The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Huenda nisimwelewe au kumfahamu vizuri Mungu nnayemwamini, na huenda nikawa na maswali mengi kuhusu huyu Mungu nnayemwamini kuliko haya ya ndugu yangu Mashaxizo ila hayo yote hayajawahi kunishawishi niamini kwamba Mungu hayupo.
Pili, misingi ya imani ya Ukristo na Uislam iko tofauti sana mkuu licha ya baadhi ya mambo kuwepo kwenye Quran na Biblia takatifu. Mfano, kwa imani yangu Kifo cha Yesu na kufuguka kwake ndio msingi na nguzo ya imani yangu ya ki Kristo wakati Quran inapinga kufa kwa Yesu.
Hoja ya dini kuja kwa lengo la kututawala, Je, hizi dini zililetwa Afica tu na haziko huko kwa hao waliotutawala? na siku hizi hazipo tena huko kwa sababu lengo lao lilikua ni kututawala ambapo kazi ya dini itakua imemaliza umuhimu wake?
Na kwanini tuhoji kwamba kwanini Mungu anaacha mabaya au maovu yatokee kana kwamba tunataka huyu Mungu afanye kazi kama tunavyotaka sisi wanadamu? Ni sawa na wewe unapesa zako umeamua kuwekeza kwenye miradi ya aina flani na kununua gari za aina unayoitaka wewe kisha mtu mwingine ambaye hata hajui wewe unapanga kitu gani na aanze kukukosoa kwamba haufanyi sawa kisa, haujafanya kama anayofikiria yeye wewe unaweza kufanya.
Nimependa kichwa cha hii habari kwamba "...can be a mere theory...." ikimaanisha inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo.