Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
-
- #221
Mkuu hakuna kitu kinaitwa UKATILI katika dunia ya ushindani. It's survival of the fittest. Mbona tulifahamu ya kuwa vita ya Kagera ingetugharimu lakini still tukaenda kupigana na Idd Amin? Huo unaouita ukatili ndio umewafikisha wazungu hapa walipo kiasi kwamba ukishindwa kuzungumza lugha yao kwa ufasaha unaitwa msamba/mbumbumbuhatujawahi kufikiria kufanya ukatili na unyama kwa viumbe ambavyo ni mfano wa watu weusi kasoro rangi.
@Then, what happened next? It looks like things have been turned upside downHistoria inasema watu weusi kabila ya Moors toka kaskazini mwa Afrika walienda Ulaya hasa Spain na kuwatwala wazungu.
Kuna methali ya Kiingereza inasema "Necessity is the mother of invention".Ina maana hatukuwa hata na sababu ya kwenda kwao kiunguzi tu !
Majibu mengi humu hayalidhishi. Hata vitabu vya Historia vinaanzia karne ya kumi na tano lakini bado mfano wetu na wa Wazungu haukuwa sawa na haukulingana. nafkiri tuendelee kufikirisha fikra mbona waarabu walifika katika kipindi cha nyuma zaidi kabla ya Wazungu kwa nini sisi tulikuwa nyuma ya jamii hizo kwenda kwao na kufanya kama wao walivyofanya? Vitabu vinasema walivyokuja ndiyo wameleta utegemezi kwetu mpaka leo na utajiri kwao mpaka leo kwa hiyo kwa namna zozote hata sisi tungekuwa na maarifa ya ku wawai kwenda kwao na kufanya walivyofanya kwa wakatu ule Africa ingekuwa tofauti( Kwa mawazo yangu).
@absolutely rightKuna methali ya Kiingereza inasema "Necessity is the mother of invention".
Ikimaanisha kwamba, uhitaji wa kitu ndio unamfanya mtu agundue vitu. Kama mtu hana uhitaji, kugundua vitu vipya kunakuwa haba sana.
Kwenye hii habari ya Waafrica kuna mengi.
AsanteSalamu zimefika 🤣
Nafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'. Huwezi kumlaumu mzungu ambaye alikuwa na utashi wa kutoka kwake kuja Africa kwa ground kuwa kwanini walikuja. Hapa ndiyo huo utashi unaouzungumzia unapoingia. Nafkiri utashi wa wazungu wa tangu1480's ndiyo unaoamua mambo mengi katika dunia hata leo. Kwa mfano hiyo entourage Mansa Musa kwenda Mecca na utajiri aliokuwa ungeweza kufanya maeneo yanayopatikana Mali (nchi) ya leo isiwe na matatizo iliyonayo leo. lakini yeye Mansa Musa utashi wake ulikuwa ni kwenda kuhiji akiwa na watu zaidi ya 1000 tena kwa kuzungukia Maurtania-Morroco-Tunisia mpaka Misri. Hapa inatupa pich ya utifauti wa utashi wa waafrica na wazungu tangu zamani.Kuna methali ya Kiingereza inasema "Necessity is the mother of invention".
Ikimaanisha kwamba, uhitaji wa kitu ndio unamfanya mtu agundue vitu. Kama mtu hana uhitaji, kugundua vitu vipya kunakuwa haba sana.
Kwenye hii habari ya Waafrica kuna mengi.
Africa ina land mass kubwa sana inland. Watu wengi walipotaka kupanua wigo wa makazi yao, walipanua wigo huo ndani ya Afrika bila kuhitaji kwenda nje. Hawakuhitaji kwenda nje kwa sababu walipata wanyama wa kuwinda, mifugo na mazao ya kilimo kwa urahisi ndani ya Afrika. Ukiangalia Bantu migration, na hata migration za watu wa Afrika kabla, utaona hili.
Bara la Ulaya licha ya kuwa halina hali nzuri sana ya hewa kwa maana ya kwamba lina baridi na vitu havioti mwaka mzima, na vinavyoota ni vichache, pia lina tabia ya kijiograpfia ya kutokuwa na hinterland kubwa sana, sehemu nyingi zipo karibu na pwani.Hili linachangia kuwafanya watu wajipanue makazi kwa kusafiri baharini, zaidi ya kujipanua makazi kwa kujikita bara.
