Kuna methali ya Kiingereza inasema "Necessity is the mother of invention".
Ikimaanisha kwamba, uhitaji wa kitu ndio unamfanya mtu agundue vitu. Kama mtu hana uhitaji, kugundua vitu vipya kunakuwa haba sana.
Kwenye hii habari ya Waafrica kuna mengi.
Africa ina land mass kubwa sana inland. Watu wengi walipotaka kupanua wigo wa makazi yao, walipanua wigo huo ndani ya Afrika bila kuhitaji kwenda nje. Hawakuhitaji kwenda nje kwa sababu walipata wanyama wa kuwinda, mifugo na mazao ya kilimo kwa urahisi ndani ya Afrika. Ukiangalia Bantu migration, na hata migration za watu wa Afrika kabla, utaona hili.
Bara la Ulaya licha ya kuwa halina hali nzuri sana ya hewa kwa maana ya kwamba lina baridi na vitu havioti mwaka mzima, na vinavyoota ni vichache, pia lina tabia ya kijiograpfia ya kutokuwa na hinterland kubwa sana, sehemu nyingi zipo karibu na pwani.Hili linachangia kuwafanya watu wajipanue makazi kwa kusafiri baharini, zaidi ya kujipanua makazi kwa kujikita bara.
Kuna hilo. Pia kuna la utashi. Wenzetu wana utashi. Wakiona mlima wanataka kuupanda.Sisi tukiona mlima tunausema ni makazi ya Mungu. Ukimueleza Muafrika wa asili habari ya wazungu kupanda milima, atashangaa sana, atauliza, kupanda mlima kunamsaidiaje? Wenzetu wanaona ni changamoto ya kuikabili na kuishinda. Wenzetu wanaishi kwa kutaka kuyapinda mazingira yaendane na wanavyotaka wao. Sisi tunaishi kwa kukubali kwamba inabidi tukubali mazingira yalivyo. Hili jambo linatakiwa kwa kuangalia pande zote mbili. Jamii inayosema inakubali mazingira tu inaweza kupata ugonjwa isitafute dawa, kwa sababu ugonjwa nao si sehemu ya mazingira? Unakubali tu. Lakini, jamii inayotaka kuyapinda sana mazingira kama dunia ya sasa ndiyo inatuletea mfumuko wa ma pandemic (kwa kupitia kirahisi utandawazi nasafari za ndege za watu wengi kimataifa), ma global warming na vitisho vya kumalizana pakubwa vita vya nyukilia.
Halafu pia, nafikiri, Waafrika wa asili walikuwa wanapenda jamii na familia zao sana, kiasi kwamba, kuondoka nyumbani kulichukuliwa kama utoro na kukosa mapenzi kwa familia au jamii yako.Wajibu kwenye jamii ulikuwa mkubwa sana, kiasi, kwenda mbali ilikuwa tatizo.
Kuna mfano wa Mfalme mmoja wa Mali ya kale, Mansa Aboubakar. Mansa Aboubakar (abdication 1311) alikuwa mfalme wa Mali kabla ya Mansa Musa. Na tunajua habari zake, kwa sababu, Mansa Musa - mtu anayehesabika kuwa tajiri kuliko wote waliowahi kutokea duniani- alivyokuja kuchukua ufalme baada ya Mansa Aboubakar, Mansa Musa alienda kuhiji Mecca. Kwenye safari hiyo, akiwa Cairo - ambapo alitoa sadaka ya dhahabu mpaka dhahabu ikashuka bei Cairo kwa miaka kadhaa - aliulizwa.Mansa Musa, ulipataje kuwa Mfalme wa Mali?
Mansa Musa akajibu. Akasema kabla yangu alikuwapo Mansa Aboubakar. Na Mansa Aboubakar kwa utashi wake mkubwa, alisema kwamba, kama unavyoona mto huu (Niger) una ng'ambo ya mbili upande huu na ule, hata ile bahari kubwa nayo (Atlantic) ukiivuka, kuna nchi upande wa pili vile vile. Akapakia mashua nyingi chakula, maji na dhahabu, akaenda safari, akaacha ufalme.Walipofika katikati ya bahari wakakutana na mawimbi makubwa sana, jahazi la mwisho likaamua kurudi kutoa habari kwamba Mansa Aboubakar amekwenda mbali sana mpaka bahari ya mawimbi makubwa.
Kuna habari kwamba Mansa Aboubakar alifika America kabla ya Christopher Columbus.
Lakini unajua nchini kwake Mali Mansa Aboubakar alichukuliwaje?
Alichukuliwa kama msaliti aliyekimbia kwao, akajiuzulu ufalme huku kawaacha watu wake. Kuna kitabu kinaandika majina ya Wafalme wa Mali.Kuna kipindi Mansa Aboubakar alifutwa, kwa sababu ya usaliti.
Sasa huyo mvumbuzi mwenye utashi wa kutaka kujua nchi nyingine zikoje, kaonwa msaliti!
Soma zaidi kuhusu Mansa Aboubakar hapa
Abu Bakr II - Wikipedia
Tukiongelea falme, hapo tutaona uvumbuzi wa kwenda nchi za mbali unahitaji mitaji mikubwa inayoweza kukusanywa katika jamii zinazoishi katika nchi zenye serikali/ falme kubwa. Ndiyo maana wavumbuzi walioanza kuvumbua nchi za mbali za dunia, hata huko Ulaya, walitoka Uhispania, Ureno, Uingereza na Italy. Ni vigumu kusikia mvumbuzi wa kutoka Croatia.
Sisi hatukuwa na city states kubwa nyingi, na chache zilizokuwepo, zilifanya biashara na watu wa nje na kuanza kuvumbua kama huo mfano wa Mansa Aboubakar. Tatizo hatukuwa na moyo wa kuvumbua.Tuvumbue wapi na sisi tuliona dunia iko kwetu?
Kitu kingine, ikumbukwe kwamba Africa haikuwa na watu wengi sana mpaka miaka ya karibuni. Inakadirikwa kwamba, kufikia mwaka 1600, Africa nzima ilikuwa na watu milioni kama 55 tu. Hii ni sawa na idadi ya Watanzania tu leo.Ulaya, ambayo ni ndogo kulinganisha na Africa na haina maliasili nyingi, inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 1600 ilikuwa na watu milioni 78. Msongamano wa watu ni moja ya sababu zinazofanya watu waende kutafuta maisha pengine, Bila msongamano wa watu, ni vigumu watu kutafuta maisha sehemu nyingine.
Zaidi, ukisoma historia, ukatafuta utafiti wa kibaiolojia wa DNA diversity, utaona kwamba, watu karibu wote wa dunia hii, wametokea Africa. Sasa labda tulishafanya misafara ya mbali, tukaja kuona madhila yake, tukaamua kujisogetza polepole.
Mpaka leo kuna watu wengi tu Africa wana falsafa za "tutabanana hapa hapa".