A God can be a mere theory, nothing more

Huenda nisimwelewe au kumfahamu vizuri Mungu nnayemwamini, na huenda nikawa na maswali mengi kuhusu huyu Mungu nnayemwamini kuliko haya ya ndugu yangu Mashaxizo ila hayo yote hayajawahi kunishawishi niamini kwamba Mungu hayupo.

Pili, misingi ya imani ya Ukristo na Uislam iko tofauti sana mkuu licha ya baadhi ya mambo kuwepo kwenye Quran na Biblia takatifu. Mfano, kwa imani yangu Kifo cha Yesu na kufuguka kwake ndio msingi na nguzo ya imani yangu ya ki Kristo wakati Quran inapinga kufa kwa Yesu.

Hoja ya dini kuja kwa lengo la kututawala, Je, hizi dini zililetwa Afica tu na haziko huko kwa hao waliotutawala? na siku hizi hazipo tena huko kwa sababu lengo lao lilikua ni kututawala ambapo kazi ya dini itakua imemaliza umuhimu wake?

Na kwanini tuhoji kwamba kwanini Mungu anaacha mabaya au maovu yatokee kana kwamba tunataka huyu Mungu afanye kazi kama tunavyotaka sisi wanadamu? Ni sawa na wewe unapesa zako umeamua kuwekeza kwenye miradi ya aina flani na kununua gari za aina unayoitaka wewe kisha mtu mwingine ambaye hata hajui wewe unapanga kitu gani na aanze kukukosoa kwamba haufanyi sawa kisa, haujafanya kama anayofikiria yeye wewe unaweza kufanya.

Nimependa kichwa cha hii habari kwamba "...can be a mere theory...." ikimaanisha inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo.
 
Mashaxizo unaelekea kuwa ATHEIST taratibu na nilikuwa naliona hili kila nikikusoma......mtihani huu unao alafu nina hakika DINI yako hujaisoma vilivyo unaisomea mitandaoni ukichanganya ni twist za atheists wengine wamekuweza.....

POOR YOU...

unahitaji msaada mkubwa wa kuondokana na hili UNAWEZA KUNI PM nikusaidie
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mashaxizo ingekuwa vizuri kama ungejaribu kutaja vigezo ambavyo kwako unaona ni muhimu kwa kutambua dini iliyosahihi.

1- Mungu ni mjuzi/anajua yote. Akisema uongo huyo hajui anachokiongea so huyo si Mungu.

2- God is reasonable one. akiact or kufundisha unreasonably huyo si Mungu.

3- Mungu hana ubaguzi na anapenda watu wote. akifanya kinyume huyo si Mungu.

4- Ni hakimu wa haki. akifanya kinyume huyo si Mungu.

5- Sheria za Mungu yanakwenda na wakati na kutekelezeka, ikiwa kinyume huyo si Mungu.

Kwa mtazamo wangu ni sifa hizo kuu.
 
Last edited by a moderator:

Then tunaambiwa mtume aliuita mwezi na kuugawa ukawa vipande viwili kwenye viganja vyake, infact wanauchulia mwezi kama mpira wa netball. then tunaambiwa Mungu kapanga kila kitu but ujinga unaendelea duniani haambiwi yeye ni source. watakao kwenda mbinguni na motoni tunaambiwa ameshawapanga.

Yaani hizi dini zinauongo kiasi kwamba hata uyo Mungu kama yupo, huko aliko anacheka sana!!!
 
Yawezekana ukawa sahihi, ila ukumbuke hata sie tunajazana makanisani na msikitini ila wengi wetu hatuna ufahamu na MUNGU tunayemwabudu.

Na huo ndio ukweli tumeadopt hako kamchezo tulikoletewa na wakoloni na wale waliotuuza.

Then nimegundua wale wasiojua maandiko ndio wanaimani sana.
 
..then tunaambiwa Mungu kapanga kila kitu but ujinga unaendelea duniani haambiwi yeye ni source. watakao kwenda mbinguni na motoni tunaambiwa ameshawapanga.

Yaani hizi dini zinauongo kiasi kwamba hata uyo Mungu kama yupo, huko aliko anacheka sana!!!

Naona umeushtukia uongo uliopo kwa jina la imani.

Hapa utaelewa kwa nini saa nyingine mtu unaona unyamaze tu, watu wakishavaa jezi ni ligi na ushabiki.
 
Tatizo lako ni kwamba unatumia logic kwa mambo mabayo yanataka Metaphysical approach ili kuyaelewa.Ukitumia logic kwenye mambo ya kiimani ni sawa tu na kumbiza kuvuli chako mwenyewe....utapoteza muda tuu na hutapata majibu ya kufaa!

Kwaiyo mkuu unataka kusema God ni unreasonable?

Then kwenye hiyo theory ya metaphysics mbona inakataa uwepo wake? na hao wanatumia metaphysics kukubali uwepo wa Mungu wanatumia tu reasoning.
 
Naona umeushtukia uongo uliopo kwa jina la imani.

Hapa utaelewa kwa nini saa nyingine mtu unaona unyamaze tu, watu wakishavaa jezi ni ligi na ushabiki.

Aisee ktk dini watu wanadanganywa sana, wengi huingia uoga wakiambiwa habari za motoni na story za watu walioangamizwa.
 

