A Golden Opportunity? Ni Kitabu kilichoandikwa na Tundu Lissu, UDSM na LHRC kuhusu Migodi ya Dhahabu

Acha ujinga,kikwete alitoa asilimai 3 hadi 4,magufuri kutoka 4 hadi 16pcnt ten non dilutable wakayi za kikwete zilikiwa dilutable.
Mkuu acha kujiaabisha hauko sahihi, soma sheria ya madini ya 2010
 
Kwa jinsi unavyopenda kuhojoreka humu hasa kwenye mada ngumu na makini huku ukiwashusha wenye hoja jenzi hayumkini wewe ni mbunge wa ccm uliyebebwa na magufuli na sasa ni chawa mwandamizi unayetafuta nafasi ya kurejea Tena 2025!
Hao Lissu na Zito wlihusikaje na mikataba mibovu ya madini? Hebu funguka nasi tukuelewe.
Mkuu sijui kama unaufahamu wa kutosha na sekta ya madini nchi hii- unasukumwa na utaifa na uanaharakati vitu ambayo vinakufanya uwe mjinga na kipofu
 
Sisi Watanganyika tunajivunia huyu Lisu ni baraka kwa taifa letu la Tanganyika Mungu azidi kumlinda dhidi yabwafilisti wanaotamani kumnyamazisha katika jitihada zake zakutetea rasilimali za Taifa letu
ukiweza na kama unaweza zaa nae ila ni mpuuzi mwingine tu duniani hapa, very selfish
 
Wakati tukitafakali maandiko haya tujiulize ni kwanini hakuna Rais aliyewahi kuchukua hatua za marekebisho hadi alipokuja Dr Josefu Magufuli? Na je alifikia malengo?
Marais wote wamefanya jitihada za kuifanya Tanzania inufaike na raslimali madini
 
Historia ya uchimbaji wa madini Tanzania

Madini katika Tanzania yameanza toka kabla ya kuja kwa wageni wa kizungu. Watanzania walitumia madini kama udongo wa chuma waliofua na kutengeneza zana mbali mbali. Aidha mfinyanzi pia ulichibwa na kutumika kwa ajili ya kutengenezea vyombo vya nyumbani kama vile vyungu na mitungi.

Brian Cooksey (2011) anaeleza kuwa Tanzania ambayo ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini na Ghana ilianza kuchimba dhahabu kwa kiwango kikubwa katika miaka ya 1890 wakati wa utawala wa Kijerumani hasa katika maeneo yanayosunguka ziwa Victoria.

Aidha Society of internatioanal Development (2009) wanabainisha kuwa palikuwepo na uchimbaji wa madini hasa dhahabu katika maeneo ya Ngasamo, sekenke, Lupa, Buhemba, Nzega na Geita. Katika eneo la Geita Kampuni ya Gold Syndicate Concession for Precious Metal na Tanganyika concession zilifanya kazi.

Chachage (1995) anaongeza kwa kusema kuwa katika kipindi hili cha utawala wa kikoloni shughuli za utafiti zilizoendeshwa na makampuni binafsi ziliwezesha ugunduzi wa dhahabu, urani, makaa ya mawe almasi na ulanga. Kwa mjerumani dhahabu na ulanga vilipewa kipaumbele kwa sababu ya matumizi yake. Ulanga ulitumika katika utengenezaji wa milipuko na taa za stima wakati dhahabu ilitumika kama fedha.

Baada ya vita kuu ya kwanza kasi ya uchimbaji mkubwa kiasi iliongezeka. kasi hii ya uchimbaji mkubwa kiasi ilizimika miaka ya 1950 kwa sababu ya bei ndogo ya dhahabu katika soko la dunia. Vita kuu ya pili iliathiri upatikanaji wa mitaji na vifaa na kusanabishama kampuni mengi yaliyokuwa yanasghugurika na utafitai na uchimbaji wa madni kuachana na shughuli hizo. hata hivyo uchimbaji uliendelezwa na wachimbaji wadogo wadogo hadi miaka ya 1990 pale wachimbaji hao wadogo walipobanwa na makampuni makubwa ya kigeni.