Kuna hilo. Pia kuna la utashi. Wenzetu wana utashi. Wakiona mlima wanataka kuupanda.Sisi tukiona mlima tunausema ni makazi ya Mungu. Ukimueleza Muafrika wa asili habari ya wazungu kupanda milima, atashangaa sana, atauliza, kupanda mlima kunamsaidiaje? Wenzetu wanaona ni changamoto ya kuikabili na kuishinda. Wenzetu wanaishi kwa kutaka kuyapinda mazingira yaendane na wanavyotaka wao. Sisi tunaishi kwa kukubali kwamba inabidi tukubali mazingira yalivyo. Hili jambo linatakiwa kwa kuangalia pande zote mbili. Jamii inayosema inakubali mazingira tu inaweza kupata ugonjwa isitafute dawa, kwa sababu ugonjwa nao si sehemu ya mazingira? Unakubali tu. Lakini, jamii inayotaka kuyapinda sana mazingira kama dunia ya sasa ndiyo inatuletea mfumuko wa ma pandemic (kwa kupitia kirahisi utandawazi nasafari za ndege za watu wengi kimataifa), ma global warming na vitisho vya kumalizana pakubwa vita vya nyukilia.
Halafu pia, nafikiri, Waafrika wa asili walikuwa wanapenda jamii na familia zao sana, kiasi kwamba, kuondoka nyumbani kulichukuliwa kama utoro na kukosa mapenzi kwa familia au jamii yako.Wajibu kwenye jamii ulikuwa mkubwa sana, kiasi, kwenda mbali ilikuwa tatizo.
Kuna mfano wa Mfalme mmoja wa Mali ya kale, Mansa Aboubakar. Mansa Aboubakar (abdication 1311) alikuwa mfalme wa Mali kabla ya Mansa Musa. Na tunajua habari zake, kwa sababu, Mansa Musa - mtu anayehesabika kuwa tajiri kuliko wote waliowahi kutokea duniani- alivyokuja kuchukua ufalme baada ya Mansa Aboubakar, Mansa Musa alienda kuhiji Mecca. Kwenye safari hiyo, akiwa Cairo - ambapo alitoa sadaka ya dhahabu mpaka dhahabu ikashuka bei Cairo kwa miaka kadhaa - aliulizwa.Mansa Musa, ulipataje kuwa Mfalme wa Mali?
Mansa Musa akajibu. Akasema kabla yangu alikuwapo Mansa Aboubakar. Na Mansa Aboubakar kwa utashi wake mkubwa, alisema kwamba, kama unavyoona mto huu (Niger) una ng'ambo ya mbili upande huu na ule, hata ile bahari kubwa nayo (Atlantic) ukiivuka, kuna nchi upande wa pili vile vile. Akapakia mashua nyingi chakula, maji na dhahabu, akaenda safari, akaacha ufalme.Walipofika katikati ya bahari wakakutana na mawimbi makubwa sana, jahazi la mwisho likaamua kurudi kutoa habari kwamba Mansa Aboubakar amekwenda mbali sana mpaka bahari ya mawimbi makubwa.
Kuna habari kwamba Mansa Aboubakar alifika America kabla ya Christopher Columbus.
Lakini unajua nchini kwake Mali Mansa Aboubakar alichukuliwaje?
Alichukuliwa kama msaliti aliyekimbia kwao, akajiuzulu ufalme huku kawaacha watu wake. Kuna kitabu kinaandika majina ya Wafalme wa Mali.Kuna kipindi Mansa Aboubakar alifutwa, kwa sababu ya usaliti.
Sasa huyo mvumbuzi mwenye utashi wa kutaka kujua nchi nyingine zikoje, kaonwa msaliti!
Soma zaidi kuhusu Mansa Aboubakar hapa Abu Bakr II - Wikipedia
Tukiongelea falme, hapo tutaona uvumbuzi wa kwenda nchi za mbali unahitaji mitaji mikubwa inayoweza kukusanywa katika jamii zinazoishi katika nchi zenye serikali/ falme kubwa. Ndiyo maana wavumbuzi walioanza kuvumbua nchi za mbali za dunia, hata huko Ulaya, walitoka Uhispania, Ureno, Uingereza na Italy. Ni vigumu kusikia mvumbuzi wa kutoka Croatia.
Sisi hatukuwa na city states kubwa nyingi, na chache zilizokuwepo, zilifanya biashara na watu wa nje na kuanza kuvumbua kama huo mfano wa Mansa Aboubakar. Tatizo hatukuwa na moyo wa kuvumbua.Tuvumbue wapi na sisi tuliona dunia iko kwetu?
Kitu kingine, ikumbukwe kwamba Africa haikuwa na watu wengi sana mpaka miaka ya karibuni. Inakadirikwa kwamba, kufikia mwaka 1600, Africa nzima ilikuwa na watu milioni kama 55 tu. Hii ni sawa na idadi ya Watanzania tu leo.Ulaya, ambayo ni ndogo kulinganisha na Africa na haina maliasili nyingi, inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 1600 ilikuwa na watu milioni 78. Msongamano wa watu ni moja ya sababu zinazofanya watu waende kutafuta maisha pengine, Bila msongamano wa watu, ni vigumu watu kutafuta maisha sehemu nyingine.
Zaidi, ukisoma historia, ukatafuta utafiti wa kibaiolojia wa DNA diversity, utaona kwamba, watu karibu wote wa dunia hii, wametokea Africa. Sasa labda tulishafanya misafara ya mbali, tukaja kuona madhila yake, tukaamua kujisogetza polepole.
