A God can be a mere theory, nothing more

A God can be a mere theory, nothing more

Mkuu nafurahishwa unaposema umefanya tafiti, ila usisahahau hata mende kule chooni anakoishi alifanya tafiti na kwa vipimo vyake aliridhika na kuona ni mahali poa pa kuishi.

Hoja zako ni za kizamani, wazungu waliwekeanaga hizo miaka ya 1300, mfano hoja ya soul and human nk. hata nyingine zilifanyiwa majaribio. Ukiona mwanasayansi anang'ang'ana sana na kukana uwepo wa mungu ujue huyu ni outdated scientist, kwa sababu hayo malumbano yalikufa baada ya wanasayansi kukubali kuwa there power working beyond nature ( invisble power). hii ilitokana na ishu zilizotokea kama vile za mama mmoja aliyedai kubakwa na mtu ambaye hakuna aliyeweza kumuona, na baadaye kuwekwa chini ya ulinzi na maafisa wa polisi, wanasaikolojia, madaktari na wanasayansi wengine, akalazwa sehemu ya wazi na ulipofika muda yule mama akapiga kelele za kuingililiwa huku washuhudiaji wakiona kana kwamba anapambana na kitu ila hawakioni na baadaye kupanua miguu kulia lia na kuacha baada ya muda, walpoenda aliponyamaza wakakuta kuna mbegu, madaktari wakachukua na kupima wakaona ni mbegu za kiume, huo si ushuhuda wa wanadini ni wanasayansi, wanadini wakaelezea kirahisi tuu kwamba kuna ulimwengu wa roho wenye kuchukua maumbo mbalimbali, huko kuna wa Mungu na wa shetani, hiyo ni miaka ya 1980 na ushee. ok. Na matukio mengine mengi tuu

MUHIMU; mimi mesoma kozi ambazo zinakataa kabisa uwepo wa Mungu, lakini kila niliposoma na kufananisha facts nikakubali kwamba dini zina branders nyingi sana ila uwepo wa Mungu hauepukiki hata kama vitabu havijandika kwa usahihi au kikamilifu kabisa kuhusu MUNGU, ni kweli katika dini kuna tamaduni nyingi tuu, ila haiondoi juu ya uwepo wa Mungu, mimi kozi yangu jambo la kwanza kabisa ni kukataa uwepo wa Mungu, ila ndo mekuwa na imani kupitiliza.

Mawazo unayotumia kuchalenji uwepo wa Mungu, yanafunua mawazo mapana uliyonayo kwa upande mmoja na pia yanafunua uchanga katika baadhi ya hoja ulizoweka hapo juu. Binafsi meona kuna maswali ambayo ni very challenging na hayajibiwi na brabra, mfano, sawli juu ya Mungu kupanga kila kitu, ni swali ambalo halihitaji mtu akurupuke kujibu, kweli ni swali tata. Mkuu complex matters should be dealt with complex minds, and I think in one or another you've tried, still I remind you that, the way we count ourselves to be complex, is the same as the white-ants count themselves to be more complex only because they are capable of building the ant-hills.
  • Umejenga mawazo ya kupinga dini, afu unasema watu huweza kupata ule uwezo kwa kusali...vip?



  • Mimi nakubali kuwa kuna mambo yanayoonyesha kuchanganya katika vitabu vya dini na huenda binadamu katia utundu sana, ila hilo haliondoi uwepo wa Mungu. Mfano sisa ni chanzo cha migogoro mingi na maafa yasababishawayo na binadamu, hilo pia halifuti ukweli kwamba siasa ni kichocheo cha maendeleo.
  • Mkuu usidharau yaliyoandikwa vitabuni yote kwa ujmla wake, mi mepokea changamoto yako ya vitabuni,nawe pokea ya kwangu. mkuu kitabu kama biblia kimeandikwa miaka 560 kabla ya Kristo, na moja ya maandiko yake ambayo ni kama mepesi sana kinasema, Adamu aliumbwa kwanza afu Hawa akatolewa toka kwa Adamu; miaka zaidi ya 2000 baadaye yaani 1800 na ushee, hiyo sayansi unayoiamini ikaja na jambo jipya lilifanyiwa tafiti na kuhakikiwa, juu ya vinasaba, (genes-by Gregory Mendel), ikaonekana mbegu ya mwanume inakuwa na jinsia mbili zaq kusabibisha uhai kwa kiumbe kipya yaani XY na yai la mwanamke lina XX, ambapo X toka kwa mwanume ikiungana na X toka kwa yai la mwanamke tunapata mtoto wa kike na Y toka mwanaume ikiungana na X toka yai la mwanamke anazaliwa mwanaume. Huoni kwamba wazo la biblia ni sahihi sna maana katika mbegu za mwanaume kuna ukike, yaani ndani ya adamu kuna ukamilifu wa mwanadamu?
  • Kuna theory inayojaribu kutafuta asli ya binamu pamoja na evelution n.k, yenyewe imejikita kuangalia kama wote tulizaliwa tokea kwa mama mmoja, inaitwa eve hypothesis, hii ilipelekea kufanyika kwa utafiti wa kisayansi wakipima mitochondria DNA, ambayo hiyo hurithishwa kwa mtoto toka kwa mama tuu maana baba haitoi kwend kwa mtoto, utafiti ulifanyika kwa kuchukua makundi ya watu maelfu kwa maelfu kwa minajiri ya maikinga kinga haya n.k watu toka amerika, ulaya, australia, asia na afrika, na walizingatia jamii kama wachina waarabu wahindi, wazungu wa aina mbali mbali yaani wekundu sana weupe sana macho ya brown, blue na white na waafrika aina mbalimbali pia, ule utafiti ulibaini kwamba wote tuna mitochodria DNA tuliyonayo ina asili ya mwanmke mmoja mweusi kwa rangi maana walipima vinasaba vya rangi ya ngozi mifupani mwao. WEWE UTEGEMEAYE SAYANSI HUONI KUWA HILO LINARUDIA YA KWAMBA SISI NI WATOTO WA MWANMKE ATWAYE HWA, YAANI MAMA WA WOTE WENYE MWILI. Biblia ilandika hayo miaka ya 560 kk, utafiti ni 1959.


  • Afu mkuu vitabu vinasema binadamu aliumbwa akawa umbo safi kisha akapuliziwa pumzi, ni siku ya binadamu huyu kufa, tunaona ile ile pumzi ya kwenye vitabu ndio inayotoewka, vipi hapo?



  • vitabu vinasema, "SIKU MOJA BINAMU ATAKUFA", MBONA IMEONEKANA WOTE TU WANYONGE JUU YA HILI NA KIFO NI SYSTEM INGAWA HATUPENDI. Ingekuwa ni nature tuu tungetokea watu wa asili mbalimbali yaani wengine wangefikwa na umauti wengine wasingefikwa, yaani ukiona hutaki jambo na unatendeshwa, basi ujue akutendeshaye ni mtawala wako, kumbuka mtumwa na bwana wake enzi hizo au wewe na serikali, kwani wewe uliwahi kuiona serikali sehemu yoyote, maana waziri mkuu husema serikali imeamua, rais serikali itatenda, mbunge ni jambo la serikali, kiongozi kafungwa jela na chombo cha serikali, swali, serikali ipo au hamna?



  • Afu mkuu sehemu uliyoonyesha uchanga, kudai dini na biblia vimeletwa na wazungu, hapana, wazungu wamepokea dini toka mashariki ya kati, na walipinga kwa upanga na kwa hoja kuliko wewe, wakijiweka chini yake, wakapata siri nyingi za jinsi ya kuitawala dunia kwa kutumia vilivyomo, baada ya kufaidika nayo wameona leo hii wewe nawe utajua kuwa ni sawa na wao basi wanakuandikia vitabu vya kuipinga nawe unapokea kana kwamba wao ni miungu, wao wakizidiwa na jambo utawasikia my God, na huku wakisari mpaka kesho,wew huku wankwambia udharau ili usikutane na nguvu za Mungu. waulize wasayansi kama kekule n.k

Understanding of a person in the invisible matters is very limited as well as the understanding of a mosquitoes to the things done by humans. Kwa mafano leo hata MBU wangepewa akili za kuelewa vitu, wasingefaulu kuelewa sawasawa habari na shughuli za mwanadamu kama zilivo, hii ingetokana na vitu kama vile;
  • Udogo wa umbo lake,
Yaani yeye maisha yake yaweza hata kufanyika kwenye kofia ya binadamu, hivi huyu asingekuwa na uwezo wa kumjua binadamu na vitu vyake kama tujuavyo sisi, kwa sababu hiyo, tungetofautiana katika tafsiri ya mlazi, yaani kwetu kama vile nyumba n.k, yeye mbu angetoa tafsiri ambayo kwetu sisi ingekuwa na vichekesho sana, maana malazi yake yangeweza kufanyika hata katika soksi yako.


  • Urefu wa maisha yake (life span)
Mbu huishi siku saba tu, hivo tutafautiana sna katika jambo la kuhesabu miaka , miez hata masaa maana yeye ndani ya siku saba katotolewa, kakua, kama kwa binadamu yaani kabalehe, baadaye katengeneza familia na akazeeka kisha akafa. Sasa huyu ukimwambia mimi ntakuja mwezi ujao, kwake is more than impossioble, na milele yake inaanzia siku 9 na kuendelea.


  • Shughuli zake,
Mbu naye ana mafanikio yake kwa muda alioishi, na kwake masaa in relation to its life span huhesabia dakika kama miaka kdhaa. Kutokana na hilo amezuiliwa kuelewa mabo mengi sana, ila kwa yeye anajihesabu kwamba ana teknolojia ya hali ya juu ya utafutaji ridhiki kama vile kufanya mbinu mbalimbali za kuzama ndani ya net na kunyonya damu, hujidhania ana uwezo mkubwa wa kufanya mambo asijue kuwa anajilinganisha na uwezo wake tuu hivyo huweza kumkwepa binadmu kwa kuikimbilia kwenye kiatu chake binadamu, na kwa kuwa binadamu hajamjali sana pindi atokapo salama kwenye kiatu huenda kuwapa elimu watoto wake juu ya njia salama ya kumwepuka binadamu kwa mafanikio, ni kuingia kwenye pango kubwa mno ambalo ni mali la asili (natural cave)

  • Mbu hajui kuwa pango asemalola asili ni kiatu alichoteneza binadamu, mbu huweza hata kuvuka mipaka kwa kutangaza kuwa huyo binadamu si lolote maana sasa mbu wamepata maendeleo, ya kuweza jificha kwenye mahandaki, wasijue kuwa kumbe wameingia kwenye sikio la binadamu, maskini mbu hawajui binadamu huyu akienda kuonga ni sunami na wanafagiwa wote, afu hawajui kuwa wakimwudhi binadamui watangamizwa kabisa kwa sumu n.k.


  • Lakini kule katika jamii yao huenda mbu wana mikutano yao na namna ya kuongazana na kufanya mambo yao kikamilifu, afu kutokana na mbu kujuana vyema juu ya mbo yao yanayoendelea kila siku katika jamii yao, wana wakati wa neema na wakati wa taabu, hivo a binadamu napopulizia dawa kama Rungu n.k, wao huomboleza vifo na kusema huyo tunaedai kuwa mwanadamu hana lolote ni kwa nini asingeingilia maafa yetu, au la hayupo kabisa ni hadidhi hadithi tu za uzushi. Masikini, mbu hawa hawajajiuliza huo uchungu wa kifo chao binadamu anaguswa kwa kiasi gani, na je mbu wote wakiamua kutoambatana na binadamu na pia wasiaamini kama binadmu anaishi je inamwasili nini binadamu. Ila binadamu anatoa ridhiki kubwa tu kwa mbu, kuanzia vitu atumiavyo, mwili wake yeye n.k
  • Mbu hamjui binadamu jinsi alivyo,
Mbu hamfahamu binadamu kama wewew unifahamuvyo mimi, au kuijua nyumba yako kama uijuavyo wewe, kutokana na umbo na upokevu wa akili yake. akitoka mtaa mmoja hadi mwingine toka saa 1:30 hadi saa 2:00 asubuhi basi hujigamba kwamba alienda nchi ya mbali sana, na hata pindi arudipo ndugu zake humshangaa kwa kuwa amebadilika umri, yaani amekuwa, kwingine jiongeze. Mbu hajui hata kidogo mambo ya siasa, utamaduni, uchumi na kijamii ya binadamu.
  • Hilo ndo jambo lilifanya Mungu ajitambulishe kwa watu kutokana na uelewa wetu, yaani leo hii ukienda kumfundisha uchumi sisimizi inabidi ulenge shughuli zake ili ujumbe ufike, usije ukaanza kumwambia '' ooh! unajua mimi nilipopata masters ya business administration" na brabra hawataelewa kwa sababu kila kitu kinahitaji difinition ni kigeni kabisa kwao.


  • Akili ya binadamu yafanya kazi kwa uzoefu wa matukio aliyoyapata kwa kupitia milango mitanmo ya fahamu,
Hivyo ni rahisi sana kuelewa vile tuu vilivyo ndani ya akili na upeo wake tuu. Kwa mfano, binadamu wa miaka ya 1200 iliyopita hata ungekuwa na uwezo wa namna gani usingeweza kumwelezea akaelewa juu ya teknolojia kama ya simu ya wire, na hii ya mkononi au tv n.k, na lolote amb alo ungemweleza angebisha sana sana kwa sababu asingeweza kuelewa yale ambayo wewe unamweleza hata kama ni ukweli kwa kua hana upeo nayo na hayaingii akilini maana akili hujifunza yale tu yafafanayo na kilichomo kichwani mwake.​

  • Hebu chukulia jamii moja ya viumbe itokee duniani na kudai haya maghorofa, nyumba hizi magari simu ni kazi ya nature,
Watakuwa na jambo moja la kujiuliza kama wana akili, hivi hii nature imeweka mlango wa kuingilia na kutokea, garini, bomba la moshi, krachi, breki, kiti cxha dereva na sponchi la kuegemea n.k, hivi hii nature mbona ni so systematic, hebu chukua hilo na la binadamu.​

  • Umbile la binadamu;
Binadamu alivyoumbika tuu, ni ushahidi tosha kwamba kuna kitu chenye uelewa na plani kabisa maana kimepanga kila kiungo kwa binadamu kuwa na kazi yake, tazama, matako kwa kukalia yametiwa sponchi, mgongo for upright, pua, viungo vya uzazi linafanyika jambo afu maendeleo yanatokea kisha mtoto attokea pale kwenye ule upenyo n.k, wanyama pia. Sasa tunachofanya wanadamu ni kama vile magari yapewe pumzi afu yadai yenewe ni kazi ya nature bila kujiangalia jinsi yalivyo kimaumbile yaani yanamfaa binadamu


  • Kumbuka expire date ya vitu;
​Binadamu hutengeneza kitu afu akaweka siku ya kuisha ubora afu pia huelekeza jinsi ya kutunza ubora huo, ukikosea basi huaribika kabla, sasa hatulioni la Mungu na binadamu, yeye katuumba na katuelekeza jinsi ya kuishi na kwamba one day tuta expire na ataamua kutufanya kitu kingine, sisi tunabisha, yaani ni sawa na tomato inayobisha kuexpire kwake afu inasema kwa aliyeitengeneza huwezi kunibadili kunifanya bidhaa nyingine kama vile mbolea n.k ha ha ha ha ha !!! binadamu duuu!