Ushiriki wa serikali

Chini ya siasa ya ujamaa uchimbaji wa madini ulikuwa chini ya serikali kwa asilimia mia moja. Ilikufanikisha hali hiyo serikali ilianzisha shirika la maendeleo la taifa (National Development Corporation- NDC) na shirika la madini la taifa (State Mining Corporation-STAMICO) mwaka 1972. STAMICO ilifanyakazi katika mazingira magumu ya ukosefu wa mtaji wa kutosha wa fedha na ujuzi. Aidha wakati huo bei ya dhahabu ilikuwa chini sana katika soko la dunia kiasi ambacho kisingeweza kumeza gharama za uzalishaji na kuzaa faida

Kushindwa kwa STAMICO kuliwapa mwanya wachimbaji wadogo wadogo ambao hata hivyo hawakuinufaisha nchi kwa kiasi kikubwa. Ili kuzibiti hali hiyo serikali iliruhusu benki kuu kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo kuanzia mwezi wa Aprili mwaka 1990 (Cooksey, 2011).
source: Je, Tanzania imeuzwa ( hakijachapishwa)
 
Basi sheria ipo tangu 2012 nadhani,kwamba mrabaha ni 16%,so mikataba ilipokwisha walitakiwa kutoa mrabaha huo,ikawa ngondo,mgodi wa kwanza kuwa impacted ni resolute nzega
Ili mtu afaidike na chochote katika uchumi au jambo lolote lazima mtu huyo ahusike na jambo hilo kwa namna moja au nyingine. Kwa kutambua hili, Tanzania imetunga sera na sheria ya madini.

Kwa mjibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 kifungu cha tano madini na umiliki wake viko chini ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hakuna mtu anaruhusa ya kutafuta , kuchmba na kumiliki madini isipokuwa kama amapewa kibali cha kufanya hivyo kwa mjibu wa sheria na mamlaka inayohusika kwa mjibu wa sheria.

Kifungu cha kumi cha sheria ya madini kinaipa haki Jamhuri ya muungano ya Tanzania kushiriki katika uchimbaji wa madini chini ya leseni maalumu ya uchimbaji wa madini bila kuwekeza chochote (Free carried interest) katika uendelezaji wa mgodi ndani ya leseni maalumu ya uchimbaji. Hisa za

Free carried interest ni matokeo ya majadiliano kati ya waziri mwenye dhamana ya madini kwa kushauriana na bodi ya ushauri ya madini na mwenye leseni maalum ya uchimbaji.

Kwa mjibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 watanzania wamepewa nafasi ya kushiriki katika undelezaji wa mali asili madini kwa kumilikishwa kisheria vitalu vya madini. Hii ni hatua mhimu sana katika safari ya kufikia kufaidika na mali asili madini.

SOURCE: Je, Tanzania imeuzwa (hakijachapishwa)
 
Ahsante sana mkuu 'Bush...'. Mada za namna hii ndizo zingeheshimika sana katika jukwaa kama hili hapa JF.

Wakati nikisoma maelezo yako, nikawa naingiwa na dukuduku la kutaka nikwambie usipige stori ndefu, tuwekee tune wenyewe. Kumbe hapo mwisho umefanya kweli.

Nchi yetu Tanzania sasa kuna ombwe kubwa sana la wasomi/wana siasa wa aina ya Tundu Lissu. Watu wameweka elimu zao pembeni na kujikita katika kuwa maroboti tu ya kutumiwa na wanasiasa hata wasiokuwa na kitu kichwani.
Katika mawaziri tulio nao/tuliowahi kuwa nao, ni wangapi wametumia taaluma zao hata kuchapisha tu makala kwenye gazeti la kawaida?

Kwa hiyo, ninapoona mtu, kama Tundu Lissu akijipambanua kuwa tofauti kabisa na wengi wengine, hiyo inanipa matumaini makubwa. Ni muhimu taifa letu lirudi kwenye misingi yake. Watu watumie elimu waliyo nayo katika kulijenga taifa hili.

Sijawahi kuona andiko lolote la maana toka kwa:

Kikwete; kabudi, Samia, Nchemba Madilu, na wengi wengine wanaotupigia kelele kila siku Bungeni na kwenye Baraza la Mawaziri, CCM na kwingineko.
Naheshimu, uwezo wa Zitto Kabwe (ukiweka mbali siasa zake).

Kwa hiyo, Tundu Lissu ni tofauti kubwa sana na hawa wengine wote kwa sasa.
Mkuu Lissu ni mchafuzi kachafua kila mahali anakopita hakuna kinachoendelea ni mharibifu
 
Wewe unaweza kuona hivyo kwa sababu zako mwenyewe; ambazo zinaweza kuwa tofauti na sababu za wengine wanaomwona kuwa mwenye msaada na matumaini.
Hii kauli yako ya kijumla hivi ni ushahidi tosha kwamba unazo sababu zako binafsi.
Chukulia kwa mfano, kazi alizokuwa akifanya Lissu huko nyuma za kutetea wananchi waliokuwa wakionewa kwenye maeneo ya migodi, hizi zote zilikuwa ni kazi za "uchafuzi"?

Kutoa tahadhari juu ya mambo yaliyokuwa yakifanywa kinyume cha taratibu/sheria katika maswala ya madini, ilikuwa ni kazi ya uchafuzi?
Ni muhimu kuyaweka maswala ya kitaifa mbele katika kutoa hukumu. Tusiyumbishwe na ushabiki wa kichama zaidi katika maswala muhimu ya nchi.
 
Mkuu Kalamu unajadili ukiwa umesimama kwenye uanaharakati na nationalism two factors which compromises objectivity.
Naomba usome hii
Gazeti la Guardian on Sunday la Septmba 14, 2011 lilichapisha habari kwenye ukurasa wake wa mbeli yenye iliyopewa kichwa cha habari: “From foes to partners: Tales of Zitto Kabwe and African Barrick Gold” kwa tafasri isiyo rasmi ya kiswahili Kutoka uadui mpaka kuwa m wenza: hadithi ya Zitto Kabwe na African Barrick Gold. Habari hiyo ilikuwa inanukuu utafiti uliofanywa na Adam Hooper raia wa Kanada ambaye katika utafiti wake alikutana na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe. Mheshimiwa Zitto alinukuliwa wakimwabia mtakiti Hooper kuwa msimammo wake kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini na hasa baada ya kuulipua usiri wa mkataba wa Buzwaji umempa umaarufu mkubwa nchini. Umaarufu huo ni silaha tosha dhidi ya Barrick na wawekezaji wengine. Mheshimiwa Zitto alimfahamisha mtafiti Hooper kuwa kwa kutumia silaha hiyo jimbo lake la Kigoma Kaskazini ni jimbo lenye mgodi lililo mbali na mgodi. Kwa adhima hii mheshimiwa Zitto alijipatia Dola za Kimarekani elfu kumi alizozitumia kwa ajili ya jimbo lake.

Habari hiyo ilizua mjadala mkubwa katika mtandao wa kijamii wa Jamiii Forum. kisanduku namba 19 hapo chini kinaonyeaha sehemu ya mjadala huo.

