A God can be a mere theory, nothing more

Biblia haina matoleo mawili Bali ni toleo moja ambalo limekusanya vitabu viitwavyo vya agano la kale na upande mwingine vitabu viitwavyo vya agano jipya

Agano la kale linahusika na viatabu vinavoelezea historia ya wateule wa Mungu ( Wayahudi/Waisrael ) ambao kupitia kizazi Chao Dunia ingepata Masiah Yesu Kristo.

Kwa maana hiyo Agano la kale limeandika historia ya mahusiano ya Mungu na wateule wake ikiwa ni pamoja na Unabii wa kuja kwa Masiah Bwana Yesu Kristo.

Agano jipya limeandikwa kuonyesha ukamilifu wa unabii Kama ulivyoelezwa katika vitabu vya agano la kale, kuhusu Masiah Yesu Kristo pamoja na nyaraka zilizoandikwa kwa makanisa mbali mbali na kwa wafuasi wa Yesu Kristo.

Yap, hapo nimekusoma.

Jee unaliongeleaje suala biblia kusema or kumanisha Jua linatembea kutoka sehem moja kwenda sehem nyengine kama ilivyoelezwa ktk Joshua 10: 13?

Cc: Kizzy Wizzy
 
Last edited by a moderator:
Nimeongelea kwa mfano wa imani ambayo angalau ninafahamu misingi yake (Imani hiyo) ni nini. Maarifa yangu kuhusu imani ya uislamu au dini nyingine hayatoshelezi mimi kutoa maelezo yoyote juu ya ni nini imani hizo huamini. Hata hivyo, kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kuwa, katika msingi mkuu wa uwepo wa Mungu dini hizi mbili yaani uislamu na ukristo hazitofautiani sana kwani zote zinaamini katika uwepo wa Mungu mmoja aliye asili ya vitu vyote. Zinatofautiana kwa namna gani.

Swali la ikiwa dini nyingine ni sahihi sina majibu yake. Ninachoweza kusema ni kuwa maelezo yangu ya mwanzo yana sehemu ya jibu hilo. Maelezo yanaeleza kuwa kumtambua mungu ni lazima ajidhihirishe kwako kwani binadam hana uwezo wa kumng'amua Mungu - Kisimbuzi (Wengine husema King'amuzi) chake (binadamu) hakiwezi kutambua hilo hadi apewe siri (key) ya msimbo (Code) wenyewe. Yupi mwenye siri (key) sahihi kati ya dini zote zilizopo? Hili nalo si suala la kibinadamu kwani anayeweza kujibu hili ni yule mwenye msimbo yaani Mungu mwenyewe kwa mujibu wa maarifa niliyo nayo.

Sasa nikija kwenye swali lako la tatu ikiwa Mungu anaweza kusema uongo. Ukifuatilia hoja katika aya iliyotangulia nimezungumzia uwepo wa msimbo (code) ambao mwanadamu huhitaji funguo (key) ili kujua kuwa Mungu yupo na yukoje. Ikiwa huwezi kujua uwepo/kutokuwepo kwa Mungu, ni vigumu kuwa unaweza kujua ikiwa kama Mungu anaweza kusema/kutosema uongo. Nirejee imani ile niliyoitumia mwanzo (ukristo). Katika imani hiyo, njia za huyo Mungu, taratibu zake, kanuni zake, sheria zake, n.k. zinashuhudiwa kuwa si za kibinadamu. Uongo ni kanuni/mwenendo/mfumo wa kibinadamu kwani wote tunauona ukiwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Ninachotaka kukuelewesha (pengine ni vigumu sana kufikia hilo lengo) ni kuwa uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu ni wa Kiroho. Roho, kama tunavyoambiwa haina tabia zinazochunguzika kisayansi (sayansi yaani haitokani na nguvu kuu nne). Kwa maana hiyo kutumia njia za kisayansi kuchunguza chunguza uwepo na tabia za Mungu siku zote utapata majibu yasiyo na mantiki. Kwa mantiki hii, kila binadamu anayekabidhiwa funguo ya Kumjua Mungu (kwa mujibu wa imani ya kikristo) hujua tu kile ambacho funguo zake zinamwezesha kujua. Na kwa kuwa kumjua mungu ni hadi ajidhihirishe mwenyewe, uhusiano wa mtu na Mungu ni wa kibinafsi zaidi kuliko tunavyojaribu kuelezea. Uhusiano huo hauelezeki kwani binadamu hana funguo za kujua msimbo mzima. Kwa mujibu wa maelezo ya kibiblia kutoka injili ya Yohana, Thomas (yule aliyetaka kutumia sayansi kumjua Mungu) alipomshika Yesu baada ya kufufuka alisema "Bwana wangu na Mungu wangu". Alichokihisi hakuna anayeweza kukielezea - hata yeye mwenyewe asingeweza kuwaambia wengine alichokihisi hadi akatamka vile.

Mungu hujidhihirisha kwa mtu mmoja mmoja kwa sababu zake na kwa njia zake - na hatuna uwezo wa kuzihoji wala kuzitambua wala kuzielezea wala ................. Chochote tunachofanya, ni ubinadamu tu!!
Oookey. Nakusoma vyema mkuu na zaidi nimekuaoma hapo uliposema kuwa mtu kumjua Mungu ni hadi Mungu ajiridhihishe mwenyewe kwa mtu husika.
But hapo naweza kuuliza ikiwaza Mungu ni mueza wa yote na anapenda watu wote kwanini ajidhihirishe kwa watu wachache? nikiwa na maana kuwa kwanini asijidhihirishe kwa watu wote if he has an ability to do so?

i bet hapo utaniambia hadi mtu huyo amuamini na kumkubali!!! but hiyo ni namna gani ya kutafuta ukweli? let me give you a simple scenario: imagine someone wants to know the effects of sex beyond nature (kuliwa/kulana tigo) would tell me that a reacher must be liwa tigo so as to have a strong evidence concern it? a someone who reject kuliwa cant testify?
Kwanini kumuamini na kumkubali Mungu iwe ni njia pekee ya kumtambua? ivi huoni huo utakua mzigo kwa mtu anaetaka kuproof yupi Mungu wa kweli ukizingatia mtu huyo hakulelewa katika imani ya kikristo? na jee waislamu na watu wa imani nyengine wakiamua kueka kigezo hicho the researcher would believe on which religion? or unafikiri mtu akiamini ukiristo tu ndio atapata jibu hilo?

Ivi huoni ukiamua kukubali na kuamini ndio tayari umeshatengeneza mind yako kukubali chochote kuhusu imani hiyo?

As a reasonable man ningeomba ufikirie na haya:
Hapo underline inaonesha tayari umesha block mind yako juu ya kitu unachokiamini, then ukizingatia hicho ni kitu ulichofundishwa/ulichorithishwa na wazazi wako, hiyo itamaanisha kwamba ungezaliwa or kulelewa na kufunzwa imani tofauti leo hii ungekua unatetea uislamu or imani nyengine.

Kwamtazamo wangu sasa naona njia pekee ya kutambua Mungu/dini flani ni ya kweli we should see its teachings. na ikiwa mafundisho yake ni ya uongo or unreasonable we should discuss it by free mind.

Thus why nimesema hizi dini zinadanganya ingawa umesema uongo huo tunauona sisi tu. ok siwezi kupinga coz thats how you have prepared to believe. But ningependa usome Joshua 10: 13 then uniambie umeelewa nini.

Kivipi jua litembee kutoka sehem moja kwenda sehem nyengine?

Then kwenye genesis uniambie ikiwa Mungu hakutambua or hakuumba Galaxies nyengine, ukumbuke Mungu hatambui hata uwepo wa sayari nyengine ktk galaxy yetu.

Shukran nasubiriri majibu.
 
Yap, hapo nimekusoma.

Jee unaliongeleaje suala biblia kusema or kumanisha Jua linatembea kutoka sehem moja kwenda sehem nyengine kama ilivyoelezwa ktk Joshua 10: 13?

Cc: Kizzy Wizzy

Naelewa sawa na binadamu mwingine yeyote anavyoelewa kuhusu mawio (sunrise) na machweo (sun set ) Kama binadamu wewe Una earth rise na earth set lete Shule Mkuu.
Ama kuhusu Joshua 10:13 ni rahisi kukufafanulia ukinijibu hoja yangu kuhusu mawio na machweo.
 
Last edited by a moderator:
Yap, hapo nimekusoma.

Jee unaliongeleaje suala biblia kusema or kumanisha Jua linatembea kutoka sehem moja kwenda sehem nyengine kama ilivyoelezwa ktk Joshua 10: 13?

Cc: Kizzy Wizzy

Dah! Best Mashaxizo umekuwa anti God sana au ndo umeshaingia kwenye kale kaimani (jokes).......

Katika Joshua 10:13 Joshua aliliambia jua simama na mwezi simama...... Aliposema hivyo haikumaanisha kwamba jua linatembea......hapo kale wengi walitumia jua na mwezi kutambua wakati........Elimu dunia inatuambia jua linachomoza mashariki na linazama Magharibi je hii nayo inamaanisha kwamba jua linatembea kutoka mashariki kwenda magharibi??

Joshua aliliambia Jua simama na mwezi simama inamaana alisimamisha wakati usitembee yaani mchana usiende wala usiku usikaribie mpaka atakapomaliza kazi ya kuuteketeza mji ule.
 
Last edited by a moderator:
Nimekusoma mkuu but hapo underline bado sijakusoma vizuri.

Jee unamanisha Jesus amekuja kurepeal the old testament?

If not, what does that verse mean?
Cc: Nkwesa Makambo

Hebrews 10: 9 then He said, "BEHOLD, I HAVE COME TO DO YOUR WILL." He takes away the first in order to establish the second.10. By this will we have been sanctified through the offering of the body of Jesus Christ once for all.

There were previously in the Old Testament, burnt offerings and sacrifices for sin, but things changed as per Hebrews 10:10
 
Mimi nilichosema kinaushahidi 100%, hata Mungu akiniuliza nitamwambia binadamu uliowapa akili wanaojiita wanasayansi walinidanganya, sasa wewe hiyo kauli aisee inaukakasi haswaaaaa, futaaaaaaaaaaa
Hapana.... Acha tu mi niendelee kuamini Mungu yupo. Acha tu niamini, kama hayupo sina cha kupoteza. Ila nikisema hayupo afu nikamkute.... Anapiga fegi yake na safari lager (huwezi jua anapenda nini).... Afu anambie we kenge ulikuwa unasemaje kule kwa Pengo kuhusu mimi???? Maweeeeeeeee..................
 
Oookey. Nakusoma vyema mkuu na zaidi nimekuaoma hapo uliposema kuwa mtu kumjua Mungu ni hadi Mungu ajiridhihishe mwenyewe kwa mtu husika.
But hapo naweza kuuliza ikiwaza Mungu ni mueza wa yote na anapenda watu wote kwanini ajidhihirishe kwa watu wachache? nikiwa na maana kuwa kwanini asijidhihirishe kwa watu wote if he has an ability to do so?

i bet hapo utaniambia hadi mtu huyo amuamini na kumkubali!!! but hiyo ni namna gani ya kutafuta ukweli? let me give you a simple scenario: imagine someone wants to know the effects of sex beyond nature (kuliwa/kulana tigo) would tell me that a reacher must be liwa tigo so as to have a strong evidence concern it? a someone who reject kuliwa cant testify?
Kwanini kumuamini na kumkubali Mungu iwe ni njia pekee ya kumtambua? ivi huoni huo utakua mzigo kwa mtu anaetaka kuproof yupi Mungu wa kweli ukizingatia mtu huyo hakulelewa katika imani ya kikristo? na jee waislamu na watu wa imani nyengine wakiamua kueka kigezo hicho the researcher would believe on which religion? or unafikiri mtu akiamini ukiristo tu ndio atapata jibu hilo?

Ivi huoni ukiamua kukubali na kuamini ndio tayari umeshatengeneza mind yako kukubali chochote kuhusu imani hiyo?

As a reasonable man ningeomba ufikirie na haya:
Hapo underline inaonesha tayari umesha block mind yako juu ya kitu unachokiamini, then ukizingatia hicho ni kitu ulichofundishwa/ulichorithishwa na wazazi wako, hiyo itamaanisha kwamba ungezaliwa or kulelewa na kufunzwa imani tofauti leo hii ungekua unatetea uislamu or imani nyengine.

Kwamtazamo wangu sasa naona njia pekee ya kutambua Mungu/dini flani ni ya kweli we should see its teachings. na ikiwa mafundisho yake ni ya uongo or unreasonable we should discuss it by free mind.

Thus why nimesema hizi dini zinadanganya ingawa umesema uongo huo tunauona sisi tu. ok siwezi kupinga coz thats how you have prepared to believe. But ningependa usome Joshua 10: 13 then uniambie umeelewa nini.

Kivipi jua litembee kutoka sehem moja kwenda sehem nyengine?

Then kwenye genesis uniambie ikiwa Mungu hakutambua or hakuumba Galaxies nyengine, ukumbuke Mungu hatambui hata uwepo wa sayari nyengine ktk galaxy yetu.

Shukran nasubiriri majibu.

Njia za Mungu hazihojiki, haziuliziki, hazielezeki, ....unless uwe na siri ya Msimbo. Paul wa Kwenye Biblia katika moja ya barua zake alisema Mungu ni upuuzi kwa binadamu wenye busara. Hakuna maelezo nitakayokupa yatakayojitosheleza.

Si kweli kwamba Mungu hujidhihirisha kwa wale wanaomwamini tu; Biblia imejaa mifano ya watu waliokuwa hawamjui Mungu lakini ambao Mungu alijidhihirisha kwao. Mungu hujidhihirisha kwa wenye dini na wasio na dini. Yesu aliwaambia mitume wake kuwa si wao waliomchagua yeye, bali yeye ndo aliwachagua. Hawa ni watu ambao kabla walikuwa hawamjui na wengine walikuwa hawamwamini kabisa. Kwa kifupi huwezi kumwamini Mungu bila yeye kujifunua kwake - Huu ndo umekuwa msingi wa hoja zangu zote. Kwa hiyo wanaomfuata na kumwamini wote ameshajifunua kwao. Ila tu kumbuka - si wote wanaosema kuwa wanamwamini, kweli wanamwamini - wengine wanajinasibisha tu ila siri ya msimbo hawajapata na biblia inatuambia kuwa tutawatambua kwa matunda yao - yaani huwezi kutoa kile ambacho huna hata kama utajisingizia.

Sababu ya Mungu kujidhihirisha kwa yule na si kwa yule hazielezeki kwani Mungu njia zake si za kibinadamu na hazichunguziki wala hazihojiki na mwanadamu. Mungu humchagua mtu kwa sababu zake za Kimungu ambazo kwetu sisi hatuwezi kuzing'amua. Ukienda katika kila jamii utakuta wapo watu "exceptional" ambao matendo yao ni tofauti kabisa na jamii iliyowazunguka hata kama hawakuwahi kuhubiriwa dini hizi zinazohubiriwa. Kila jamii ina dini, dini za jamii nyingi hazihubiriwi majukwaani au hata kwenye biblia au vitabu vitakatifu - nyingi ziko kwenye oral tradition. Kutokana na kuwa Mungu njia zake ni zisizoelezeka binadamu wanaofunuliwa kwa njia mbali mbali hujaribu kuwapa wenzao kile walichokipata - ingawa kwa makosa mengi na mara nyingi hatufanikiwi. Mwelekeo wa dini zote ni mmoja - kuelekea kwenye "purity" na "perfection" ambazo ndio sifa kuu za Mungu.

