A - Town Gangsters walioitikisa Arusha kwa matukio ya uhalifu

Juston si ndo mwenye jengo ilipo Equity Bank Arusha?, pia aliwahi kupata tender ya Maegesho Arusha? .

Naskia kunakipindi walimuhamishia Dodoma akitokea Kisongo

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Phalme na Fikirini Chonjo na hoteli yao Barracuda.

Arusha ulikuwa mji exciting sana miaka hiyo.
 
Hata mzee Mwinyi aliisafisha Moshi ya miaka ya themanini kwa kutoa greenlight kwa pgo kuwala shaba majambazi.

Ila kuuwa majambazi sio suluhisho la kudumu la ujambazi kwani inakuwa kama kukata kichwa cha yule Hydra wa hadithini.
Lakini ndio njia sahihi ya kusafisha takataka kwenye Jamii.South afrika, USA,Rwanda wamefanikiwa Sana kwa njia hio.Jambazi ni chombo cha kutestia bunduki kama Ina fanya kazi sawasawa
 
Haiwezi kua kazi yako sababu matukio hayo yote yanajulikana Arusha nzima, wewe sio wa kwanza kuyasimulia, sio kazi yako na acha kupoteza muda kutaka kupata credit kwa vitu ambavyo viko wazi tu.
 
Wewe unaijua chuga kindakindaki,fred jebi si alichomwa kisu
Fred Jebby hakuchomwa kisu Bali aliumwa sana mguu hadi umauti ukamfika.
Huyu mwamba hakuwa mwizi wala Jambazi , Na isitoshe Baba yake Fred mzee Jebby alikiwa polisi (trafik) maarufu sana hapa arusha ila tatizo LA Fred Jebby ni ubabe na ukorofi uliopitiliza yaani alikuwa haogopi MTU .
Baba yake tu ndio alikuwa anammdu Fred maana mzee wake ubabe anauweza
 
Hebu muelezeeni na askari wa kuitwa Chui kama sijakosea nasikia aliwahenyesha vilivyo majambazi hapo Arusha
 
Huyu msela mavi kweli.
Yule dogo aliyetobelewa macho na Scorpion kila mtu alikuwa anamuombea yamkute mabaya. Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa anaongoza kundi la wahalifu yaani vibaka wapora simu na mikoba ya wadada.

Hivyo yalipomkuta yale watu walifurahi ndio maana hawamkumsaidia.

Hivyo hawa wanaoishi vijijini huko na usela wao wanahisi Dar kunawezekana waje wajaribu kama watarudi ssalama.
 
Maisha ya Dunia ni kuukimbiza upepo tu.
Wapo wapi sasa
 
Story nzuri Ila lugha uliyotumia sio ya humu ya wahuni wenzako ambao bahati mbaya humu hawaingii
 
Kwa asiyejua anaweza akafikiri hivi visa ni maigizo ila ukweli maisha ya Arusha miaka ya nyuma yalikosa kabisa usalama, japo hadi leo hizo element hazijakwisha.
Kuna jamaa aliitwa Sunda, alikuwa maarufu sana kwenye madini miaka hiyo vip yeye hakuwa na visa? Maana sijaona alikotajwa.
Kuna jambazi aliuawa kwa risasi pale Sabato Maji ya chai aliitwa Kibonge, kuna mwenye habari zake?
Vipi pia kuhusu biashara ya uchunaji ngozi? Kuna jumba moja liko momella pale lilijulikana kama kwa Lyimo, huyo Lyimo ilisemekana alikuwa anadili na hizo biashara za kupoteza watu na kuchuna ngozi, yaani enzi hizo ilikuwa hakuna kutembea usiku kwa miguu peke yako, kuna mzungu pia pale Someli ilisemekana alikuwa anadili na hizo bizness, alikuwa na mashamba ya kahawa eti vibarua walikuwa wanapotea tu.
Bila kumsahau yule Mrefu aloimbwa na Mch. Faustine Munishi.
Mwenye nondo hizi azilete tafadhali.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 

Wahalifu wa aina hiyo wako duniani kote, sio Arusha tu. Marekani walikuwepo kina Al Capone, Lucky Luciano, Sammy Gravano, Tookie Williams, Raymond Washington, n.k.

Wadaresalama msijione wa kipekee sana. Bashite alifanya uhuni wa kipuuzi mara ngapi na hamkufanya chochote? Yule msukuma aliyefariki alitaka kugawanya jiji kimandazi mandazi, na hamkuthubutu hata kuongea. Hawa pia ni gangsters.
 
Do you think msukuma aliyefariki angefanya hivyo kwa Arusha mngefanyaje?

Usiongelee watu waliokwenye mamlaka kufanya yasiyofaa kwa kulindwa na dola ukadhani ni rahisi kama kudhibiti vibaka wenye silaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…