A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Swali jingine linalofanana na hilo....ni kivipi Uingereza nchi ndogo iliweza kutawala karibu dunia nzima...Ni mind set au fikra..

Fikra za waafrika mpaka hatujaweza kutoka nje ya mipaka yetu...
 
Tatizo munasoma history ya darasani tu na kuona inatosha.
Kwanza kufanya mtu mtumwa haimaanishi ndo unaakili
Tumejenga pyramids kabla hata hatujawatumikisha waisrael kutoka Misri. Inamaana kabla ya kizazi cha yakobo.. waafrika tulishaweza kujenga pyramids of egypt.

Wazungu kukutana na waafrika sio suala la karene ya 15 (hii ni historia mbovu ya darasani)

Utawala wa kwanza Afrika ulikua wa mgiriki kabla ya kuzaliwa yesu... utawala uliofuata ulikua wa italy chini ya Kaisari na cleopatra na mwisho akaja mwarabu baadae baada ya yesu kuzaliwa ambapo tunaona watu kama kina Mansa Musa washaanza kukijenga chuo cha Timbuktu (chuo kikuu cha kwanza duniani) chuo ambacho kilianza kama madrasa kwa jengo moja
hadi majengo matatu makubwa.

Kingine... afrika tulishazunguka dunia nzima kama wazungu hawajaanza kutembea majini... Search Mandingo from mali
Mandingo walifika America kabla ya Christopha Columbas... kabla ya vasco dagama.
Mandingo wamefanya operation kwa kutumia misuli ya wanyama kama nyuzi

Rejea kwenye historia... mji wa kwanza na mtawala wa kwanza duniani anaitwa Nimrod.. nimrod alikua mweusi na ndiye mtawala wa kwanza wa sehem iliyoitwa Babeli... nimrod ni mweusi kwakua baba yake alikua ni Kush.. kush means black

kuna mambo mengi sana
ila waafrica au watu weusi tulishastaarabika..tulikua na akili... tulimiliki dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
Warabu wa Misri na Libya washakataa wao si waafrika, wapo wapo tu
 
Mkuu tunajibu ki-shabiki lakini swali lako la ki-falsafa sana, natamani nikujibu ila maelezo nimarefu sana.

Imagine phd holder wa kizungu yupo maabara anatafuta dawa ya COVID-19, Phd wa Tanzania yupo msitu wa pande anakata mizizi kujifukiza ili apone!

PHD Mzungu akigundua hiyo dawaa atauza dunia nzima, phd wa Tanzania akipona, hajui ni jani lipi limemponyesha, na hana cha kusaidia wengine!
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja kati ya waafrika wapumbavu ni wewe, mda hii unaingiza mambo ya kijinga. na nyie ndo mnafanya waafrika tufeli kila siku, usenge tu... Mods nipigeni ban nipo tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo mkuu. Hii mijitu kijinga sana. Kila wakati wanawaza siasa. Kila mmoja anaye sema kitu kizuri kwa serikali basi wanfikiria kuwa ni member wa CCM.

Sisi wengine hata hiyo katiba ya CCM yenyewe hatuijui. Jamani! Inakuwa shida kweli.

Japo kuwa nawaelewa kuwa wangetaka msuguano wa vyama vya kisiasa, lakini tatizo CCM hawana wapinzani. Mpinzani gani ambaye umebaki CHADEMA? Hakuna mtu huko. Wote ni, kwa kijerumani tunasema, "Sie sind Menschen, die ständig kiffen. Die Betonung liegt aber wohl am Kiffen."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali jingine linalofanana na hilo....ni kivipi Uingereza nchi ndogo iliweza kutawala karibu dunia nzima...Ni mind set au fikra..