MKUU HOJA ZAKO NI NYINGI NA LAZIMA ZIJIBIWE KIKAMILIFU, MMIMI NAISHIA HAPA. TAFAKARI NAMI NATAFAKARI ZA KWAKO.
 
Nimekuuliza biblia ni nini? maneno ya nani na kwa misingi ipi? umeshindwa kujibu. Sasa unataka mimi nifanyeje hapo. embu chukulia mimi sijui lolote kuhusu biblia sasa wewe unanipa somo. teh teh teh!!!
Mashaxizo kuna andiko niliandika kuwa katika hoja zako unaonesha uko underage au ni impaired reasoning, wewe umeandika hutaki bla bla kwa kutumia bla bla. Nimekujibu uondoe bla bla ndiyo uje na maswali yenye mashiko.
Najua biblia ni nini, Biblia ni maktaba ambayo ndani yake kuna vitabu vilivyoandikwa na watu zaidi ya arobaini wakiwa na uvivio wa Roho wa Mungu.
Biblia imegawanya katika vitabu vilivyokusanywa pamoja kuwakilisha Agano la kale na vile vinavyowakilisha Agano jipya.
Kuhusu Agano la kale na jipya nilikwisha kukupa jibu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa Quran imesema hivyo. na hiyo ni sababu nyengine ya mimi kuchopoka huko.


Nakuelewa vizuri Tz mbongo. wewe tu hutaki kunielewa. Ok hapa nadhani nimeshakujibu dai la kisayansi kutokana na uwepo wa theory nyingi za kisayansi zilizotolewa na watu tofauti kabla ya kuproviwa miaka hii. Nadhani tuko pamoja hapo.

Qurani si Maneno ya Mungu na ikiwa ndio basi yamechanganywa na maneno ya watu waongo na wasioweza kufikiri sawa sawa!!!!! sadly Quran yenyewe imejieleza kwamba mle hakuna neno ata moja la mtu or kitu chengine chochote.

Kwa maana hiyo ule uongo na unreasonableness vilivyo mle ni vya Mungu mwenywewe. Narudia tena kutokana na hayo ndio nimechopoka huko coz Mungu hawezi kuwa na udhaifu huo. Usiniulize udhaifu gani coz nimeelezea huko juu na nikakuuliza but hukutaka kunijibu kwa madai kwamba tujadili whether ni maneno ya Mungu or ya mtu. ok. mimi nakuelewa vizuri tu.
Na hapa najikita kwenye hilo.

Qurani si maneno ya Mungu coz Mungu hakukishusha hiko kitabu bali Muhammad ndie aliekuwa akiongea na maswahaba wakaandika. So ikiwa unaushahidi kwamba Maneno hayo hayatoka kwa Muhammad naomba uweke huo ushahidi.

Hoja no: mbili.

Ukitoa ushahidi wa maneno kutoka ktk Quran yenyewe unijbu pia ikiwa Mungu ni unreasonable na pia unijibu ikiwa Mungu anaweza kusema uongo. coz hata hivyo vinapatikana kwenye Quran hiyo hiyo.

Ukijadiliana na mie usiwe na haraka mkuu,haujajibu swali langu lakini nashangaa unasema umejibu kwa kueleza habari za Gravitation.

Swali ni kwamba Mtume muhammad aliwezaje kujua mambo ya kisayansi hali ya kuwa hakuwa mwanasayansi wala hata kusoma hakujua, ni mambo ambayo wanasayansi zama hizi wametumia vifaa vya kisasa kujua hayo mambo?

Kutoa mfano wa Isaac inakuwa bado haujajibu swali hata kidogo inakuwa umeacha hoja hewani. Jibu swali nawe utajibiwa maana maswali yako mengine yanategemea muafaka wa hoja hii.
 
Kweli hiyo? Nakumbuka Musa naye kwn biblia alipewa amri ya kuuwa hadi watoto,inaelekea naye alikuwa anataka kwenda mbinguni.

Yes, maanan mwisho ni kwenda kwake! Mungu anajua yote in advance, kwa hiyo alikuwa anajua atakachopkifanya Musa, alikuwa ana maana gani kumwambia hivyo!
 
Hahahahahaaaaa! Kumbe ni she!!!

Ivi Nkwesa kule niliongelea utofauti na ufanano wa Yese na Issa or wa Uislamu na Ukiristo?

Uliongelea similarities na differences za Wakristo na Waislam kuhusu Yesu/Issa huku ukiweka mambo yanayoshabihiana kuwa ni makubwa na yanayotofautiana kuwa ni minor. Nikakukumbusha kuwa kutojua kwako imani ya Kikristo ndiko kulikufanya ufanye hitimisho ambalo ni la MTU asiyejua.
Mimi ni He sijui umekula maharage ya wapi mkuu
 
Nkwesa Makambo means Nvuta Bangi....kavutishwa bangi ya ulokole huyu-na kalewa hasa pasi na kuelewa chochote,..anakwenda kwenda tu kama ling'ombe.

Ni miongoni mwa makondoo ya Gwajima huyo.
IGWE utwa masiku gwe ntuta ugwe !
Nimevutishwa kweli kweli
 
Last edited by a moderator:
Naona umeshindwa kuthibitisha..hapo makka watu walikuwa wakiabudu masanamu na ndiyo wakawa wameweka hao masanamu 360 ndani ya Al kaaba, Mtu alipofanikiwa kuuteka mji wa Makka akavuja hiyo misanamu.

Maelezo yako hayana uhalisia.
Tz mbongo unataka nikuthibitishie nini ? Hao masanamu waliitwaje ? Na kutokumjua Mungu kwa Muhammad ndiko kulimfanya amkarabati mungu wa makuraish na kuwapeni ninyi.
Allah ni mungu aliyekarabatiwa na Muhammad kwa kuwaondoa wasaidizi wake 360 na mabinti zake ili ampwekeshe.
Muhammad ndiye aliyemtengeneza Allah wenu ...
Na kaabah ndiyo sehemu takatifu ya Allah wenu na kila msalipo lazima muelekeze nyuso zenu kwenye madhabahu ya Allah ambayo ni kaabah yenye jiwe jeusi ndani.
Mnadanganywa ati kaabah ilijengwa na Ibrahim pasipo ushaidi wa kihistoria nanyi mnakubali tuu..
 
Last edited by a moderator:
Tz mbongo unataka nikuthibitishie nini ? Hao masanamu waliitwaje ? Na kutokumjua Mungu kwa Muhammad ndiko kulimfanya amkarabati mungu wa makuraish na kuwapeni ninyi.
Allah ni mungu aliyekarabatiwa na Muhammad kwa kuwaondoa wasaidizi wake 360 na mabinti zake ili ampwekeshe.
Muhammad ndiye aliyemtengeneza Allah wenu ...
Na kaabah ndiyo sehemu takatifu ya Allah wenu na kila msalipo lazima muelekeze nyuso zenu kwenye madhabahu ya Allah ambayo ni kaabah yenye jiwe jeusi ndani.
Mnadanganywa ati kaabah ilijengwa na Ibrahim pasipo ushaidi wa kihistoria nanyi mnakubali tuu..

Ukimaliza jazba njoo tujadili.
 
Last edited by a moderator:
Yes, maanan mwisho ni kwenda kwake! Mungu anajua yote in advance, kwa hiyo alikuwa anajua atakachopkifanya Musa, alikuwa ana maana gani kumwambia hivyo!

Lakini ndiyo kwa Amri ya Mungu pia Musa aliua wanawake, watoto na wakajichukulia mabinti bikra.
 
Huwezi kujadili kuhusu Allah na Muhammad akili yako imekatazwa tangia utoto unakaririshwa Tu. Unapenda ujadili kuhusu Yesu na Ukristo.
Kalagha bhaho....

Sawa.. ila wewe ukiona umemaliza jazba basi njoo tujadili mambo kwa ushahidi,aina ya majibizano bila ushahidi unayotaka wewe mie siyahitaji.

We umekaririshwa kwamba Malaika mkuu ndiyo aligeuka kuwa Shetani( Lucifa) hili ni jambo ambalo huwa linanishangaza sana.
 
Sawa.. ila wewe ukiona umemaliza jazba basi njoo tujadili mambo kwa ushahidi,aina ya majibizano bila ushahidi unayotaka wewe mie siyahitaji.

We umekaririshwa kwamba Malaika mkuu ndiyo aligeuka kuwa Shetani( Lucifa) hili ni jambo ambalo huwa linanishangaza sana.

Sina jazba kabisa, sina Shaka na ninachokiamini, hivyo ninaweza kutetea ninakiamini wakati wowote lakini pia sina hofu kuhusu chochote na yeyote katika mababa wa Imani na mitume sina Shaka na mienendo yao kwa kuwa walikiishi kile wanachokiamini hivyo hakuna hoja unayoweza toa Muislam wewe itayopunguza hadhi wala heshima zao.
Mimi nakuhoji kuhusu Allah na Muhammad kwa kuwa ndiyo wakuu wa Uislam.
Acha porojo toa hoja kujibu hoja sielewi unapodai ushahidi Una maana gani ? Wataka ushahidi gani kwa mungu wa kusadikika ?
 
Nimekusoma sana FATHER OF REALITY. Labda niseme tu kuwa NAAMINI MUNGU YUPO lakini sie huyu wa Quran, biblia wala mabudha. God kwa maana ya 'Super Natural Power' isiyo na pirika za kumtaka mtu aende kanisani wala msikitini.

Afu mkuu uo mfano wa mbu nimecheka sana. Coz it means vyovyote itavyokua mbu wengine wangekubali na wengine wangepinga. mara nyingi waumini mnapenda kusema Sijui akili za watu ni finite while God ni infinite. ikiwa ni hivyo tuseme waumini nao wana infinite mind?

Then mkuu umegisia suala la uumbaji wa binadamu hapo ukiuhusisha na science huku ukimfagilia Mungu. ivi unaongeleaje uumbaji wake wa dunia, other planets and galaxies?
 
Last edited by a moderator:
Tununu nnkamu gwangu,..Kyala ikutula mwalafyale,...Kyala ugwa kumwanya akusajege fijo nnkamu.

Malafyale sio mwalafyale nkamu. Ndagha fijo...
Mma nitike ulusajo ulu usumile kwa Kyala gwa Kumwanya.
 
Mashaxizo kuna andiko niliandika kuwa katika hoja zako unaonesha uko underage au ni impaired reasoning, wewe umeandika hutaki bla bla kwa kutumia bla bla. Nimekujibu uondoe bla bla ndiyo uje na maswali yenye mashiko.
Najua biblia ni nini, Biblia ni maktaba ambayo ndani yake kuna vitabu vilivyoandikwa na watu zaidi ya arobaini wakiwa na uvivio wa Roho wa Mungu.
Biblia imegawanya katika vitabu vilivyokusanywa pamoja kuwakilisha Agano la kale na vile vinavyowakilisha Agano jipya.
Kuhusu Agano la kale na jipya nilikwisha kukupa jibu.

Kabla ya kuendelea nini maana ya 'uvivio'?
 
Last edited by a moderator:
Ukijadiliana na mie usiwe na haraka mkuu,haujajibu swali langu lakini nashangaa unasema umejibu kwa kueleza habari za Gravitation.

Swali ni kwamba Mtume muhammad aliwezaje kujua mambo ya kisayansi hali ya kuwa hakuwa mwanasayansi wala hata kusoma hakujua, ni mambo ambayo wanasayansi zama hizi wametumia vifaa vya kisasa kujua hayo mambo?

Kutoa mfano wa Isaac inakuwa bado haujajibu swali hata kidogo inakuwa umeacha hoja hewani. Jibu swali nawe utajibiwa maana maswali yako mengine yanategemea muafaka wa hoja hii.

Hutaki tu tuelewane coz hutaki kujibu yale maswali.

Labda nikuulize. Jee wavumbuzi woote waliogundua vitu duniani wanajua kusoma na kuandika? Kusoma na kuandika kunasaidia nini kuvumbua kitu kipya? Hutaki kukubali kwamba kunawavumbuzi wasiojua kusoma na zaidi wa miaka hiyo. ukiwa unashindwa kujibu yale maswali basi.
 
Uliongelea similarities na differences za Wakristo na Waislam kuhusu Yesu/Issa huku ukiweka mambo yanayoshabihiana kuwa ni makubwa na yanayotofautiana kuwa ni minor. Nikakukumbusha kuwa kutojua kwako imani ya Kikristo ndiko kulikufanya ufanye hitimisho ambalo ni la MTU asiyejua.
Mimi ni He sijui umekula maharage ya wapi mkuu

Aisee! Ivi biblia inaruhusu uongo kama inavyowadanganya?
 
Aisee! Ivi biblia inaruhusu uongo kama inavyowadanganya?

Nimechoka kujadili nawe, impaired reasoning inaonekana katika kila andishi lako. Huo uwongo unaousema inakuwaje huuweki ? Umekaririshwa neno uongo wa kwenye Biblia huku huusemi uwongo wenyewe tuuone na sijui ni uwongo kwa kutumia kipimo kipi ?
 
Nimekusoma sana FATHER OF REALITY. Labda niseme tu kuwa NAAMINI MUNGU YUPO lakini sie huyu wa Quran, biblia wala mabudha. God kwa maana ya 'Super Natural Power' isiyo na pirika za kumtaka mtu aende kanisani wala msikitini.

Afu mkuu uo mfano wa mbu nimecheka sana. Coz it means vyovyote itavyokua mbu wengine wangekubali na wengine wangepinga. mara nyingi waumini mnapenda kusema Sijui akili za watu ni finite while God ni infinite. ikiwa ni hivyo tuseme waumini nao wana infinite mind?

Then mkuu umegisia suala la uumbaji wa binadamu hapo ukiuhusisha na science huku ukimfagilia Mungu. ivi unaongeleaje uumbaji wake wa dunia, other planets and galaxies?

Nimekusoma sana FATHER OF REALITY. Labda niseme tu kuwa NAAMINI MUNGU YUPO lakini sie huyu wa Quran, biblia wala mabudha. God kwa maana ya 'Super Natural Power' isiyo na pirika za kumtaka mtu aende kanisani wala msikitini.

Afu mkuu uo mfano wa mbu nimecheka sana. Coz it means vyovyote itavyokua mbu wengine wangekubali na wengine wangepinga. mara nyingi waumini mnapenda kusema Sijui akili za watu ni finite while God ni infinite. ikiwa ni hivyo tuseme waumini nao wana infinite mind?

Then mkuu umegisia suala la uumbaji wa binadamu hapo ukiuhusisha na science huku ukimfagilia Mungu. ivi unaongeleaje uumbaji wake wa dunia, other planets and galaxies?

Kuhusu uhusiano wa Mungu na binadamu, ndo nlitumia mfano wa mbu kuelezea, yani vitu vingi tunafahamu kwa limit yetu tuu, na hiyo ni asili, kwamba huweza kwenda mbali ya yale yanayokuzunguka. Huenda Mungu anavyjieleza au anavoelezewa na wanadamu ni tofauti kubwa mno. Hapana mkuu binadamu ni finite, hata wewe muumini wa nature unaliona wazi, ndo maana ya kugunduwa na kuboresha yaani ni alama ya kutokuwa wakamilifu, Mungu alipoumba dunia hajaimodify kwa kuiumba tena na tena ila dunia ni inclusive, power to modify it are on it.

Kuhusu maumbile ya ulimwengu (universe) bado point ni ileile yaani ukiangalia mambo yalivopangika, unaona kabisa kilichoyapanga hivo kina, kwa mafano akili, yaani akili kuliko sisi mbali mno, kama ni uwezo yaani ni uwezo kuliko sisi mbali mno mno, na jinsi binadamu tunavyojitahidi kufanya mabo kimpangilio kwa akili zetu tukija kufanya kautafiti kidogo tunajikuta sisi ni sehemu ndogo mno ya akili na uwezo uonekao kuwepo au kutututawala. Yaani ukianzia na mfumo jua, na ukadokezewa kwamba jua pamoja na kusapoti sayari zote hizi ikiwemo dunia bado ni mojawapo ya nyota, hivi sisi tunachokijua tena hatujafika 03% ni juu ya mfumo huu tunaoishi, sasa nyota zinakusanyika na kutengeneza galax which means millions of stars, hebu fikiri kama kila moja ina mfumo kama huu tuishio, afu hizo galaxies zinakusanyika pamoja na kufanya milk way zinaozunguka zote sasa, na distance from one star to the other is trililions and trililions that we failed tu use number we measure in terms of light years in which one minute as part of that light year consist of not more than 150 million kilometres.

Ndo mana watu wa dini, mfano mimi uwa nasema hivi kama katika mifumo hiyo kuna sayari na kuna viumbe basi sisi sio pekee wa kumtukuza Mungu, hata tukitia mgomo yeye Atatukuzwa, kumbuka msemo katika biblia, "wakinyamaza hawa basi mawe haya yatapaza sauti"

Hii mifumo utagundua kuwa imepangwa kwa kujua kwamba kila kilichomo kina kazi maalumu kwa uwepo wa mifumo fulani. hivi hujawahi kujiuliza je hiyo nature msemayo kama ina uwezo huo ni lazima iwe na ufahamu mkubwa sana, maana kwa mfano wake binadamu katengeneza maghorofa, magari, tvs, simu n.k kweli ni vitu complex sana, hebu chukua tu kwa kujifanya mjinga toka kitabu cha wakristo yaani biblia pale kisemapo Mungu alisema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu wakatawale dunia, huoni kuwa kuna ukweli, kwamba walau twafanana naye Baba yetu, maana Yeye aliumba vitu tokea vitu visivyoonekana, ok kwa yeye tuseme ni chanzo cha materials, sisi tumunda vitu hivyo hiyo tokea vitu visivyoonekana huoni hiyo pointi ina maana sana.

Mkuu ukitaka kujua haya mambo fuata wanadini ambao waweza kukuelezea Mungu nje ya Biblia na Koran au vitabu vingine, kwa mfano Wakatoliki wanatumia Biblia katika imani yao, lakini mafundishao yao ya msingi yanasema katika maandiko na mapokeo Mungu kajifunua kidogo sana, yaani katoliki wanasema Mungu ni mkuu mno haishii hapo tuu, ndiyo maana misingi ya katoliki hawa hukumu hukumu watu hovyo na kusema hawa motoni hawa motoni, kwa sabababu wanajua Mungu aliyetuumba anashughulika na viumbe wake kwa namna nyingi na za ajabu sana, hapo najibu lile swala la kujiona labda kutoamini hivi vitabu ni kama kuwa salama sana. kuna sheria ya asili lazima ushikamane nayo.

Hivi ulishawahi fikiri juu ya natural law ifanyavyo kazi ndani ya watu, uliwahi kufikiri juu ya world ethics similarlities na je ulishawahi kujiuliza juu ya cultural universality, HAVE YOU EVER ASKED YOURSELF ON THE UNIVERSALITY OF THE CONCEPT GOD, DO YOU THINK IT CAME IN HUMAN MIND BY CHANCE, AND IF SO HOW MANY WERE TO COME IN HUMAN MIND BY CHANCE, AND WHY NOT ALL BUT SOME OF THEM? Kwa hpa uwa nawapongeza na kuwakubali wakatoliki, katika kitabu chao kikuu cha mafundisho ya kanisa kifafanuacho maandiko na mambo ya MUNGU, wanasema, Binadamu ni kiumbe cha dini kwa asili yake, ila si dini fulni.

Uliobaki ni ukengeufu. Ukengefu ni kulazimisha kutoka katika asili, mfano ufiraji si sawa maana lile shimo ni kwa ajili ya haja kubwa, tumejuaje, asili imeonyesha shimo maalumu kama hakuna matatizo mengine huleta mazao yaani mimba na mwishowe kiumbe. Lakini watu hubadili asili kwa ukengeufu, kujichua, ushoga n.k, kipimo kisiwe mbona kuna raha, hapana si utaratibu, NDUGU AMINI TUNATAWALIWA, WE ITA VYOVYOTE NA ONE DAY UTATAKIWA UJIBU.
Kwa nini china kwa namna yao wazungumze habari za nadharia ya tumuitaye Mungu, Wanyakyusa, Wajerumani, Waingereza, Waskotlandi, Wanaigeria n.k, huoni kama ni asili ya binadamu, kwa nini watu wakatae kitu ambacho kimetokea kwote bila kupangwa.

Nakupongeza kwa kudai kuwa unamwamini lakini si huyu wamtangazaye hwa wakristo, waislamu, wahindu n.k, sawa sina tatizo, hebu jiulize, hivi kama tulikuta misitu, mito, madini, wanyama , jumla yake huitwa mazingira, na tunatakiwa tuyatunze kwa utaratibu ili vidumu na viwe katika ubora wake, na utaratibu huo ukiuchunguza hatupangi sisi ila sisi tunautafiti tu, yaani upo na haijarishi unajua au haujui, ukivunjwa mazingira yanaharibika, hiyo inaonyesha utwala mkuu wa aliyeviweka hivyo, afu kule kutafiti na nini, ndo kutawala ambako Mungu katuagiza.
Unafikiri binadamu atafanikiwa kujiita kiumbe huru asiishi kwa utaratibu, ukiuliza utaratibu huo atatoa wapi, ndo kuna maelekezo ya msingi na ya usawa ndani ya watu wote, hivi kwanini watu wanapiga debe kuhalalisha ndoa za jinsia moja, kwa nini, mbona hawaandamani kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia tofauti, ni asli, TUNATAWALIWA NA MWINGINE. Yani jambo hili kwa asili yake si sawa katika jamii za wanadunia. Evil is evil by itself and good is good by itself.

Sasa sisi wenyewe tunatawaliwa na huyo, MUNGU, alama yake ni kifo ambacho haijarishi umejifunza kutunza afya yako namna gani ni lazima ufe, sasa huyo mtawala kakuletea mwongozo hapohapo katika jamii yako yaani, jamii zote zina kataa wizi, dhuruma, uasherati kwa maana ya kwamba iwe ni kabila au nini, wana taratibu ya kuchukuana mtu mume na mke, yaani, MFANO, yule babu wa KIHAYA ambaye hakuwa mkristu wala mwislamu, alifuata taratibu ya namna ya kabila lake katika mambo mbalimbali alikuwa sahihi, na atamfikia Mungu.

Hiyo inatokana na concept of good and evil which is universal with the exception of the special circumstances, kwa mfano kwote duniani kuua ni jambo baya, sasa wale ambao walikuwa wanatolewa kafara kwa ajili ya wengine, katika maibada ibada, maana yake wachache wapate mabaya ili wengi wawe salama yaani wapate mazuri.

Tofauti imekuja kujitokeza pale tafri za maneno si dhana (si concempt) yenyewe juu ya zinaa, uasherati n.k. hivo wewe usifikiri upo salama kwa kuikataa Biblia au Koran, ishu ni kutenda mema na kukataa mabaya, watu wa namana yako wapo wengi tuu na wataingia mbinguni, yapi hayo, jamii imepewa, usiazime akili nyepesi ukafikiri kuchukua msichana au mvulana bila ya utaratibu limeitwa baya kwa sababu ya ujio wa hizi dini, la hasha, wale wameleta tafsri tuu, hilo ni baya tangu kabila lako, vivo hivyo, uwongo, fitina, wivu, uuaji, ulevi kupindukia uondoao utu wa mtu n.k, yaani kwa kifupi hiyo tuitayo mizimu sijui vibwengo, pia kuna mambo hawayataki, hujaona mtu anapoteza uganga kwa sababu amekuwa mzinzi.

Kwa sisi tuaminio vitabu hivi, mfano katika Biblia inasema katika warumi, wale wote waliokosa pasipo sheria watahukumiwa pasipo sheria, maana wana sheria iliyoandikwa ndani ya mioyo yao, YAANI ILE DHAMIRI NJEMA, ikiwaelekeza yapi mema na yapi mabaya. Hini la dini ipi bora na brabra ni la juzi juzi tuu, katika uwepo wa nguvu za uovu na wema ,ndipo palipolazimu hitaji la kujua maovu yapo chini ya nani na mema yapo chini ya nani, mbona mambo haya ni kama vivuli tuu, hivi hatuoni kuna mkuu wa jeshi la polis, na pia kuna magenge ya wahuni yakiwa na kiongozi mkuu, mbona vitu vya dunia twaweza kuvielewa kirahisi. HIYO NI VISIBLE WORLD WHICH IS THE EXEMPLARY OF THE INVISIBLE ONE.
Ok niishie hapo.


 
Back
Top Bottom