Mpaka leo kuna watu wengi tu Africa wana falsafa za "tutabanana hapa hapa".
Well saidNafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'.
Mansa Musa kasafiri unamlaumu, asingesafiri ungemlaumu kwa nini Waafrika hawajasafiri!Nafkiri aya ya sita inagusa kile nilichokuwa ninakiamini. ingawa wewe umesema utashi. Mimi nitaita 'akili'. Kwakweli, masuala au maswali kama haya yanayotugusa waafrika moja kwa moja kwamba kwanini tuko katika hali hii,watu wengi hata waandishi wengi wa Afro-Centric huweka 'blind eye'. Huwezi kumlaumu mzungu ambaye alikuwa na utashi wa kutoka kwake kuja Africa kwa ground kuwa kwanini walikuja. Hapa ndiyo huo utashi unaouzungumzia unapoingia. Nafkiri utashi wa wazungu wa tangu1480's ndiyo unaoamua mambo mengi katika dunia hata leo. Kwa mfano hiyo entourage Mansa Musa kwenda Mecca na utajiri aliokuwa ungeweza kufanya maeneo yanayopatikana Mali (nchi) ya leo isiwe na matatizo iliyonayo leo. lakini yeye Mansa Musa utashi wake ulikuwa ni kwenda kuhiji akiwa na watu zaidi ya 1000 tena kwa kuzungukia Maurtania-Morroco-Tunisia mpaka Misri. Hapa inatupa pich ya utifauti wa utashi wa waafrica na wazungu tangu zamani.
Ugundue tuna interest tofauti, we don't need to dominate wazungu in order to survive ujue.Mkuu hakuna kitu kinaitwa UKATILI katika dunia ya ushindani. It's survival of the fittest. Mbona tulifahamu ya kuwa vita ya Kagera ingetugharimu lakini still tukaenda kupigana na Idd Amin? Huo unaouita ukatili ndio umewafikisha wazungu hapa walipo kiasi kwamba ukishindwa kuzungumza lugha yao kwa ufasaha unaitwa msamba/mbumbumbu
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;
Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?
Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?
Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?
Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?
HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?
NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU
Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums
KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.
HAKUNA binadamu ambaye hapendi utajiri mkuu. Ndio maana hata mama muuza vitumbua akiuza idadi chache ya vitumbua vyake leo tofauti na idadi aliyouza jana roho yake inasononeka sanaWazungu waliondoa habari za kutaka kuishi kwa amani, wao kipaumbele chao kikawa kupata utajiri.Na ukiwa na mawazo hayo ndiyo unapata habari za kuafanya wenzako watumwa na makoloni.
@Hahahaaaaa. Hii nimeipenda sana mkuu. Asante sanaWatoto wa Kiitalia walikuwa wakideka na kujiliza baada ya vita hivi Wazazi wao waliwatishia jina la Huyu Jemedari Hannibal wakanyamaza mara moja - "Hannibal huyoo anakuja nyamazaaa".
Utajiri ni nini?HAKUNA binadamu ambaye hapendi utajiri mkuu. Ndio maana hata mama muuza vitumbua akiuza idadi chache ya vitumbua vyake leo tofauti na idadi aliyouza jana roho yake inasononeka sana
But our (African) survival largely depends on "Wazungu" domination. Wazungu wakisema wanatunyima misaada ya hali na mali, uonaona namna serikali za Afrika zinavyohaha kuomba msamaha ili kuendelea kupata ufadhili? Makomandoo wa Ufaransa waliingia Ivory coast kisha kumkamata Rais wao Bagbo, wakamtandika makofi ya uso kisha kumpeleka The Hague. Where was the African Union?Ugundue tuna interest tofauti, we don't need to dominate wazungu in order to survive ujue.
Sent using Jamii Forums mobile app
@Hapo kwenye neno dunia ulipaswa kusema neno wazungu kwa maana wao ndio waliovunja amani kwa kuwafanya waafrika kuwa watumwa kwa maendeleo yaoSwali la muhimu hapa ni, je, ingewezekana dunia kupata maendeleo ya kiuchumi bila amani kuvunjwa? Bila watu kufanywa watumwa na vita kubwa kufanyika?
Asante kwa hii point pia mkuu. Ila ninaomba uitolee ufafanuzi kidogo kama inawezekana. What did Fabius really do kubadili upepo wa vita?
@Scenario hii inategemea na ujasiri wa mtu. Mimi ninakwenda ila kuna mwingine hawezi kwenda hata ukimpa silaha.Ukiambiwa uende porini ambako kuna Simba wamejaa, ambako utaliwa na Simba, huna silaha wala nyenzo, ila kuna utajiri mwingi sana, ukienda utakufa, usipoenda utabaki na maisha ya hela ya kubadikisha mboga kila siku, hutakuwa tajiri, lakini hutakufa, utaenda?