Fikra za waafrika mpaka hatujaweza kutoka nje ya mipaka yetu...
Thanks. This is a very good question too
 
1.Technology-mzungu na muafrica walikutana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 15 wakati huo mzungu yupo mbali kidogo katika teknolojia mfano silaha hivyo tusingeweza kuwateka kama tungeenda

2.Umasikini -Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital sasa kwa mfano mkwawa angeweza ku finance jeshi lake kwenda Ulaya ?

3.Kutokuwa na Wazo hilo- Mu Africa hakuwa na wazo la kumtawala mzungu kama mtumwa kwa sababu wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule

4.SABABU ZA KIUTAWALA-Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kwa mfano Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya lakini huku kwetu tuliongoz kitemi kila kabila na mtemi wake hivo isingewezekana wote wakubaliane katika kwenda Ulaya na kuteka wazungu
uko sahihi pia historia inaonyesha wazi kuwa hao waingeleza walikuwa savages tu kabla ya mrumi kuwapelekea ustaarabu hivyo kwa stages nane za ustaarabu utumwa ni stage ya kwanza na unapojitambua ndio unaenda nyingine hivyo wao kuwaza kujitafutia watumwa ni kwa kuwa wao walipitia hiyo stage kabla yetu si kwa kuwa wana akili zaidi ila kwa kuwa bado hatujatoka kwenye hatua hii aya awali kuelekea hizo zingine ndo maana tunaona kuwa wao wana akili zaidi
 
Mkuu tunajibu ki-shabiki lakini swali lako la ki-falsafa sana, natamani nikujibu ila maelezo nimarefu sana.

Imagine phd holder wa kizungu yupo maabara anatafuta dawa ya COVID-19, Phd wa Tanzania yupo msitu wa pande anakata mizizi kujifukiza ili apone!

PHD Mzungu akigundua hiyo dawaa atauza dunia nzima, phd wa Tanzania akipona, hajui ni jani lipi limemponyesha, na hana cha kusaidia wengine!
Unasumbuliwa na upuuzi tu kwani phd holder wetu hahifadhi kumbukimumbu ya jani lililomponya?

Hao unaowasifu unadhani dawa wanazitoa mbinguni ama humo humo misituni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu safi sana hili
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani anasema walikuwa weusi?!

Sent from my TECNO-J5 using Tapatalk
Kuna watu hapa wanatudanganya kuwa ule ustaarabu wa Egypt midhali tu Egypt iko Afrika basi ulikuwa ustaarabu wa watu weusi. Ndio nikakumbusha kuwa Egyptian siku zote ni weupe, na ule ustaarabu waliutengeneza wao.
Weusi wako Sudani Kusini na mambo yao tunayaona yanafanana tu na ya weusi wengine duniani.
 
Unasumbuliwa na upuuzi tu kwani phd holder wetu hahifadhi kumbukimumbu ya jani lililomponya?

Hao unaowasifu unadhani dawa wanazitoa mbinguni ama humo humo misituni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama PhD yupi wa kwetu aliyewahi kufanya hivyo?
PhD za kiafrika zina mwisho wa aina mbili:
1. kupata title ya 'Dr' ili aitumie kugombea uongozi wa kisiasa au ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya, mkoa, RAS etc
2. kufanya kazi university na kuchapisha machapisho mengi kwa mtindo wa kachumbari (hebu google publications za profesa mmoja wa bongo umjuaye halafu uziorodheshe zote, kisha ondoa jina la author uulize mtu yeyote kuwa huyu aliyeandika machapisho haya ni mtaalamu wa nini? Hutapata jibu kwa sababu ni kachumbari! Publications za kudandia!). Halafu anakuwa profesa hadi anastaafu kisha anarudi namba 1 hapo juu (siasa) au anarudi kijijini kulima na kunywa ulanzi na wasiosoma (hadi wanashangaa kasoma nini sasa!)
 