Ikiwa ni hivyo hao wanaedai yupo wamemtambuaje?
Anyway you have free chance to choose either to believe on God or Devil.

Jiulize tu swali hili dogo,... Mtu anawezaje kufanya miujiza??
Soma point no. 9 ktk thread Mkuu.
Mkuu unaweza kuelezea shetani ni nani? ni kiumbe?
 

Yah! kichwa kinasomeka vizuri.
Hata mimi naweza kusema Mungu yupo based on certain definition but Mungu wa waislamu na wakiristo hawezi kuwa Mungu coz ni muongo, unreasonable na anajicontradict.

Najua utashangaa mkuu but research yangu imeniridhisha hayo.
 

Mkuu dini nimeisoma madrasa, nikasisoma kwenye darsa msikitini, nikaisoma shule na kuifanyia mitihani, hata chuo nimesoma ...... na shariah.

Unaposema dini nimeisoma mitandaoni hunitendei haki mkuu. vizuri umekubali kwamba hata post zangu za mwamzo ulikua unaziona, hukutaka tu kusema kwamba nilipinga ububusa and be unreasonable kisa dini imesema.

Anyway, unaweza ukawa sahihi na hisia zako kwa mtazamo wako or mtazamo wa kiimani. naweza kuja pm but nahisi hutopata kuwaamsha na wengine. Kuna maswali nimeuliza hapo kwa mada unaweza kunisaidia majibu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Aisee ktk dini watu wanadanganywa sana, wengi huingia uoga wakiambiwa habari za motoni na story za watu walioangamizwa.

Sema wewe. Sisi tunaonekana vichaa.

Najua watu wanotambua hizo habari za motoni ni uongo na story nzima ni uzushi lakini wanakwenda kuswali kwa sababu dini kwao imekuwa kama therapy.

Hawakubali kukubali uhalisia wa maisha kwamba life is not fair. Hivyo mtu anaona akiswali kidogo shida zake zinapungua na anakua na amani fulani.
 
Ikiwa ni hivyo hao wanaedai yupo wamemtambuaje?

Soma point no. 9 ktk thread Mkuu.

Mkuu unaweza kuelezea shetani ni nani? ni kiumbe?

Ikiwa umeziweka akili zako kukataa uwepo wa Mungu hata uambiwe nini hautoelewa/utajifanya kutoelewa....

ikiwa mganga anaweza kukufanyia mazingaombwe/Viini macho Basi vise versa is true vilevile kwamba kuna alie zaidi ya vyote Katika Dunia hii..Nae Ni MUNGU.

Usidanganywe na akili zako zilizokuzwa na kupaliliwa na Theories, Principles na Ujuvi mdogo sana wa watu wa Dunia hii ambao nao wana uelewa finyu kuhusu Mwenyezi MUNGU.

Kumbbuka kama unataka kukubaliana na Mimi Kuhusu uwepo wa Mungu Kubali kwanza kwamba Ujuzi, Akili, Maarifa na vyote unavyojivunia ni Finyu, na hafifu.

Human Knowledge has Big Limitations to revel presence of God Only Faith can work through it.
 
Hapana kaka, sijashangaa nafikiri unanielewa misimamo yangu kama nnavyoielewa yako na hatujawahi kwaruzana.Huu mjadala ungeweza kutufikirisha na kusaidia watu kutafakari juu ya Mungu. Kama tu watu wangekuja na maandiko na maelezo ya kujitosheleza kuhusu Mungu wanae mwamini.Narudia tena, naamini Mungu yupo licha ya kutokumwelewa kiufasaha, lakini hata tunapokua kwenye ibada hua najaribu kufikiriaJe, hivi katika watu hawa wote kila mmoja ana uelewa sawa au ufaham sawa kuhusu Mungu anaemwabudu? Hapo naongelea watu ambao wako kwenye kusanyiko moja achilia mbali dini au dhehebu lingine.
 

Sasa hizo ni sifa za kutambua dini sahihi au hizo ni za Mungu?
 

Hapa mimi ndo nlikua napataka hii inaonesha dhahiri watu walivo na uelewa mdogo wa Mungu basi kama hamtujui Mungu kwakua sisi ni wadhaifu sana na yeye alie Mkuu sana its safe to say kuna mambo ya uongo tunayompakazia Mungu wetu na huenda yanayotokana na huo udhaifu wetu na ukuu wake tuendeleeni kujitahidi kumtafuta Mungu tusichoke tena bila woga tukazane
 

Kwani ukweli ni upi ambao unakufanya wewe useme hayo mambo ya motoni ni uongo?
 

Kumbuka kwa sisi wakristu tunashauriwa kumwomba roho mtakatifu atusaidie kuweza kumjua vyema huu Mungu, Bila yeye ni Ngumu kumfahamu Yehova Muweza wa yote.

usitegemee akili zako mweyewe, tumwombe yeye atuwezeshe kuweza kumjua zaidi.
 
Kwa nini tanzania haijawahi kutawaliwa na mnyakusa ni kwamba hakuna wasomi, kwa nini kwa nini ujerumani haijawahi kutawaliwa na mweusi hakuna weusi waliosoma kule...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…