A Golden Opportunity? Ni Kitabu kilichoandikwa na Tundu Lissu, UDSM na LHRC kuhusu Migodi ya Dhahabu

A Golden Opportunity? Ni Kitabu kilichoandikwa na Tundu Lissu, UDSM na LHRC kuhusu Migodi ya Dhahabu

Sikuwa nafahamu kwamba huyu Tundu Lissu ana Ushawishi Mkubwa namna hii sio tu leo ambapo tunamuona kwenye Jukwaa la Siasa bali kazi ya kutetea Nchi, Taifa na Wanachi wake ameianza Zamani ktk Ujana wake woote.

Kwamba Tundu Lissu anaweza kuwa na Influence kwenye Tasisi kubwa kama baraza la Taifa la kiislam BAKWATA, Baraza la Kikristo Tanzania CCT, Tanzania Episcopal Council TEC, Legal and Human Right Centre(LHRC) na miamba wengine wa Uchumi ktk taasisi mbalimbali kama University of Dar Es Salaam.

Ushiriki wa Taasisi kubwa za namna hii katika uchambuzi, utafiti na hatimaye ku ripoti taarifa hizi za Uchimbaji wa madini ya Dhahabu Tanzania umetokana na ukweli kwamba;

1. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba Tanzania na vitu vyote vilivyomo.
2. Kwamba Mungu alipomuumba Mwanadamu alitaka aishi maisha ya ukamilifu na utajiri hivyo kila alipo Mwanadamu kuna vyanzo vya uchumi vinavyomuwezesha kuishi na Kustawi.

Wame quote kitabu cha Zaburi 24: 1.

Katika Utafiti na matokeo yao waligundua mambo makuu matatu.

1. Migodi ya Dhahabu inatoa kiasi kidogo cha mapato ya Kodi
2.Usiri Mkubwa kwenye miradi ya madini na hivyo hatari ua kuwepo mazingira ya Rushwa
3.Watu na wananchi jirani katika migodi hii hawananufaiki chochote na wanazidi kuwa maskini.

Mada mahususi
1. The Tax System and its Hidden subsidies
2. Alleged Tax Evasion
3. Democracy and Transparency
4. Local economic development

Uhondo unapatikana zaidi ukiangalia jinsi walivyochambua mapato na uvunaji wa madini ya Dhahabu kutoka migodi ifuatayo

➡️AngroGold Ashanti, kampuni inayomilikiwa kwa ubia wa Ghana na South Africa hawa wanamiliki migodi ya GGM huko Geita
➡️Barrick- hii ya Wakanada wanamiliki mgodi wa Bulyankulu
➡️Australian company wanaomiliki Migodi ya Dhahabu ya North Mara under East African Gold Mines brand.

Pia wameongelea "The Buzwagi contract"

Ktk takwimu zao kwenye majedwali mbali mbali wame extraxt data na taarifa kutoka kwenye vyanzo mbali mbali ikiwemo
Tume ya Taifa ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Tanzaniani Chamber of Mines, Tanzania Revenue Authority TRA.

Jambo lingine lilonishangaza ktk ripoti hii ni kuwa matatizo yanayotokana na migogoro na Machimbo ya madini ya Dhahabu yanafanana ktk Nchi nyingi za Africa, ambapo inaonekana baadhi ya viongozi ktk nchi hizo wanashirikiana na wezi wa kigeni na kudidimiza wananchi wao.

Basi mwisho wakamaliza na Recomendations zao.

Walitoa mapendekezo 7.
Ukitazama kwa umakini ni Copy and Paste ya zile za Tume ya Uchunguzi ya Prof Usoro na Prof Mruma.

Hii ni repoti ya mwaka 2008 toleo la pili.
Ahsante sana mkuu 'Bush...'. Mada za namna hii ndizo zingeheshimika sana katika jukwaa kama hili hapa JF.

Wakati nikisoma maelezo yako, nikawa naingiwa na dukuduku la kutaka nikwambie usipige stori ndefu, tuwekee tune wenyewe. Kumbe hapo mwisho umefanya kweli.

Nchi yetu Tanzania sasa kuna ombwe kubwa sana la wasomi/wana siasa wa aina ya Tundu Lissu. Watu wameweka elimu zao pembeni na kujikita katika kuwa maroboti tu ya kutumiwa na wanasiasa hata wasiokuwa na kitu kichwani.
Katika mawaziri tulio nao/tuliowahi kuwa nao, ni wangapi wametumia taaluma zao hata kuchapisha tu makala kwenye gazeti la kawaida?

Kwa hiyo, ninapoona mtu, kama Tundu Lissu akijipambanua kuwa tofauti kabisa na wengi wengine, hiyo inanipa matumaini makubwa. Ni muhimu taifa letu lirudi kwenye misingi yake. Watu watumie elimu waliyo nayo katika kulijenga taifa hili.

Sijawahi kuona andiko lolote la maana toka kwa:

Kikwete; kabudi, Samia, Nchemba Madilu, na wengi wengine wanaotupigia kelele kila siku Bungeni na kwenye Baraza la Mawaziri, CCM na kwingineko.
Naheshimu, uwezo wa Zitto Kabwe (ukiweka mbali siasa zake).

Kwa hiyo, Tundu Lissu ni tofauti kubwa sana na hawa wengine wote kwa sasa.
 
Humu JF wamo wengi tu , naelewa akina Lissu walikuwa mbele kuwateteta

..Lissu ameeleza mambo mengi sana kutetea Wazanzibar.

..Kutetea mpaka haki za wakina Abdulah Kassim Hanga na wenzake waliouawa wakati wa Sheikh Abeid Karume.

..Sio sahihi Wazanzibar kumchukulia Lissu kama adui anapotetea haki za Watanganyika.
 
Kwa Taarifa tu ni kuwa Lissu wanamkubali sana Wanzanzibar na Youtube Channel nyingi zinatembelewa na Wazanzibar as long as zinaongelea mambo yao.

Yaani kuna baadhi ya mitaa wanatune Youtube kwa makundi kusikiliza Hotuba zake.
 
Kwa hiyo, ninapoona mtu, kama Tundu Lissu akijipambanua kuwa tofauti kabisa na wengi wengine, hiyo inanipa matumaini makubwa. Ni muhimu taifa letu lirudi kwenye misingi yake. Watu watumie elimu waliyo nayo katika kulijenga taifa hili.
Umeeleza vizuri sana Mr Kalamu na kuonesha umuhimu wa kutumia Elimu kama Chachu ya kuleta fikra mpya na maendeleo.

Hii ndio ng'ao pekee inayotumiwa na Wazungu kusonga mbele kwenye Nchi zao.

Umemtaja Dr Kikwete, Dr Samia na Dr Mwigulu Nchemba, naamini wanayo mengi ya kushare nasi labda wanakosa Motivation.
 
..Lissu ameeleza mambo mengi sana kutetea Wazanzibar.

..Kutetea mpaka haki za wakina Abdulah Kassim Hanga na wenzake waliouawa wakati wa Sheikh Abeid Karume.

..Sio sahihi Wazanzibar kumchukulia Lissu kama adui anapotetea haki za Watanganyika.

Tatizo ni watu kutomfahamu hasa kauli Zake zinapoungana na Mbowe ambaye huingiza dini
 
Mimi hushangaa sana namna Botswana ilivyo nikilinganisha na Tanganyika , hasa uchumi wake unategemea dhahabu na almasi , Tanganyika toka wakati wa Nyerere hakuna kilichopatikana zaidi ya kuundwa CCM baada TANU na kutembeza mwenge kila mwaka
Ni lazima ushangae, kwa sababu hujui mchango mkubwa uliofanywa na Tanzania katika ukombozi wa bara hili.
Unalinganisha Botwana, huku hujui Botswana ni nchi ya watu wachache sana. Ndiyo, Botswana wamefanikiwa sana na sababu kubwa ni utulivu wa viongozi wao wa juu. Hapa kila ukiongelea habari za Tanzania, unachojuwa pekee ni Mwalimu Nyerere, kana kwamba ndiye anayeongoza nchi hii miaka yote hii.

Botwana walitegemea na wanaendelea kutegemea Almas na ufugaji wa ng'ombe toka enzi zote. Tanzania tumekuwa tukitegemea vitu gani?
Kahawa, ilidorola Brazil ilipochukuwa soko. Mkonge ukakosa soko, kwa sababu waJapan waligundua 'synthetic fibres'; vile vile na pamba!

Sasa mtu usiyekuwa na fikra timamu unakuja hapa na kujionyesha wewe ni mjuwaji, kwa lipi?

Leo nipo tayari na wewe. Tuendelee.
 
Umeeleza vizuri sana Mr Kalamu na kuonesha umuhimu wa kutumia Elimu kama Chachu ya kuleta fikra mpya na maendeleo.

Hii ndio ng'ao pekee inayotumiwa na Wazungu kusonga mbele kwenye Nchi zao.

Umemtaja Dr Kikwete, Dr Samia na Dr Mwigulu Nchemba, naamini wanayo mengi ya kushare nasi labda wanakosa Motivation.
EEEEnHEeeeee!

Kuna 'motivation' zaidi ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi? Hiyo ni 'motivation' tosha kabisa ya kukusukuma utumie elimu yako katika kuinua maisha ya wananchi unaowaongoza.
 
EEEEnHEeeeee!

Kuna 'motivation' zaidi ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi? Hiyo ni 'motivation' tosha kabisa ya kukusukuma utumie elimu yako katika kuinua maisha ya wananchi unaowaongoza.
Hiyo ni External, kuandika na kushare kile unachokifahamu inahitaji Self Motivation, the Inner Instincts
 
Tatizo ni watu kutomfahamu hasa kauli Zake zinapoungana na Mbowe ambaye huingiza dini

..99% ya Waznz ni Waislamu.

..kuna watu wanatumia hali hiyo kama " kichaka " ili viongozi wa Ccm toka Znz wasikosolewe.

..Samia anayechangia wachungaji wa hovyo kama Mwamposa ndio wa kuwakausha makoo Waislamu kumtetea?

..Tujiulize Samia alikuwa wapi wakati Cuf wakipakaziwa kwamba ni chama cha kidini cha Waislamu?
 
Hahaha hii sasa mpya.
 
Hiyo ni External, kuandika na kushare kile unachokifahamu inahitaji Self Motivation, the Inner Instincts
'Philosophical' - hili tuliachie hapa. Litavuruga mada hii nzuri kabisa.

Binafsi ningeshukuru sana wakati huu akijitokeza msomi/wasomi wakachambua kwa kina kabisa manufaa Tanzania iliyokwisha pata toka tulipoanza kunadi madini yetu.

Pesa hii tuliyopata imefanya kazi zipi hasa za kusogeza mbele uwezo wetu?
 
..Ni mpya kivipi?

..Hujamsikia RC Chalamila kwenda Kanisani kwa Mwamposa na kutoa mchango toka kwa Mama Abduli?

..Ccm wanachezea sana akili za Watanzania kwa propaganda za udini na ukabila.
Wanafata wingi wa kura wala hawana dhima ya imani yoyote
 
'Philosophical' - hili tuliachie hapa. Litavuruga mada hii nzuri kabisa.

Binafsi ningeshukuru sana wakati huu akijitokeza msomi/wasomi wakachambua kwa kina kabisa manufaa Tanzania iliyokwisha pata toka tulipoanza kunadi madini yetu.

Pesa hii tuliyopata imefanya kazi zipi hasa za kusogeza mbele uwezo wetu?
Huo uwanja wa kujadili manufaa ya Madini Kwa Tanzania hautaruhusiwa maana utawavua nguo baadhi ya Watu
 
Gesi gani!?..huwa mnaongea vitu hamna details navyo,kwa Sasa tunamiliki gesi ya mtwara kwa zaidi ya 45%,gas ya Lindi mikataba bado,gesi gani aliyofelisha jakaya?
Kama ni kweli kwanini ushindi kama huu kwenye gesi umekuwa siri kiasi kwamba wanaofahamu umiliki 45%ni wewe tu na baddhi ya watu wachache?
 
Back
Top Bottom