Tanzania inahitaji watu wakweli wa kutuelekeza wapi pa kwenda. Kwa bahati mbaya sana wasomi wetu na kwa ujumla wasomi wote duniani hawezi kutwambia ukweli. Mwandishi mmoja wa kimarekani aliwahi kuandika na kuonya hatari ya kuwasikiliza wasomi na wanazuoni. Kwa maoni yake wasomi na wanazuoni hawasemi maisha halisi. Wanasema jinsi mambo yanavyopaswa kuwa badala ya mambo yalivyo. Wanasiasa wetu nao ambao wengi wao wakiwa wametokana na wasomi na wazuoni wao wanasema tunayotaka kusikia hata kama ni uongo. Wanacheza na akili zetu kwa faida yao na hasara kwetu. Wanaharakati wetu nao ni yale yale wanapinga tu tena wanapinga kila kitu na kutufanya tuamini kuwa tabibu anayekutoa damu kwa ajili ya kupima kama una malaria anakuibia damu yako, na ukimkubalia utakufa mda si mrefu na wa kumlaunu ni mama yako mzazi aliyekupeleka zahanati kwa matibabu.

Wasomi,wanazuoni na wanaharakati wanatuonyesha kuwa katika karne hii ya sayansi na teknolojia na utandawzi huu tunaweza kuendela kuchimba dhahabu na madini mengine kwa sepetu, jembe na sululu. Kwamba tunaweza kuvuna mali asili zetu bila kuwekeza hata senti tano. Kwamba tunaweza kutumia mitaji ya watu na kisha tukawapangia nini na kiasi cha kuchukua. Kwa kweli watanzania tunastahili zaidi ya haya.

wanaharakati wa haki za binadamu, mazingira na demokrasia wamekuwa wakipinga uwekezaji katika sekta ya madini ulimwnguni kote.

Lakini wanaharakati hawa wamekuwa wanasahau kwamba Mungu aliwalekeza wanadamu waende wakavitawale na kuvitumia vyote vilivyomo. Hata hivyo vitabu vyote vitakatifu vinahimiza matumizi endelefu ya mazingira.

Sayansi imetusaidia kuelewa kuwa hakuna dhana wala kanuni iliyosimama pekee yake inayoweza kutoa elekezo sahihi kuhusu nini kinapaswa kufanyika na ni kipi hakipaswi kufanyika.Kanuni na dhana zote zinapawa kuangaliwa ili kutoa elekezo sahihi la namna kila jambo linavyopaswa kufanyika.

Hivi sivyo wanaharakati wanavyofanya kazi.Agharabu wanaharakati huchukua dhana na kanuni moja na kuishikia bango hadi kieleweke. Kwa kufanya hivi wamejipatia umaarufu mkubwa na kuwafanya wengine waonekane ni wanyama, wasaliti na wauza nchi.

Kwa hali ilivyo sasa hivi ambapo kilimo hakina tija, kupinga uwekezaji katika sekta ya madini ni kutowatendea haki watanzania wengi. Kwa jinsi hali ilivyo kuwachochea wakazi wa maeneo ambako hazina kubwa ya madini imegunduliwa wakatae kuhama ilikupisha uwekezaji ni kutowatendea haki watanzania wengi pia. Kwa jinsi hali ilivyo kudhani kuwa uchimbaji mdogo mdogo unatija kuliko uchimbaji mkubwa wa madini ni kuwanyima haki watanzania wengi.Hata hivyo wawekezaji hasa wawekezaji wakubwa kuchimba madini kwa namna ambayo si endelevu ni kuwanyima watanzania wa sasa na wajao haki.

Sumu haina kuonja ni maneno yalioandikwa nyuma ya daladala moja mjini Mwanza. Msemo huu hauna maana yoyote kwa wanaharakati kwani wao sumu lazima iwe nyingi. Mtizamo huu wa wanaharakati unawaona wachimbaji wakubwa tu ndio wanaochafua mazingira. Wanasukumwa na dhana na kanuni ya mfuko mrefu (the deep pocket doctrine). Dhana hii inaelekeza kuwa kama mdogo na mkubwa, maskini na tajiri, mwenyeji na mgeni wakifanya kosa sawa ilikuhakishiwa kulipwa, kujulikana na kujipatia umaarufu mkubwa mkomalie mkubwa, tajiri na mgeni.

Wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa Bulyanhulu wote hawakuwa wazaliwa wa pale. Wengi wao walienda pale na kwa kiasi kikubwa kuharibu utaratibu wa maisha wa wenyeji wa pale. Wanaharakati hawakuona hadi pale wakubwa walipoingia. Inasemekana kuwa wakati wa uondoaji wa wachimbaji wadogo pale wenyeji walitumia fursa hiyo pia kulipa kisasi cha ubaya waliotendewa na wachimbaji wakuja.

Tumeeona huko nyuma kuwa wachimbaji wadogo kwa mwaka wanazalisha dhahabu karibu sawa na mgodi mkubwa wa kisasa. Tunajua kuwa dhahabu lazima isafishwe na kemikali. Je kemikali hizo zinaenda wapi? Tarime wamechimba dhahabu miaka nenda miaka rudi, Geita nako wamefanya hivyo.Kwa kuwatendea haki watanzania wanaharakati wanapaswa kueleza kemikali hizo zilituzwaje na madhara yake ni yapi.

Mara nyingi wanaharakati wamekuwa wakitumiwa na washindani katika sekta ya madini. Kunaushindani mkubwa kati ya wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa juu ya nani aendeleee kuwepo. Mara zote wanaharakati kwa uumini wao wa dhana ya mfuko mrefu husimama na wachimbaji wadogo dhidi ya wachimbaji wakubwa ambao huungwa mkono na serikali. Lakini katika karne hii ya sayansi na teknolojia baado tunaamini madini yanaweza kuchibwa kwa jembe na sululu? Kwa tija iliyoletwa na wachimbaji wadogo wadogo bado kuna mtu anadhani kuwa uchimbaji mdogo mdogo unamanufaa kwa watanzania wote? Watanzania wanapaswa kutafakarI na kuchukua hatua sahihi.

SOURCE: Je, Tanzania imeuzwa (hakijachapishwa)
Mkuu Kalamu ukipata bahati ya kusoma huu muswada utampiga Lissu kila unapomuona
 
Mkuu 'Comte', kwanza naomba nikufahamishe kwamba mimi ni mtu ninayejiamini katika fikra zangu. Siyumbishwi kwa kusoma vijalada kama hivi.

Niseme kwa sasa, haraka haraka; nitasoma, pamoja nakuwa maandishi ya aina hii huwa nayapuuzia mara ninapoyaona humu.
Pili, nitayasoma haya, nikijuwa wazi michango yako (historia yako) humu JF nikiifahamu vizuri toka muda kitambo, pamoja na kwamba hatujawahi kujadili jambo kati yetu. Safari hii nitatenga muda nikusikilize kuhusu hili, kama nitaona umakini katika kujadili haya, kwa manufaa ya taifa kama ulivyosema, na siyo ushabiki wa kivyama kama nikujuavyo.

Tatu, nilianza kusoma hadi katikati ya uliyowasilisha kwenye makala hiyo. Nimechoka kuendelea hadi mwisho kwa sababu sikuona uhusiano kati ya Lissu na Kabwe. Hawa ni watu wawili tofauti kabisa. Sasa, kama makala yako hii inamzungumzia Lissu huko mwisho, nitarudi niisome yote na nione uhusiano upo wapi.

Zito ana akili nzuri, lakini ni mtu mwenye tamaa. Anajisahau sana inapokuja kwenye maslahi yake binafsi na maslahi ya wananchi wa nchi hii. Kwa sababu hiyo, pamoja na kujuwa uwezo wake mzuri kiakili, simpi nafasi ya uongozi mzuri katika nafasi yoyote ile serikalini.

Baadae.
 
Mkuu Kalamu kama tunachojadili ni sekta ya madini na huoni ni namna gani Lissu na Kabwe wanamfanano basi tuishie hapo
 
Hawa ni watu wawili ambao ni tofauti kabisa kwa kila hali unayotaka kuwalinganisha.
 
Back
Top Bottom