Wewe unaweza kuona hivyo kwa sababu zako mwenyewe; ambazo zinaweza kuwa tofauti na sababu za wengine wanaomwona kuwa mwenye msaada na matumaini.
Hii kauli yako ya kijumla hivi ni ushahidi tosha kwamba unazo sababu zako binafsi.
Chukulia kwa mfano, kazi alizokuwa akifanya Lissu huko nyuma za kutetea wananchi waliokuwa wakionewa kwenye maeneo ya migodi, hizi zote zilikuwa ni kazi za "uchafuzi"?
Kutoa tahadhari juu ya mambo yaliyokuwa yakifanywa kinyume cha taratibu/sheria katika maswala ya madini, ilikuwa ni kazi ya uchafuzi?
Ni muhimu kuyaweka maswala ya kitaifa mbele katika kutoa hukumu. Tusiyumbishwe na ushabiki wa kichama zaidi katika maswala muhimu ya nchi.
Mkuu Kalamu unajadili ukiwa umesimama kwenye uanaharakati na nationalism two factors which compromises objectivity.
Naomba usome hii
Gazeti la Guardian on Sunday la Septmba 14, 2011 lilichapisha habari kwenye ukurasa wake wa mbeli yenye iliyopewa kichwa cha habari
: “From foes to partners: Tales of Zitto Kabwe and African Barrick Gold” kwa tafasri isiyo rasmi ya kiswahili Kutoka uadui mpaka kuwa m wenza: hadithi ya Zitto Kabwe na African Barrick Gold. Habari hiyo ilikuwa inanukuu utafiti uliofanywa na Adam Hooper raia wa Kanada ambaye katika utafiti wake alikutana na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe. Mheshimiwa Zitto alinukuliwa wakimwabia mtakiti Hooper kuwa msimammo wake kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini na hasa baada ya kuulipua usiri wa mkataba wa Buzwaji umempa umaarufu mkubwa nchini. Umaarufu huo ni silaha tosha dhidi ya Barrick na wawekezaji wengine. Mheshimiwa Zitto alimfahamisha mtafiti Hooper kuwa kwa kutumia silaha hiyo jimbo lake la Kigoma Kaskazini ni jimbo lenye mgodi lililo mbali na mgodi. Kwa adhima hii mheshimiwa Zitto alijipatia Dola za Kimarekani elfu kumi alizozitumia kwa ajili ya jimbo lake.
Habari hiyo ilizua mjadala mkubwa katika mtandao wa kijamii wa Jamiii Forum. kisanduku namba 19 hapo chini kinaonyeaha sehemu ya mjadala huo.
Tanzania inahitaji watu wakweli wa kutuelekeza wapi pa kwenda. Kwa bahati mbaya sana wasomi wetu na kwa ujumla wasomi wote duniani hawezi kutwambia ukweli. Mwandishi mmoja wa kimarekani aliwahi kuandika na kuonya hatari ya kuwasikiliza wasomi na wanazuoni. Kwa maoni yake wasomi na wanazuoni hawasemi maisha halisi. Wanasema jinsi mambo yanavyopaswa kuwa badala ya mambo yalivyo. Wanasiasa wetu nao ambao wengi wao wakiwa wametokana na wasomi na wazuoni wao wanasema tunayotaka kusikia hata kama ni uongo. Wanacheza na akili zetu kwa faida yao na hasara kwetu. Wanaharakati wetu nao ni yale yale wanapinga tu tena wanapinga kila kitu na kutufanya tuamini kuwa tabibu anayekutoa damu kwa ajili ya kupima kama una malaria anakuibia damu yako, na ukimkubalia utakufa mda si mrefu na wa kumlaunu ni mama yako mzazi aliyekupeleka zahanati kwa matibabu.
Wasomi,wanazuoni na wanaharakati wanatuonyesha kuwa katika karne hii ya sayansi na teknolojia na utandawzi huu tunaweza kuendela kuchimba dhahabu na madini mengine kwa sepetu, jembe na sululu. Kwamba tunaweza kuvuna mali asili zetu bila kuwekeza hata senti tano. Kwamba tunaweza kutumia mitaji ya watu na kisha tukawapangia nini na kiasi cha kuchukua. Kwa kweli watanzania tunastahili zaidi ya haya.
wanaharakati wa haki za binadamu, mazingira na demokrasia wamekuwa wakipinga uwekezaji katika sekta ya madini ulimwnguni kote.
Lakini wanaharakati hawa wamekuwa wanasahau kwamba Mungu aliwalekeza wanadamu waende wakavitawale na kuvitumia vyote vilivyomo. Hata hivyo vitabu vyote vitakatifu vinahimiza matumizi endelefu ya mazingira.
Sayansi imetusaidia kuelewa kuwa hakuna dhana wala kanuni iliyosimama pekee yake inayoweza kutoa elekezo sahihi kuhusu nini kinapaswa kufanyika na ni kipi hakipaswi kufanyika.Kanuni na dhana zote zinapawa kuangaliwa ili kutoa elekezo sahihi la namna kila jambo linavyopaswa kufanyika.
Hivi sivyo wanaharakati wanavyofanya kazi.Agharabu wanaharakati huchukua dhana na kanuni moja na kuishikia bango hadi kieleweke. Kwa kufanya hivi wamejipatia umaarufu mkubwa na kuwafanya wengine waonekane ni wanyama, wasaliti na wauza nchi.
Kwa hali ilivyo sasa hivi ambapo kilimo hakina tija, kupinga uwekezaji katika sekta ya madini ni kutowatendea haki watanzania wengi. Kwa jinsi hali ilivyo kuwachochea wakazi wa maeneo ambako hazina kubwa ya madini imegunduliwa wakatae kuhama ilikupisha uwekezaji ni kutowatendea haki watanzania wengi pia. Kwa jinsi hali ilivyo kudhani kuwa uchimbaji mdogo mdogo unatija kuliko uchimbaji mkubwa wa madini ni kuwanyima haki watanzania wengi.Hata hivyo wawekezaji hasa wawekezaji wakubwa kuchimba madini kwa namna ambayo si endelevu ni kuwanyima watanzania wa sasa na wajao haki.
Sumu haina kuonja ni maneno yalioandikwa nyuma ya daladala moja mjini Mwanza. Msemo huu hauna maana yoyote kwa wanaharakati kwani wao sumu lazima iwe nyingi. Mtizamo huu wa wanaharakati unawaona wachimbaji wakubwa tu ndio wanaochafua mazingira. Wanasukumwa na dhana na kanuni ya mfuko mrefu (the deep pocket doctrine). Dhana hii inaelekeza kuwa kama mdogo na mkubwa, maskini na tajiri, mwenyeji na mgeni wakifanya kosa sawa ilikuhakishiwa kulipwa, kujulikana na kujipatia umaarufu mkubwa mkomalie mkubwa, tajiri na mgeni.
Wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa Bulyanhulu wote hawakuwa wazaliwa wa pale. Wengi wao walienda pale na kwa kiasi kikubwa kuharibu utaratibu wa maisha wa wenyeji wa pale. Wanaharakati hawakuona hadi pale wakubwa walipoingia. Inasemekana kuwa wakati wa uondoaji wa wachimbaji wadogo pale wenyeji walitumia fursa hiyo pia kulipa kisasi cha ubaya waliotendewa na wachimbaji wakuja.
Tumeeona huko nyuma kuwa wachimbaji wadogo kwa mwaka wanazalisha dhahabu karibu sawa na mgodi mkubwa wa kisasa. Tunajua kuwa dhahabu lazima isafishwe na kemikali. Je kemikali hizo zinaenda wapi? Tarime wamechimba dhahabu miaka nenda miaka rudi, Geita nako wamefanya hivyo.Kwa kuwatendea haki watanzania wanaharakati wanapaswa kueleza kemikali hizo zilituzwaje na madhara yake ni yapi.
Mara nyingi wanaharakati wamekuwa wakitumiwa na washindani katika sekta ya madini. Kunaushindani mkubwa kati ya wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa juu ya nani aendeleee kuwepo. Mara zote wanaharakati kwa uumini wao wa dhana ya mfuko mrefu husimama na wachimbaji wadogo dhidi ya wachimbaji wakubwa ambao huungwa mkono na serikali. Lakini katika karne hii ya sayansi na teknolojia baado tunaamini madini yanaweza kuchibwa kwa jembe na sululu? Kwa tija iliyoletwa na wachimbaji wadogo wadogo bado kuna mtu anadhani kuwa uchimbaji mdogo mdogo unamanufaa kwa watanzania wote? Watanzania wanapaswa kutafakarI na kuchukua hatua sahihi.
SOURCE: Je, Tanzania imeuzwa (hakijachapishwa)
Mkuu Kalamu ukipata bahati ya kusoma huu muswada utampiga Lissu kila unapomuona