, ma nuclear weapons etc, hayo maendeleo yakakayomaliza maisha duniani yatakuwa na maana gani?
 
Mkuu hakuna kitu kinaitwa UKATILI katika dunia ya ushindani. It's survival of the fittest. Mbona tulifahamu ya kuwa vita ya Kagera ingetugharimu lakini still tukaenda kupigana na Idd Amin? Huo unaouita ukatili ndio umewafikisha wazungu hapa walipo kiasi kwamba ukishindwa kuzungumza lugha yao kwa ufasaha unaitwa msamba/mbumbumbu
Ugundue tuna interest tofauti, we don't need to dominate wazungu in order to survive ujue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?

NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.

Salute infantry Soldier!
Mada yako nzuri sana,inahoji nafasi ya bara la afrika na hiba yake katika historia ya Ulimwengu huu!
Kwanini Waafrika Hawakuvamia Ulaya na Marekani na Kuchukua Mateka?

Historia Tuliyofundishwa darasani inamapungufu mengi sana! Imekosewa mno! Imeondoa heshima ya mwafrika mahala pake panapostahili.

Afrika ni Bara Mama la Mabara yote! Wakati wa Utawala wa Ustaarabu wa Wayunani na Warumi Hakuna sehemu wameacha kutaja bara la Afrika.
Aliyetunga Mtaala wa Historia ya Afrika na Kuanza na hadithi za Uvamizi wa Ulaya Afrika alikusudia kupotosha yafuatayo;-

1. AFRICA/AFARIK/AFRIGA - Ilitokana na maneno ya kiyunani "afarik/Afriga" ikimaanisha eneo lenye Joto au nchi yenye ahueni ya Hali ya hewa cf. Prof Bethwell Ogot - General History of Africa Vol. 1.

Kwa hoja hiyo naungana na Sir Kiranga kuunga mkono hoja ya "necessity" Afrika ilijitosheleza mno! Afrika ndio iliyozalisha chakula wakati wote wa Utawala wa Roman Empire.

Mwaka 218 -201 KK (Kabla ya Kristo) Afrika iliivamia Ulaya na Kuteka mali nyingi na lengo ilikuwa ni kuangusha dola ya Kirumi, Vita hivi ni maarufu sana na vilijulikana kama Vita vya pili vya Punic vikiongozwa na JENERALI HANNIBAL kutoka Cathage (Afrika Kaskazini) kuvuka bahari ya Mediterranean na Kupiga Hispania mpaka roma italy,Majeshi ya Askari wa Miguu (Infantry) na Vifaru vya Tembo vilitikisa mitaa ya Barcelona,Sicily mpaka macedonia ! Kichapo walichokipata Wazungu walibaki wanasimulia vizazi hadi vizazi - Kama sio Unjanja na Mbinu za Fabius Cuntactor basi leo Afrika ingeitawala Ulaya kwa kipindi kirefu sana!

Watoto wa Kiitalia walikuwa wakideka na kujiliza baada ya vita hivi Wazazi wao waliwatishia jina la Huyu Jemedari Hannibal wakanyamaza mara moja - "Hannibal huyoo anakuja nyamazaaa".

Hivyo Tungeanza kusimuliwa kwanza Jinsi Afrika ilivyoivamia Ulaya na Kuipiga halafu tuambiwe baadae mambo ya Berlin Conference ya juzi juzi.
Hivyo Mambo ni mengi sana! Afrika imeficha Siri ya Ustaarabu wa Hii Dunia - Na hao mabwana Mzungu hawataki kabisa Mwafrika aijue thamani yake.

Uvumbuzi mwingi uliofanyika Marekani Ulifanywa na Black Americans.(Saa,Mbegu bora,Lishe,Sabuni, na nk)

Hili Hawabishi kabisa kuwa Chuma kwa mara ya Kwanza uvumbuzi wake ulifanyika Afrika.

Hata Swala la Biashara ya Utumwa liliposhindikana kwa binadamu wote(Encomienda and Indentured labour) ndipo walipogeukia Afrika na ikawezekana - Kila mzungu na Wazawa wa marekani walipojaribu kufanya kazi za kitumwa walikufa kama Samaki kwenye Ndoo.
Mwafrika alipofikishwa Marekani Alimudu Kazi za Kitumwa kwa Ufanisi Mkubwa mnooooo.

Waafrika Hatukuhitaji kuteka Mtu kwa Sababu Kazi zetu tulizimudu wenyewe vema!
Waafrika Hatukuhitaji Kuvamia Maeneo mengine kwa sababu Bara letu lilitutosha kabisa.
Asante.
 
Wazungu waliondoa habari za kutaka kuishi kwa amani, wao kipaumbele chao kikawa kupata utajiri.Na ukiwa na mawazo hayo ndiyo unapata habari za kuafanya wenzako watumwa na makoloni.
HAKUNA binadamu ambaye hapendi utajiri mkuu. Ndio maana hata mama muuza vitumbua akiuza idadi chache ya vitumbua vyake leo tofauti na idadi aliyouza jana roho yake inasononeka sana
 
Watoto wa Kiitalia walikuwa wakideka na kujiliza baada ya vita hivi Wazazi wao waliwatishia jina la Huyu Jemedari Hannibal wakanyamaza mara moja - "Hannibal huyoo anakuja nyamazaaa".
@Hahahaaaaa. Hii nimeipenda sana mkuu. Asante sana
 
HAKUNA binadamu ambaye hapendi utajiri mkuu. Ndio maana hata mama muuza vitumbua akiuza idadi chache ya vitumbua vyake leo tofauti na idadi aliyouza jana roho yake inasononeka sana
Utajiri ni nini?

Ukiambiwa uende porini ambako kuna Simba wamejaa, ambako utaliwa na Simba, huna silaha wala nyenzo, ila kuna utajiri mwingi sana, ukienda utakufa, usipoenda utabaki na maisha ya hela ya kubadikisha mboga kila siku, hutakuwa tajiri, lakini hutakufa, utaenda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugundue tuna interest tofauti, we don't need to dominate wazungu in order to survive ujue.

Sent using Jamii Forums mobile app
But our (African) survival largely depends on "Wazungu" domination. Wazungu wakisema wanatunyima misaada ya hali na mali, uonaona namna serikali za Afrika zinavyohaha kuomba msamaha ili kuendelea kupata ufadhili? Makomandoo wa Ufaransa waliingia Ivory coast kisha kumkamata Rais wao Bagbo, wakamtandika makofi ya uso kisha kumpeleka The Hague. Where was the African Union?
 
Swali la muhimu hapa ni, je, ingewezekana dunia kupata maendeleo ya kiuchumi bila amani kuvunjwa? Bila watu kufanywa watumwa na vita kubwa kufanyika?
@Hapo kwenye neno dunia ulipaswa kusema neno wazungu kwa maana wao ndio waliovunja amani kwa kuwafanya waafrika kuwa watumwa kwa maendeleo yao
 
Asante kwa hii point pia mkuu. Ila ninaomba uitolee ufafanuzi kidogo kama inawezekana. What did Fabius really do kubadili upepo wa vita?

Fabian Strategy - Ilikuwa ni mbinu ya Kuwachelewesha na Kuwazubaisha maadui! Wakati wewe ukijipanga vema kushambulia.
Huyu Bwana badala ya Kutuma Askari wake Wakapambane na Majeshi ya Hannibal Ana kwa Ana - Alituma askari wachache kuziba njia na kuvunja madaraja ambayo hannibal angetumia kuja Roma.

Alituma Askari wake Kukwea Juu ya Vilima na Kushambulia kwa mbali majeshi ya Hannibal kwa upande danganyifu(indirection) au Misdirection.Hivyo Majeshi ya Hannibal yakaelekeza nguvu kwenye WRONG TARGET.

Aliaamuru Wana vijiji kuchoma mashamba yao na Chakula chao chote na kuikimbia miji yao na kwenda kujificha walikoambiwa.

Hii iliwafanya ASkari Wa Hannibal The Great kukosa chakula na kushuka Morale ikawachelewesha kuufikia Mji wa Roma na Wakajikuta wamekosa Nguvu na Supply ya Vita.

Wanaojifunza Guerrilla Warfare lazima Wamsome Quintus Fabius Maximus. Alichangia nadharia nzuri sana katika Vita.

Merci Beacoup!
 
Ukiambiwa uende porini ambako kuna Simba wamejaa, ambako utaliwa na Simba, huna silaha wala nyenzo, ila kuna utajiri mwingi sana, ukienda utakufa, usipoenda utabaki na maisha ya hela ya kubadikisha mboga kila siku, hutakuwa tajiri, lakini hutakufa, utaenda?
@Scenario hii inategemea na ujasiri wa mtu. Mimi ninakwenda ila kuna mwingine hawezi kwenda hata ukimpa silaha.

Na hii kitu (risk taking) ndio humtofautisha mjarisiamali na mtu wa kawaida. Inawezekana hata huko porini hakuna Simba ila watu wanataka kupima ujasiri wako.

Wazungu waliweza kutoka kwao na kuja kwetu Afrika kwa maana walikuwa ni risk takers. Walijua wanakuja watakutana na dhoruba kali baharini wakiwa na majaazi still wakaja.

Walijua wanakuja kukutana na watu wasiokuwa na taarifa za kutosha juu yao still wakaja na kutuma wapelelezi. The higher the risk one is willing to take, the higher the return.
 
Back
Top Bottom