A day in the Buddhist college

A day in the Buddhist college

Kama maswali yameisha nitaendelea na sehemu ya pili

A NIGHT INSIDE BUDDHIST COLLEGE
Binadamu ni mtu anayependa uhuru na ukimchunga atatafuta mbinu ya kuwa huru
Ndani ya kile chuo tulichungwa sana na kama ikitokea umekamatwa umetoroka adhabu yake ilikuwa ni kufukuzwa chuo moja kwa moja
Hatukurusiwa kuvaa nguo zetu za nyumbani kila kitu kilikabidhiwa na kufungiwa store siku tulipowasili na tukapewa hayo manguo ambayo ndio ilikuwa 24/7 tunayavaa popote tulipokuwa (tulikuwa na pair mbili)
Chuo kilikuwa kilometer moja kufika mjini na nusu kilometer kufika barabara kuu
Chuo kilizungushiwa ukuta wa matofali na fence ya umeme na security lights lakini pia mijibwa mikali yenye roho mbaya sana
Wanachuo walilala floor ya chini na ya pili na mamaster floor ya tatu kwahiyo kama ungetaka kutoroka usiku ilibidi ufanye yafuatayo
- utaimu mijibwa ikiwa haiko upande wa mabweninini
- mtu akusaidie kuzima umeme kwenye fence
- ufanikiwe kuruka ukuta wa mita tatu bila kishindo na bila kuyastua makubwa huko yaliko
-ufanikiwe kuvuka security lights bila kuonekana na mamaster ghorofa ya tatu
-kisha utambae kwenye majani umbali wa nusu km mpaka kufika barabara kuu ndio unakuwa salama
Ukikaribia barabara kuu unavua manguo ya kibuddha ndani una T-shirt na jeans na kapelo na raba (nguo hizi zilikuwa zinafichwa mbali sana)
Unaingia mjini unafanya yako halafu wakati wa kurejea hali ni ileile, yani ilikuwa ukirudi bwenini salama unamshukuru Mungu na kujiapiza kuwa hutotoroka tena


Hii inanikumbusha kwa asilimia moja (1%) tu ya maisha yangu ya JKT (Makutupora - Dodoma). Sasa nyie watawa ni nini hasa kilichokuwa kinawasukuma kwenda mjini? Ni ngono, mziki, hewa ya mafuta ya magari, au nini?
 
mbimbinho chi gong ni nguvu inayotoka tumboni/ kitovuni, wale waimbaji wazuri hutumia koo na tumbo kutoa sauti zao na zina tofauti
kuna connection kubwa sana kati ya mind na chi gong, ukijifunza tai chi movement zake ni za taratibu mno lakini lakini zilizobeba uzito mkubwa
angalia mapigo mawili ya tai chi na karate/kung fu/judo
ukipanga tofali 3 ukampa mtu wa karate/judo au kung fu azivunje atavunja zote tatu lakini ukimpa mtu wa tai chi avunje atakuuliza unataka avunje ipi au ngapi na atafanya hivyo


love it
 
Hii inanikumbusha kwa asilimia moja (1%) tu ya maisha yangu ya JKT (Makutupora - Dodoma). Sasa nyie watawa ni nini hasa kilichokuwa kinawasukuma kwenda mjini? Ni ngono, mziki, hewa ya mafuta ya magari, au nini?

Hahhahaaaaa kwanza Kifyatu mwanadamu, huwa hapendi kuchungwa na ukifanya hivyo atatafuta uhuru kwa njia azijuazo mwenyewe
Lakini pia South Africa ni mji uliojaa starehe za kila aina...kwasisi ilikuwa ni kama kwenda kupata ladha halisi ya maisha tuliyozoea nyumbani Tanzania... You know sort of....mziki kidogo, chupa kidogo, tundi kidogo, nyama kidogo...na cha kushangaza zaidi uwezo wa kuruka mitego yote ya chuo utoke na kurudi salama kwakuwa ilikuwa ni jambo gumu mno kutoka na kurudi salama
 
Last edited by a moderator:
Naam! mshana jr uwe unanitag.
Mambo yangu haya

Tutaendelea na simulizi

IBADA ZA AJABU/ ZA KUSHANGAZA

Mojawapo ya ibada za kushangaza sana ilikuwa ni ibada ya kuchoma pesa!!!hili lilifanyika kwa siri mno na hata kwa wanachuo ni wachache sana tuliokuwa tunalifahamu hilo

