Dr. T. V. N. Persaud ni Profesa wa Anatomia (sayansi inayohusu mwili na viungo vyake jinsi vilivyo, Profesa wa Matibabu ya watoto na magonjwa yao (Pediatrics) na Afya ya Mtoto, na Profesa wa Ukunga, Jinakolojia (Elimuuzazi), na Sayansi ya mambo ya Uzazi katika Chuo Kikuu cha Minatoba, Winnipeg, Manitoba, Kanada. Hapo, alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia kwa miaka 16. Yeye ni mashuhuri katika uwanja wake. Yeye ni mwandishi au mhariri wa vitabu 22 na amechapisha vitabu zaidi ya tafiti 180 za kisayansi. Mnamo mwaka 1991, alipokea tuzo ya kipekee kabisa iliyotolewa katika uwanja wa Anatomy huko Kanada, J.C.B. Grant Award kutoka katika Chama cha wana-Anatomia wa Kanada. Alipoulizwa juu ya miujiza ya kisayansi katika Qur- aan ambayo aliifanyia tafiti, alisema yafuatayo: Namna nilivyoelezwa ni kwamba, Muhammad alikuwa mtu wa kawaida. Hakuweza kusoma, hakujua (namna ya) kuandika. Kwa kweli, alikuwa asiyejua kusoma. Sisi tunazungumzia kadiri ya miaka elfu moja na mia mbili [kwa kweli kadiri ya miaka elfu moja na mia nne] iliyopita. Unamkuta mtu asiyejua kusoma na kuandika akitoa matamko na kauli zenye maarifa mengi na cha ajabu ziko sahihi kuhusiana na sayansi. Mimi binafsi yangu, sioni ni vipi hii inawezaje kuwa ni bahati nasibu tu. Kuna mambo mengi sana ya
uhakika na, kama Dr. Moore, sioni tatizo katika fikra zangu kuwa hii msukumo au uhusiano utokao kwa Mwenyezi Mungu ndio uliomwongoza yeye atoe kauli hizi.
Profesa Persaud amejumuisha baadhi ya Aayah za Qur-aan na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya vitabu vyake. Pia aliziwasilisha Aayah na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) katika mikutano kadhaa wa kadhaa.
Huo ni mfano mmoja tu wa maelezo ya wanasayansi kuhusu jambo hili,sasa wewe unayesema ni jambo la kawaida tu toa maelezo na si kuacha jambo kama lilivyo.
Ni sawa na kuambiwa chumbani kwako kuna nyoka halafu ukasema utalala hotelini halafu ukaita huo ndiyo ufumbuzi wa hilo tatizo badala ya kwenda kumtowa huo nyoka.