Kama maswali yameisha nitaendelea na sehemu ya pili
A NIGHT INSIDE BUDDHIST COLLEGE
Binadamu ni mtu anayependa uhuru na ukimchunga atatafuta mbinu ya kuwa huru
Ndani ya kile chuo tulichungwa sana na kama ikitokea umekamatwa umetoroka adhabu yake ilikuwa ni kufukuzwa chuo moja kwa moja
Hatukurusiwa kuvaa nguo zetu za nyumbani kila kitu kilikabidhiwa na kufungiwa store siku tulipowasili na tukapewa hayo manguo ambayo ndio ilikuwa 24/7 tunayavaa popote tulipokuwa (tulikuwa na pair mbili)
Chuo kilikuwa kilometer moja kufika mjini na nusu kilometer kufika barabara kuu
Chuo kilizungushiwa ukuta wa matofali na fence ya umeme na security lights lakini pia mijibwa mikali yenye roho mbaya sana
Wanachuo walilala floor ya chini na ya pili na mamaster floor ya tatu kwahiyo kama ungetaka kutoroka usiku ilibidi ufanye yafuatayo
- utaimu mijibwa ikiwa haiko upande wa mabweninini
- mtu akusaidie kuzima umeme kwenye fence
- ufanikiwe kuruka ukuta wa mita tatu bila kishindo na bila kuyastua makubwa huko yaliko
-ufanikiwe kuvuka security lights bila kuonekana na mamaster ghorofa ya tatu
-kisha utambae kwenye majani umbali wa nusu km mpaka kufika barabara kuu ndio unakuwa salama
Ukikaribia barabara kuu unavua manguo ya kibuddha ndani una T-shirt na jeans na kapelo na raba (nguo hizi zilikuwa zinafichwa mbali sana)
Unaingia mjini unafanya yako halafu wakati wa kurejea hali ni ileile, yani ilikuwa ukirudi bwenini salama unamshukuru Mungu na kujiapiza kuwa hutotoroka tena
Hii inanikumbusha kwa asilimia moja (1%) tu ya maisha yangu ya JKT (Makutupora - Dodoma). Sasa nyie watawa ni nini hasa kilichokuwa kinawasukuma kwenda mjini? Ni ngono, mziki, hewa ya mafuta ya magari, au nini?