Kwenye Synagogue la kibuddha/Temple kulikuwa na shrines 3
Ya kwanza ilikuwa mbele ambapo sanamu kubwa la Buddha mkuu liliwekwa likiambatana na essence burner, candles na Sutra

Madhabahu ya pili ilikuwa nyuma kulia ikipambwa na sanamu la kuan yi pusa mishumaa na nyudi na vitambaa vya rangi nyekundu.. Huku ilikuwa ni kwa kuomba baraka

Madhabahu/shrine ya tatu ilikuwa nyuma kushoto ikipambwa na sanamu kubwa la bodhisattva mwenye mikono elfu moja, nyudi mishumaa maua na vitambaa vya njano,.huku ilikuwa ni kuomba kuondokana na mikosi mbalimbali na ibada za vifo zilifanyika upande huu
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona CHAKRA au SUTRA imeingia, witnessj. LOL

I am sorry, I am just messing around.

Lakini kwa kweli mkuu mshana jr nimelipenda hili bandiko lako. Mimi nimejifunza the philosophical approaches za dini zote hapa duniani kutoka Atheism mpaka Zoroastrianism. Lakini sijaingia kwenye mambo ya jikoni ya hizi dini isipokuwa UKRISTU, UISLAMU, na UYAHUDI. Kwa hiyo nimefurahi sana ulipofungua ka-mwanya kadogo sana katika hii imani ya BUDDHISM.

Sante.
Kifyatu. Ha haa haa we kweli kifyatu!
 
Last edited by a moderator:
Naomba na mie unitag, huko majukwaa mengine unakopost mada zako bado sijaomba kibali.
 
Hapa naona CHAKRA au SUTRA imeingia, witnessj. LOL

I am sorry, I am just messing around.

Lakini kwa kweli mkuu mshana jr nimelipenda hili bandiko lako. Mimi nimejifunza the philosophical approaches za dini zote hapa duniani kutoka Atheism mpaka Zoroastrianism. Lakini sijaingia kwenye mambo ya jikoni ya hizi dini isipokuwa UKRISTU, UISLAMU, na UYAHUDI. Kwa hiyo nimefurahi sana ulipofungua ka-mwanya kadogo sana katika hii imani ya BUDDHISM.

Sante.
Kifyatu. Haa haaa haa we kweli kifyatu!
 
Last edited by a moderator:
go on broda tumejifunza kitu, si kila ukionacho chafaa kwa matumizi
 
Baba pale uliposema kuwa unamiliki silaha umenipa ukakasi kidogo,iliwezekana vipi kwenye chuo chenye sheria kali kama ulivyotanabaisha.

Ni kweli kabisa lakini ilikuwa kwa njia haramu na hata waliokuwa wanajua hili ni watanzania wasiozidi watatu
 
Mshana jr,hii habari ina sisimua ,navuta picha nakosa majibu!,napata maswali yanayeyuka,
Swali la kwanza,uhusiano wa mabudha na ushetani upoje?
 
Mshana jr,hii habari ina sisimua ,navuta picha nakosa majibu!,napata maswali yanayeyuka,
Swali la kwanza,uhusiano wa mabudha na ushetani upoje?

Ubudha si ushetani lakini pia hauna Uungu ndani yake
Unajua kuna shetani(ibilisi) na Lusifer hawa wawili wote ni roho walioasi toka mbinguni
Shetani ndiye aliyemdanganya(kumwambia ukweli? )hawa Kisha akalaaniwa
Lucifer yeye alitaka kuwa kama Mungu yaani apate mamlaka na uwezo wa kimungu! Lakini akashindwa na kutimuliwa mbinguni

Kwahiyo Shetani alilaaniwa na kufukuzwa kutoka Eden lakini Lucifer yeye hakulaaniwa bali allifukuzwa toka mbinguni....kufika huku duniani shetani akawa ni roho kamili ya ibilisi inayodanganya na kupotosha watu
Lakini Lucifer yeye akachukua umbo la mwanadamu na kuendelea na mkakati wake wa Kupata uwezo na akili zaidi Ili Amfikie Mungu ndipo hapo synagogue la kwanza la luceferianism lilianzishwa na as time goes on wakatokea kina Illuminati Freemasons Buddhism confuscious nknk
 
Back
Top Bottom