Ukisoma biblia, kuna siku mitume wake yesu walimwambia kuwa wamewaona watu wakiponya na kutoa pepo kwa jina lake lakini watu hao walikuwa hawafuatani nao na wakajaribu kuwakataza - yaani hao watu wengine waliokuwa wakiponya na kutoa pepo kutumia jina la Yesu hawakuwa na ushirika nao - kwa leo unaweza kusema hawakuwa dini moja. Yesu aliwajibu kuwa mtu hawezi akafanya haya tunayofanya sisi na akaweza asipokuwa nao. Alisema "Waacheni kwa sababu asiye kinyume chetu, yuko na sisi". Katika dini zote, hata katika wasio na dini - utakuta watu wastaarabu hadi utashangaa. Na vile vile utawakuta watu wengine wanaojinasibisha kumfata Mungu lakini matendo yao hayafanani na Mungu. Cha muhimu kujua ni kuwa Mungu si dini wala hahusiani na dini, bali dini ni njia ambayo binadamu wanajaribu kuitumia ......... Mungu hahitaji uwe na dini ili akufikie.

Mungu anatuvuta kwake, kwa njia zake na kila mmoja kwa wakati wake; kazi yetu sisi ni kumsikiliza na kumfuata. Mengine yote unayoyaona ni ubinadamu tu na vurugu zetu.
 
Hapana.... Acha tu mi niendelee kuamini Mungu yupo. Acha tu niamini, kama hayupo sina cha kupoteza. Ila nikisema hayupo afu nikamkute.... Anapiga fegi yake na safari lager (huwezi jua anapenda nini).... Afu anambie we kenge ulikuwa unasemaje kule kwa Pengo kuhusu mimi???? Maweeeeeeeee..................

Mamaweeeeeeee!!!! tufunge huu mjadala, aiseee!! tusitafute laana za Mungu. mimi sitaki tena kuendelea na huu uzi.
 
Kama uwepo wa Mungu ni theory jiulize hiyo pumzi Binadamu aliipata wapi na je Binadamu ana uwezo kuidhibiti isimtoke? Amini Mungu aliyeumba mbingu na dunia yupo na tu hai na Mungu no Roho alituumba kwa mfano wa Roho yake kwa hiyo hijalishi u taahira kilema nk.
 
Naelewa sawa na binadamu mwingine yeyote anavyoelewa kuhusu mawio (sunrise) na machweo (sun set ) Kama binadamu wewe Una earth rise na earth set lete Shule Mkuu.
Ama kuhusu Joshua 10:13 ni rahisi kukufafanulia ukinijibu hoja yangu kuhusu mawio na machweo.

Hahahaaaa! hizo ndo zile siasa nilizoziongelea ktk point no. 5.

Mungu mjuzi wa vitu vyote hawezi kuongea pumba zile ubaya zaidi ni kwamba mnatetea tuuuuuuu. Ok.
 
Dah! Best Mashaxizo umekuwa anti God sana au ndo umeshaingia kwenye kale kaimani (jokes).......
Hahahaaa! best everlink usijehuku! (joke) sjapinga uwepo wake infact Mungu yupo but sio huyu wa waislamu na wakiristo!!!!! Ukipitia mada hapo juu unaweza kupata jibu kwanini nimesema hivyo.
Katika Joshua 10:13 Joshua aliliambia jua simama na mwezi simama...... Aliposema hivyo haikumaanisha kwamba jua linatembea......hapo kale wengi walitumia jua na mwezi kutambua wakati........Elimu dunia inatuambia jua linachomoza mashariki na linazama Magharibi je hii nayo inamaanisha kwamba jua linatembea kutoka mashariki kwenda magharibi??

Joshua aliliambia Jua simama na mwezi simama inamaana alisimamisha wakati usitembee yaani mchana usiende wala usiku usikaribie mpaka atakapomaliza kazi ya kuuteketeza mji ule.

Then hizo ndio siasa nilizoelezea ktk moja ya point huko juu. kwamba waumini wakiona sehemu flani Mungu wao kawaingiza chaka basi watatafuta njia yoyote ili Mungu wao asionekane kakosea. Na hilo haliko kwa wakiristo tu bali hata kwa waislamu Mungu wao akisema dunia ni flati wanakuja na siasa namna hiyo!!! Ivi itawezekana vipi Waislamu wawe sahihi na wakiristo wawe sahihi pia ukizingatia hao ni imani mbili tofauti na hata miungu yao haifanani?

Maana mnaakt kana kwamba Mungu kuna maneno hayajui! ivi ni kweli Mungu hawezi kusema kasimamisha wakati?
Then pale kachanganya jua na mwezi sasa jee unataka kuniambia na mwezi hautembei? Or mwezi unahusika vipi na mambo ya wakati?

Then mimi au wewe au mtu yoyote anapoongelea kuhusu kuzama na kutoka kwa jua ni tofauti na akiongea Mungu. coz Mungu ndio kaumba hivyo vitu na yeye anaona tofauti na tunavyoviona sisi. Binadamu akiona jua linatembea ni sawa coz ndivyo anavyoliona. Jee unataka kuniambia yule aliemba jua na vitu vyote naye anaona hivyo hivyo? (tunavyoona sisi)
Mmmmmh! Haya bhan.
 
Last edited by a moderator:
Kama uwepo wa Mungu ni theory jiulize hiyo pumzi Binadamu aliipata wapi na je Binadamu ana uwezo kuidhibiti isimtoke? Amini Mungu aliyeumba mbingu na dunia yupo na tu hai na Mungu no Roho alituumba kwa mfano wa Roho yake kwa hiyo hijalishi u taahira kilema nk.

Ndiyo maana nawaambiaga kuwa kusema hakuna mungu nayo ni Imani pia kama Imani zengine.
 
Hebrews 10: 9 then He said, "BEHOLD, I HAVE COME TO DO YOUR WILL." He takes away the first in order to establish the second.10. By this will we have been sanctified through the offering of the body of Jesus Christ once for all.

There were previously in the Old Testament, burnt offerings and sacrifices for sin, but things changed as per Hebrews 10:10
Mkuu tukisema haya matabu yenu matakatifu yanajikontradict sijui kwanini hamtaki kukubali. Yani vitabu vyenu vinajicontradict sana ila si ninyi si waislamu nyote mnasiasa hizo hizo za kumsadia Mungu maana ambayo mnahisi inasound. ok nisiongee sana naomba usome Matayo 5: 17. na hiyo ni agano jipya too.

Naomba uniweke sawa hapo waebrania 10: 9 na Hapo Matayo 5: 17.

Aya zote hizo zinapatikana ktk agano jipya.

Cc: everlenk
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaa! hizo ndo zile siasa nilizoziongelea ktk point no. 5.

Mungu mjuzi wa vitu vyote hawezi kuongea pumba zile ubaya zaidi ni kwamba mnatetea tuuuuuuu. Ok.
Mashaxizo kwa kweli umeonyesha kiwango cha juu mno cha upumbavu ( siktukani Kama hujitamvui pole) kwa kuwa unaamini Mungu hayupo nimekusamehe kwa kuwa ni matokeo ya upumbavu.
Kinyume chake ni kwamba Mimi ninayeamini Mungu aliumba viti vyote vilivyopo na yeye ndiye mwekaji wa vile muviitavyo cosmic na physical constants tena kwa kunena tu. Sioni cha ajabu jua kuonekana limesimama tuli hata Joshua amalize kile alichomwomba Mungu amtendee.
Upumbavu mwingine ni pale ambapo umejifanya hujui habari ya sunset na sunrise au hujaona maandiahi husika.
Jikague na ujiedit Kama uko sawa kabla hujajibu na kujianika zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tukisema haya matabu yenu matakatifu yanajikontradict sijui kwanini hamtaki kukubali. Yani vitabu vyenu vinajicontradict sana ila si ninyi si waislamu nyote mnasiasa hizo hizo za kumsadia Mungu maana ambayo mnahisi inasound. ok nisiongee sana naomba usome Matayo 5: 17. na hiyo ni agano jipya too.

Naomba uniweke sawa hapo waebrania 10: 9 na Hapo Matayo 5: 17.

Aya zote hizo zinapatikana ktk agano jipya.

Cc: everlenk
Mashaxizo
Contradiction inaonekana na Lazy thinkers tu, critical thinker hawezi ona kile kinachoonwa na lazy thinker Kama contradiction simply ni kwamba critical thinker anasoma kwa kuangalia context na sio pretext sawa na lazy thinker Kama wewe

Matthew 5:17-18New International Version (NIV)

17 “Do not think that I have come to abolish the Law or the Prophets; I have not come to abolish them but to fulfill them. 18 For truly I tell you, until heaven and earth disappear, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law until everything is accomplished.
Nimekuwekea hadi mstari wa 18 ili nawe ujifunze kusoma sawa na critical thinkers.
Yesu anaposema ;
...until everything is accomplished
Kwa lazy thinker unaelewa nini ?
Je haikuwa kwamba everything had been accomplished ?
Kukuibia elimu kidogo, kufa kwa Yesu Kristo ilikuwa ni accomplishment, kufufuka ikawa ni new era.
Kufufuka kwake ilikuwa ni kutangaza Agano jipya.
Wake up man

At times unajidhalilisha wakati mwenyewe waona umeweka nondo kwa kuwa ni lazy thinker.
 
Last edited by a moderator:
Njia za Mungu hazihojiki, haziuliziki, hazielezeki, ....unless uwe na siri ya Msimbo. Paul wa Kwenye Biblia katika moja ya barua zake alisema Mungu ni upuuzi kwa binadamu wenye busara. Hakuna maelezo nitakayokupa yatakayojitosheleza.
Huyo jamaa anaakili nyingi sana. Sijui kwanini waimini hamtaki kukubaliana na magenius!!! mnapenda kudanganywa danganywa.
Si kweli kwamba Mungu hujidhihirisha kwa wale wanaomwamini tu; Biblia imejaa mifano ya watu waliokuwa hawamjui Mungu lakini ambao Mungu alijidhihirisha kwao. Mungu hujidhihirisha kwa wenye dini na wasio na dini. Yesu aliwaambia mitume wake kuwa si wao waliomchagua yeye, bali yeye ndo aliwachagua. Hawa ni watu ambao kabla walikuwa hawamjui na wengine walikuwa hawamwamini kabisa. Kwa kifupi huwezi kumwamini Mungu bila yeye kujifunua kwake - Huu ndo umekuwa msingi wa hoja zangu zote. Kwa hiyo wanaomfuata na kumwamini wote ameshajifunua kwao. Ila tu kumbuka - si wote wanaosema kuwa wanamwamini, kweli wanamwamini - wengine wanajinasibisha tu ila siri ya msimbo hawajapata na biblia inatuambia kuwa tutawatambua kwa matunda yao - yaani huwezi kutoa kile ambacho huna hata kama utajisingizia.
Unajikontradict ndugu. Let me ask you once again. Kwanini Mungu mpenda watu wote ajidhihirishe kwa watu wachache?
Sababu ya Mungu kujidhihirisha kwa yule na si kwa yule hazielezeki kwani Mungu njia zake si za kibinadamu na hazichunguziki wala hazihojiki na mwanadamu. Mungu humchagua mtu kwa sababu zake za Kimungu ambazo kwetu sisi hatuwezi kuzing'amua. Ukienda katika kila jamii utakuta wapo watu "exceptional" ambao matendo yao ni tofauti kabisa na jamii iliyowazunguka hata kama hawakuwahi kuhubiriwa dini hizi zinazohubiriwa. Kila jamii ina dini, dini za jamii nyingi hazihubiriwi majukwaani au hata kwenye biblia au vitabu vitakatifu - nyingi ziko kwenye oral tradition. Kutokana na kuwa Mungu njia zake ni zisizoelezeka binadamu wanaofunuliwa kwa njia mbali mbali hujaribu kuwapa wenzao kile walichokipata - ingawa kwa makosa mengi na mara nyingi hatufanikiwi. Mwelekeo wa dini zote ni mmoja - kuelekea kwenye "purity" na "perfection" ambazo ndio sifa kuu za Mungu.
Ukisoma biblia, kuna siku mitume wake yesu walimwambia kuwa wamewaona watu wakiponya na kutoa pepo kwa jina lake lakini watu hao walikuwa hawafuatani nao na wakajaribu kuwakataza - yaani hao watu wengine waliokuwa wakiponya na kutoa pepo kutumia jina la Yesu hawakuwa na ushirika nao - kwa leo unaweza kusema hawakuwa dini moja. Yesu aliwajibu kuwa mtu hawezi akafanya haya tunayofanya sisi na akaweza asipokuwa nao. Alisema "Waacheni kwa sababu asiye kinyume chetu, yuko na sisi". Katika dini zote, hata katika wasio na dini - utakuta watu wastaarabu hadi utashangaa. Na vile vile utawakuta watu wengine wanaojinasibisha kumfata Mungu lakini matendo yao hayafanani na Mungu. Cha muhimu kujua ni kuwa Mungu si dini wala hahusiani na dini, bali dini ni njia ambayo binadamu wanajaribu kuitumia ......... Mungu hahitaji uwe na dini ili akufikie.
Hahahahahaaaaa! Mkuu unajikontradict sana! Ntuzu umesoma hapo underline?
Mkuu ikiwa ulitrace post zangu humu hata tusingezozana! Coz huo ndo msimamo wangu thus why hata ktk kichwa cha habari ya thiredi hii kinasomeka 'A God CAN BE....' Najua kuandika Mungu hayupo but sikuandika hivyo! naomba utafakari hilo mkuu. Mungu ninaemuamini ni kama alivyoeleza Asprin = hawezi kuwa na pirika za kuandika matabu coz si muandishi.
Mungu anatuvuta kwake, kwa njia zake na kila mmoja kwa wakati wake; kazi yetu sisi ni kumsikiliza na kumfuata. Mengine yote unayoyaona ni ubinadamu tu na vurugu zetu.

Hapa unaendelea kujizonga mkuu!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kama uwepo wa Mungu ni theory jiulize hiyo pumzi Binadamu aliipata wapi na je Binadamu ana uwezo kuidhibiti isimtoke? Amini Mungu aliyeumba mbingu na dunia yupo na tu hai na Mungu no Roho alituumba kwa mfano wa Roho yake kwa hiyo hijalishi u taahira kilema nk.

Hahahahaaaaa! kijana it seems umeshapewa sumu za kutosha! Pole sana.

Pumzi mapigo ya moyo ni spirit or i can say your subconscious mind yako ndio inawezesha yote hayo.

So kabla ya kuuliza subconscious mind or spirit/roho inatoka wapi andaa jibu huyo Mungu wako katokea wapi.
 
Ndiyo maana nawaambiaga kuwa kusema hakuna mungu nayo ni Imani pia kama Imani zengine.

What is this Mkuu?
Hivi umeisoma vizuri post ya mdau uliemjibu hivyo?

Hata kama uliemjibu hivyo anastahili uko wrong sana mkuu. Always we proof something which exist.
 
Mashaxizo kwa kweli umeonyesha kiwango cha juu mno cha upumbavu ( siktukani Kama hujitamvui pole) kwa kuwa unaamini Mungu hayupo nimekusamehe kwa kuwa ni matokeo ya upumbavu.
Kinyume chake ni kwamba Mimi ninayeamini Mungu aliumba viti vyote vilivyopo na yeye ndiye mwekaji wa vile muviitavyo cosmic na physical constants tena kwa kunena tu. Sioni cha ajabu jua kuonekana limesimama tuli hata Joshua amalize kile alichomwomba Mungu amtendee.
Upumbavu mwingine ni pale ambapo umejifanya hujui habari ya sunset na sunrise au hujaona maandiahi husika.
Jikague na ujiedit Kama uko sawa kabla hujajibu na kujianika zaidi.

Mkuu hata usijali you can call me any name that you wish to call me. iknow thats your habit to call somebody fool because he reject what you believe. nakumbuka hata Annael amekuambia hilo. So be free im not care at all coz i know as well as I see!

Unaposema Nasema or Naamini Mungu hayupo hunitendei haki mkuu!!!! nimesema Mungu anaweza kuepo kwa maana ya Super natural power but si huyu wa Quran na biblia. sijui kwanini hutaki kukubali hapo wakati wewe ni mmoja kati ya wachache walioona post zangu humu!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom