Naona hatimaye mnafarakana wenyewe!,poleni sana ndugu na karibuni katika ulimwengu huru!
sasa ni nani asiyejua kama dini zipo siku nyingi ingawa zingine ni za juzi juzi?ina maana wewe ndio hicho hicho unachokijua kuhusu dini?
Inamaana na wewe ulichokieleza kuhusu dini ndiyo hicho hicho?
uelewa wako wa hizi dini unanipa mashaka makubwa,haya ndio matatizo ya kurithi dini bila kujua chochote kuhusiana na hizo dini matokeo yake ndio haya....
Unaona sasa tatizo la kujadili mada bila ushahidi? Nakwambia mtume alivunja masanamu yote we unasema mtume aliabudu sanamu.
Mbona unachepusha maandishi yangu ? Wapi nimeandika mtume wenu aliabudu sanamu ?
Mtume wenu alimkarabati Allah aliyekuwa anaabudiwa na Makuraish na kumfanya ndiye mnaye Mwabudu nyini, huku mahala pa ibada na namna ya kuabudu mkirithishwa.
Kila andishi langu unalipotoa ili kukwepesha mjadala.
Nasisitiza wakati wa makuraish, Makkah kulikuwa na Wakristo na Wayahudi walimwabudu Yhwh na Makuraish wakiendelea kuabudu miungu yao, alichofanya Muhammad ni kukarabati miungu ya Makuraish na kutumia mungu wa makuraish (Allah) katika Dini yake mpya (Islam)
Nilijua lazima utakuja na maelezo kama hayo...maana wewe ndiyo umekuja kusema hizi dini ni utumwa, nikakwambia dini zipo kila mahali na hazijaanza jana wala juzi. Sasa unapokuja kuniuliza mie kama hicho hicho ndicho nachojua kuhusu dini unategemea nikujibu vp swali kama hilo?
Unakataa maneno yako sasa?
Haya tumalize ubishi mkuu,naomba uniambie Mtume muhammad alipokuwa akiwalingania watu kwa siri hapo mwanzoni kabla uislamu haujawa na nguvu, alikuwa akiwalingania jambo lipi hapo makka ambayo ibada yao ilikuwa ni kuabudu hayo masanamu?
Achana na hayo ya Muhammad kuwalingania nini ? Issue ni kuwalingania kuhusu Allah. Hivyo ilikuwa ni kuabudu Allah yule yule kwa mtindo mpya
sasa unataka kusema kwamba uislamu au ukristo ulikuwepo Afrika kabla hawajaja Waarabu au Wazungu?labda tuanzie hapo kwanza
Suala si nani kaleta dini afrika dini zimepelekwa na zipo kila mahali,we eleza huo utumwa wa dini ni upi?
Tatizo umeanza tu na suala la makka kuabudu masanamu ila haujaeleza ni vp hayo hiyo ibada ya masanamu ilianza vp wala hujaeleza historia ya dini za waarabu,hivyo swali langu unapaswa kujibu kuwa mtume alikuwa akiwalingania nini tena kwa siri? Maana mtume alikuwa akiwalingania watu kuacha kuabudu masanamu maana ndiyo ilikuwa ibada ya kuabudu masanamu,na ndiyo maana mwanzoni alianza kulingania kwa siri hadi baadaye ndipo alipoanza kulingania kwa uwazi. Sasa unapokuja na kusema mtume alikarabati sanamu ndiyo napokuuliza sasa alikuwa akilingania nini wakati wote huo?
Dr. T. V. N. Persaud ni Profesa wa Anatomia (sayansi inayohusu mwili na viungo vyake jinsi vilivyo, Profesa wa Matibabu ya watoto na magonjwa yao (Pediatrics) na Afya ya Mtoto, na Profesa wa Ukunga, Jinakolojia (Elimuuzazi), na Sayansi ya mambo ya Uzazi katika Chuo Kikuu cha Minatoba, Winnipeg, Manitoba, Kanada. Hapo, alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia kwa miaka 16. Yeye ni mashuhuri katika uwanja wake. Yeye ni mwandishi au mhariri wa vitabu 22 na amechapisha vitabu zaidi ya tafiti 180 za kisayansi. Mnamo mwaka 1991, alipokea tuzo ya kipekee kabisa iliyotolewa katika uwanja wa Anatomy huko Kanada, J.C.B. Grant Award kutoka katika Chama cha wana-Anatomia wa Kanada. Alipoulizwa juu ya miujiza ya kisayansi katika Qur- aan ambayo aliifanyia tafiti, alisema yafuatayo: Namna nilivyoelezwa ni kwamba, Muhammad alikuwa mtu wa kawaida. Hakuweza kusoma, hakujua (namna ya) kuandika. Kwa kweli, alikuwa asiyejua kusoma. Sisi tunazungumzia kadiri ya miaka elfu moja na mia mbili [kwa kweli kadiri ya miaka elfu moja na mia nne] iliyopita. Unamkuta mtu asiyejua kusoma na kuandika akitoa matamko na kauli zenye maarifa mengi na cha ajabu ziko sahihi kuhusiana na sayansi. Mimi binafsi yangu, sioni ni vipi hii inawezaje kuwa ni bahati nasibu tu. Kuna mambo mengi sana ya
uhakika na, kama Dr. Moore, sioni tatizo katika fikra zangu kuwa hii msukumo au uhusiano utokao kwa Mwenyezi Mungu ndio uliomwongoza yeye atoe kauli hizi.
Profesa Persaud amejumuisha baadhi ya Aayah za Qur-aan na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya vitabu vyake. Pia aliziwasilisha Aayah na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) katika mikutano kadhaa wa kadhaa.
Huo ni mfano mmoja tu wa maelezo ya wanasayansi kuhusu jambo hili,sasa wewe unayesema ni jambo la kawaida tu toa maelezo na si kuacha jambo kama lilivyo.
Ni sawa na kuambiwa chumbani kwako kuna nyoka halafu ukasema utalala hotelini halafu ukaita huo ndiyo ufumbuzi wa hilo tatizo badala ya kwenda kumtowa huo nyoka.
Basi wewe nithibitishie haya:
Nijibu kwanza hayo ili mimi nibadili mtazamo.
- , Mungu yuko wapi?????
- Ni jinsia gani???
- Ni mfano wa nani, mzungu , mwafrika, muhindi , mchina, mwarabu??????
- Kwanini aumbe dunia tu, hizo sayari nyingine zilikujaje??????
- Biblia iliandikwa na nani?????
- Mtu akifa anaenda wapi????? ni vizazi vingapi vimepita hadi sasa mbona havifufuki??????
Vizuri umeanza kwamba Nachokiamini wewe.
Kila mtu huamini apendacho vile vile huwezi kuniambia vyote viaminiwavyo ni kweli/sahihi. kwa mantiki hiyo huna uhakika unachokiamini wewe ni sahihi or nnachokiamini mimi sio sahihi. Mimi nimewekq fact kwamba hicho mnachokiamini wakiristo na waislamu sio sahihi.
Once again vizuri ulivyorest your case ila hiyo ni mbaya kwa lishe ya ubongo wako.
Yesu alisali kwa Mungu yupi ikiwa naye ni Mungu? Kunamiungu mingapi? Au unapingana na biblia iliposema Yesu ni Mungu?
Kwani mimi dini gani?
Jee unamanisha kila mtu anaamini dini?