Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yah ni kweli ulivyosema.
I mean dini na madhehebu yake.
Ni kweli haiwezekani dini zote zikawa sahihi,kwahiyo zipo dini ambazo si sahihi na ipo dini ambayo ndiyo sahihi.
Kwahiyo uwepo wa dini nyingi na kila moja kudai ndiyo sahihi haifanyi kutokuwepo kwa dini sahihi yenyewe, hata hao wanaosema hakuna mungu huofautiana kwa mambo mengi tu.
Ok. Sasa je, ni ipi dini sahihi?
Zaburi 14:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu
Ok. Sasa je, ni ipi dini sahihi?
Sahihi ni ile ambayo nabii au matukio yake yamethibitishwa na wanatafiti wa historia iwe ni wana dini au sio wanadini....
Hapo sasa Panahitaji kuwe na vigezo ambazo vitatumika kujua ni ipi dini sahihi.
OK. Bila shaka utafiti huo umeshafanywa.
Wapo wanahistoria ambao wamefanya utafi huo na kugundua uwepo wa Mungu eg: Thomas Aquiras na wengineo wengi. pia kunawanahistoria waliogundua dini ya kweli, hapa kila dini imawanahistoria wake wanaokubali dini fulani ni sahihi, = Ukiristo umesjibitishwa kwamba ni dini sahihi pia Uislamu umethibitishwa hivyo hovyo.
Mpaka hapo ithibati zimefanywa but inawezekana vipi uislamu iwe dini sahihi na ukiristo uwe hivyo hivyo?
Pia kunawanahiatoria wengi tu waliofanya utafiti na kugundua hakuna Mungu wala dini sahihi. eg Thomas hobbes na wengineo wengi.
Ikiwa issue ni utafiti wa wanahistoria mbona kuna majibu tofauti na yamayopingana juu ya tafiti hizo?
Kupitia majibu ya wanahistoria unachanganya na zako na kuangalia maandiko husika ndipo unajua iliyokweli.
Mimi ni mkristo na world view yenye mashiko ni Ukristo hasa kwa maisha, kifo na kufufuka Historical Jesus
Chukua majibu ya wanahistoria changanya na zako mkuu
Wewe ni unahisi ni vigezo gani sahihi vitakavyoweza kutujulisha dini fulani ni sahihi?
Hilo swali na tuliangalie kupitia no. 2 kwenye mada. No. mbili inaongelea uingizwaji wa dini (ukiristo na uislamu huku Africa hasa Afrika mashariki. Iko wazi kwamba dini hizo zililetwa na Wakoloni na waarabu ambao walikuja kututawala na kutufanya watumwa as a result tumekua nchi tegemezi hadi leo.
Jee dini sahihi inaweza kuletwa na madhalimu?
Swali lako kuhusu vigezo ni kwamba kwa mimi ninaweza nikatoa vigezo ambavyo kwa mtu asiye amini ktk dini vikawa havimgusi,hivyo ningependa viwe vigezo ambavyo hata asiye amini ktk dini naye akapata cha kujifunza tofauti na mtazamo aliyonao hivi sasa.
Swala la pili ni suala la kihistoria zaidi si kirahisi kama unavyoeleza wewe, lakini kwanza tujue ni ipi dini sahihi kabla ya kujua afrika dini ziliingiaje.
Ok. ni vipi vigezo vya dini sahihi?
Unaposema ukiristo ni world view yenye mashiko unamanisha nini? mbona hiyo theory ya kufa na kufufuka ipo hata ktk uislamu?
Jee unaweza kuwa specific kidogo kwanini ukiristo ni dini sahihi? coz nahisi ukishikilia world view yenye mashiko tu huo ni ububusa.
Ninachokitaka ni kwamba tujadiliane pamoja si suala la mimi tu kutaja hivyo vigezo kwa sababu tutaanza kubishana kuhusu hivyo vigezo.
Kitu cha kwanza, Kama kushikilia world view yenye mashiko ni ububusa basi kujadili nawe ni ububusa zaidi.
Pili nimekwambia World view ya Kikristo tangu uumbaji, kuzaliwa kwa Bwana Yesu, mafundisho ya Bwana Yesu na namna alivyo yaishi Yale aliyoyafundisha na kufundisha Yale ambayo aliyaishi kiasi kwamba lawama pekee alizopata kutokana na maisha na matendo yake ni uoga wa watawala juu ya namna alivyopata wafuasi wengi watiifu na waaminifu kwake.
Kufa na kufufuka kwake ndiko hasa kunako nipa tumaini juu ya maisha yangu haya na yale ya baada ya kifo.
Katika Uislam theory ya kufa na kufufuka inahusu nani na alikufa lini na kufufuka lini ?
Nnaposema ububusa hapo namanisha ni ile hali ya kuingia ktk hiyo imani kwasababu ya kukubalika kwakwe world wide bila ya wewe kuwa na specific reasons.
Pili kuzaliwa, alivyoishi na hayo mengine hapo ukitoa mafundisho (ambayo yako kwenye biblia) wewe uliyajuaje? lengo la kuuliza hivyo ni kutaka tu kujua kwamba yote ulioongea hapo yanatoka kwenye biblia or kuna na source nyengine ili tuwe specific na kitu tunachojadili.
Hivyo hivyo ilivyokwenye biblia kuhusu Yesu ni hivyo hivyo kuhusu Issa ktk uislamu kunatofauti ndogo tu ambazo sio main key yetu hapa.
Kwamba kule ni Yesu huku ni Issa.
Kule alisulubiwa na kufa siku 3 na kufufuka huku hakusulubiwa wala hakufa.
Kule Mungu huku Nabii.
hizo ndio tofauti.
Uwiyano.
Miaka.
Alizaliwa na Maryamu.
Hana baba.
Alifanya miujiza.
Alikwenda mbinguni na atarudi.
Mashaxizo kupitia tofauti hizo ukijibidisha kuzitafutia majibu zinaweza kukuongoza kufikia pahala ambapo unaweza kutambua nani ameandika uongo say kuhusu Yesu Kristo Kati ya Biblia na Quran then utakuwa umeanza safari na kuendelea na safari ya kuchuja hadi ubakie na itayostahili kwa vigezo vya wazi.Nnaposema ububusa hapo namanisha ni ile hali ya kuingia ktk hiyo imani kwasababu ya kukubalika kwakwe world wide bila ya wewe kuwa na specific reasons.
Pili kuzaliwa, alivyoishi na hayo mengine hapo ukitoa mafundisho (ambayo yako kwenye biblia) wewe uliyajuaje? lengo la kuuliza hivyo ni kutaka tu kujua kwamba yote ulioongea hapo yanatoka kwenye biblia or kuna na source nyengine ili tuwe specific na kitu tunachojadili.
Hivyo hivyo ilivyokwenye biblia kuhusu Yesu ni hivyo hivyo kuhusu Issa ktk uislamu kunatofauti ndogo tu ambazo sio main key yetu hapa.
Kwamba kule ni Yesu huku ni Issa.
Kule alisulubiwa na kufa siku 3 na kufufuka huku hakusulubiwa wala hakufa.
Kule Mungu huku Nabii.
hizo ndio tofauti.
Uwiyano.
Miaka.
Alizaliwa na Maryamu.
Hana baba.
Alifanya miujiza.
Alikwenda mbinguni na atarudi.