Kuna watu hapa wanatudanganya kuwa ule ustaarabu wa Egypt midhali tu Egypt iko Afrika basi ulikuwa ustaarabu wa watu weusi. Ndio nikakumbusha kuwa Egyptian siku zote ni weupe, na ule ustaarabu waliutengeneza wao.
Weusi wako Sudani Kusini na mambo yao tunayaona yanafanana tu na ya weusi wengine duniani.
Hadi karne ya 16 nchi za kiafrika kusini mwa Jangwa la sahara,zilikuwa na majanga matupu mpaka pale zilipofikiwa ama na waarabu, washiraizi au wazungu.

Nakumbuka utawala wa kilwa, na tawala nyingi za pwani ziliwahi kupata ustaarabu kwa maingiliano na wageni, lakini makabila ya Interior ilikuwa majanga matupu.
Kuna mitaa huko bara hadi leo watu wanaamini mtu mweupe ni Mungu au malaika fulani hivi, na ako tayari kutowa loloto ili kupata baraka zake.
 
Kama PhD yupi wa kwetu aliyewahi kufanya hivyo?
PhD za kiafrika zina mwisho wa aina mbili:
1. kupata title ya 'Dr' ili aitumie kugombea uongozi wa kisiasa au ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya, mkoa, RAS etc
2. kufanya kazi university na kuchapisha machapisho mengi kwa mtindo wa kachumbari (hebu google publications za profesa mmoja wa bongo umjuaye halafu uziorodheshe zote, kisha ondoa jina la author uulize mtu yeyote kuwa huyu aliyeandika machapisho haya ni mtaalamu wa nini? Hutapata jibu kwa sababu ni kachumbari! Publications za kudandia!). Halafu anakuwa profesa hadi anastaafu kisha anarudi namba 1 hapo juu (siasa) au anarudi kijijini kulima na kunywa ulanzi na wasiosoma (hadi wanashangaa kasoma nini sasa!)
Hatareeeeeee
Hii ni kweli bila mawaa
 
Kwanza kabisa wazungu hawajatuletea dini. Tulikuwa na dini kabla hawajafika kwetu.

Pili, Waafrika hawakuwa na haja ya kwenda Ulaya kwa sababu waliridhika na neema nyingi za bara lao. Wakina Vasco da Gama wameondoka kwao kutafuta vitu ambavyo kwao havioti, wa Afrika hawakuwa na sababu ya kwenda Ulaya. Waliridhika na maisha yao.

Tatu, hizo habari za kumfanya mtu mwingine mtumwa zinaweza kuwa na manufaa kwa mtu mwenye akili fupi. Kwa kipindi kifupi. Maendeleo yanayotegemea utumwa ni maendeleo yasiyo sustainable. In the long run, jamii zilizoendekeza itumwa ama zilianguka (Rome) au ziliacha utumwa (Marekani).

Ndiyo maana watu wenye elimu wamepiga marufuku utumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana hatukuwa hata na sababu ya kwenda kwao kiunguzi tu !
Majibu mengi humu hayalidhishi. Hata vitabu vya Historia vinaanzia karne ya kumi na tano lakini bado mfano wetu na wa Wazungu haukuwa sawa na haukulingana. nafkiri tuendelee kufikirisha fikra mbona waarabu walifika katika kipindi cha nyuma zaidi kabla ya Wazungu kwa nini sisi tulikuwa nyuma ya jamii hizo kwenda kwao na kufanya kama wao walivyofanya? Vitabu vinasema walivyokuja ndiyo wameleta utegemezi kwetu mpaka leo na utajiri kwao mpaka leo kwa hiyo kwa namna zozote hata sisi tungekuwa na maarifa ya ku wawai kwenda kwao na kufanya walivyofanya kwa wakatu ule Africa ingekuwa tofauti( Kwa mawazo yangu).
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?

NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.
Kwanza nianze kwa kukataa kwamba walishindwa, sababu ni kuwa watu weusi hawajawahi kujaribu wakashindwa na hatujawahi kufikiria kufanya ukatili na unyama kwa viumbe ambavyo ni mfano wa watu weusi kasoro rangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom