A - Town Gangsters walioitikisa Arusha kwa matukio ya uhalifu

A - Town Gangsters walioitikisa Arusha kwa matukio ya uhalifu

Hizo mambo ni za vijijini huko.... Eti unakaba unaenda kwenye kesi kuanzia wakili, mkuu wa wilaya sijui nani... Balozi, diwani woooote ni ndugu zako wa arusha.

Unaleta umafia unategemea ndugu,. Arusha ndogo saana usela wa vijijini tu uliwachanganya..


Njoo ufanye uo usee city centre we ni mwanaume.
Tulia dada huko daslam mmelegea sana huko daslam alijitokeza mtu anaitwa scorpion akamtoboa mtu macho hadharani lakin hakuna msaada wowote alioupata huyo mtobolewa macho sasa ndo ajitokeze mtu na shortgun mtamfanya nini?
 
Wewe ni mwenyeji wa Arusha?

Do you know what I mean?

Wewe ni mkongwe wa Arusha?

Unazijua “mbanga” za Arusha?

Unawajua hawa?

Kyusa, Zungu, Kababuu, Pengo, Mojaa, Juma Kipisi, Jumanne Mjusi, Sadiki Mkindi na Wengineneo?

Kwa mkongwe wa Arusha, nina hakika kabisa majina haya yamekusisimua sana.

That is a list of daring gangsters waliokuwa hawaogopi lolote linapokuja swala la Uporaji wa madini ya vito na pesa.

They didn’t care even to Kill their loved ones.

SADIKI MKINDI


Alikuwa ni handsome boy. Wengi walimchukulia kama “mtoto wa mama”

Lakini ungeambiwa matukio yake hakika mwenyewe ungebroo.

Familia yao ilikuwa ikimiliki majengo Mengi Jijini Arusha

Inasemwa hata kiwanja ulipo msikiti wa Bondeni ni chao..

Sadiki alisoma ulaya,

Naam, Sadiki alikuwa akiishi sweden ambapo alioa msweden pia.

Alikuwa pia akipiga madili ya drugs pale Sweden.

Akaja kuharibu!

Alimpiga na kumjeruhi vibaya mkewe.

Wakaunganisha na misala yake ya nyuma.

Sadiki akawa deported bongo.

Sadiki akarudi rasmi jijini Arusha.

Akaendeleza umafioso wake.

Familia yake ilikuwa na ushawishi hivyo ikawa inamlinda na kuogopwa na dola.

Dili yake ya kwanza ilikuwa ni kumvamia mzungu maeneo ya USA RIVER na kumpora madini na pesa katika tukio ambalo mzungu yule aliuwawa.

Katika Msala huu Sadiki alishikiliwa kwa muda mrefu kidogo kituo cha polisi.

Hakikujulikana ni katika mazingira gani, Lakini Sadiki akaja kuachiwa.

Alipotoka akajiweka mapenzini kwa mtoto Rose.

Waarachuga wenyewe wanaita Rosee

Rose alikuwa mrembo.

Sadiki akamharibu rose kwa kumlisha “maunga”

Pia Kwa wivu wa Sadiki Rose alijaa makovu ya viwembe na kuchomwa kwa pasi mapajani.

Rose akachuja

Rose akaiona jioni yake bila kupitia mchana.

Sadiki akamtelekeza

Sadiki akajiweka kwa mtoto mkali aitwaye Baby

Baba yake Baby alikuwa ni Meja mstaafu wa Jeshi aliyebobea maswala ya mizinga.

Aliitwa Meja

Familia ya baby ilifanya juu chini kumuhepusha Baby na Saidiki

Mapenzi upofu, Baby hakuhofu

Yaliyomkuta mamba na boko yatamkuta.

Hakika

Ni mpaka ulipofika usiku mmoja.

Usiku wa huzuni Arusha.

Baby alikuwa akipokea kipigo kutoka kwa Sadiki kwenye gheto lao.

Majirani walisikia kilio cha Baby.

Lakini nani wa kumfunga paka Kengele?

Majirani walijua Umafia wa Sadiki

Hivyo hawakusogea.

Baadaye pakawa kimya

Ukimya ule uliwahadaa Majirani wakajua “yameisha”

Lakini....

Ukimya ule ulidumu kwa siku tatu isivyo kawaida.

Kumbe mauti yalimkuta Baby tangu usiku ule wa kwanza.

Sadiki ana roho ngumu sana.

Unawezaje kukaa na maiti kwa siku tatu?

Kumbe Sadiki hakuwa bwege!

Alikuwa akifanya mipango jinsi ya kuukwepa ule msala.

Akahitimisha kwa kuita Taxi

Ilipofika akamuhadaa dereva kuwa Baby kazidiwa anahitaji kupelekwa hospitalini.

Safari yao ikawapeleka Mount Meru Hospital.

Walipofika mapokezi Sadiki akatoweka kusikojulikana.

Baadaye madaktari wakabaini kuwa wametelekezewa mwili.

Baadhi ya wagonjwa waliutambua mwili wa Baby.

Familia yake ikafahamishwa.

Mashuuda wanasema baba wa Baby Major Makange alijiapiza kuwa Baby atakuwa mhanga wa mwisho wa Sadiki. Na kama polisi wamemshindwa atamalizana naye.

Sadiki akatoweka jijini Arusha.

Polisi waliponda kusachi nyumba ya Sadiki wakakuta nguo za baby zilizokuwa na damu nyingi.

Hii inamaanisha kuwa Sadiki alimbadilisha nguo na kuusafisha mwili wa Baby kabla ya kwenda kumtelekeza hospitali.

Sadiki akakamtiwa Dar Akasafirishwa mpaka Arusha.

Familia yake ilishapoteza Influence Arusha kwenye kesi hii.

Mtu pekee aliyekuwa na influence alikuwa baba mkubwa wa Sadiki Brigedia Mkindi aliyekuwa mshauri wa mgambo mkoni Arusha.

Lakini naye hakusaidia kitu.

Mlinzi wa Mount Meru Hospital alidai kumtambua Sadiki kwa kuwa alimuona hospitalini pale alipolazwa kwa muda mrefu hospitalini pale akiugua TB wakati akiwa chini ya ulinzi kwa tukio la kumwibia mzungu wa USA RIVER

Mlinzi huyu alimuona Sadiki siku anatelekeza maiti ya Baby.

Shaidi mwingine ni alikuwa ni dereva taxi aliyekodiwa na Sadiki.

Majirani waliosikia ugomvi pia.

Daktari aliyefanyia postmortem mwili wa Baby ndiye aliyepiga msumali wa mwisho kwa kusema chanzo cha kifo ni kipigo kabla maiti haijatelekezwa hospitalini.

Ndugu msomaji, Kwenye kesi za mauaji, Kuna elements mbili ni muhimu sana kuthibitisha mashtaka.

Actus Reus/ kitendo kiovu. Lazima kiwe kimetendeka. Kwa kesi yetu Baby tayari alikuwa amekufa na kifo chake hakikuwa cha asili.

2. Mens Rea/ Nia ovu.

Mara nyingi si rahisi kwa mtuhumiwa kuiambia mahakama kuwa alikuwa na dhamira ya kuua.

Mahakama yenyewe hupima dhamira ovu kwa kuangalia mambo yafuatayo

Kusababisha majeraha hatari kwa maisha (grievous harm)

ii) Kushambulia maeneo ya mwili hatari kwa uhai (Vulnerable body parts)

iii) Nguvu iliyotumika kushambulia

iv) Mara ngapi umeshambulia? Ingawa hata shambulio moja linaweza kutosha

vi) Siraha iliyotumika na ukibwa wake

vii) Maneno aliyotamka mshambuliaji kabla, wakati ma baada ya shambulio

viii) Matendo ya mshambuliaji kabla, wakati na baada ya kushambulia

Maneno ambayo majirani walisikia Sadiki akimwambia Baby wakati anampiga akisema “nitakuua”

Na kitendo cha Sadiki kuutelekeza mwili hospitalini

Na kitendo cha yeye kukimbilia Dar,

Yote haya yalithibitisha NIA OVU

Sadiki akahukumiwa Kunyongwa baadaye ikawa kifungo cha maisha

Sadiki alitoka jela(sijui kwa njia gani) na amefariki mwaka jana.

Kabla ya umauti naambiwa kuwa alipooza upande mmoja.

Unahisi Story Imekwisha?

No! Ndio inaanza...

Arusha haikupoa!

Likafata kundi kabambe la kupora madini.

Hii sasa ilikuwa ni Kampuni kabisa, Walikuwa hadi na mwanasheria.

Ilikuwa hivi,

Kuna wakati Rais “mmachinga” alienda India kuhamasisha uwekezaji

Wahindi wakamchana kuwa hawawezi kuja kwani kuna mtu Arusha anaitwa JUSTONI NYERE(code) anawasumbua sana na amehatarisha sana maisha yao kwenye biashara ya vito.

Mmachinga akamvutia waya PM akimuuliza nani huyo anaitwa JUSTON NYERE aliyejitangazia Jamuhuri Arusha?

Vipenyo wakaingia kazini.

Njia kutoka Arusha mjini kwenda KIA ikawa under Surveillance.

Yakabainika Mengi yakihusisha maafisa madini wa Serikali

Akiwemo wakili HIGH MWELI

JUSTON MWELI alikuwa “manyamela” wafuatao;

Eugene(alikuwa mdogo wa ex minister), Iddy Mkulu, Abdilahi Musa aka BANJOO, Elisante, Gody Molel aka MOJAA, Kyusa, Kababuu, Pengo na Juma Mjusi.

Juma Mjusi aliitwa Mjusi kwa uwezo wake wa kufandia kuta akiwa anafaya Unyamela.

Ilikuwa ni bora ukutane na mtoa roho kuliko kukutana na manyamela hawa wakiwa kazini.

Mchoro ulikuwa hivi;

JUSTON NYERE alifungua kampuni ya kununua na kununua na kusafirisha madini.

Kampuni yake akaiita NMJ(code) na ofisi zake zilikuwa Golindoi Road

Kampuni ilikuwa gheresha

Alichokuwa akifanya JUSTON ni kujenga mahusiano na maafisa madini.

Ili madini yasafirishwe ni lazima maafisa hawa wasaini nyaraka za export.

Hapa ndipo game lilipokuwa linaanzia..

Maafisa hawa walikuwa wanamtonya JUSTON nani ameshaenda kwao na ni muda gani wamesign documents.

Taarifa hii ingemfanya JUSTON kumtuma dereva taxi mmoja aitwaye Martin pale ofisi ya madini chaap.

Actually Martin ni “nyamela” wa JUSTON anayezuga kama dereva taxi ili asibainike.

Yeye kazi yake ni kuwaungia mkia wenye madini baada ya kutoka kwenye ofisi ya madini.

Dereva Martin angewafatilia watu wale njia nzima kutokea Arusha kwenda KIA na njiani alikuwa akiwapa codes manyamela kina Banjoo ambao wanakuwa wapo maeneo ya polini katika njie ile.

Hapo Martin angekuwa kamaliza majukumu yake.

Do you know what Next?

Ungesikia tu habari redioni au kwenye TV kuwa kuna wafanyabiashara wa madini wamevamiwa na majambazi wakielekea uwanja wa ndege KIA.

Wala isingeshangaza pia kusikia kuwa tukio lile limepokonya uhai wa mtu.

Manyamela wanachukuwa madini na kurudisha kwa JUSTON

Juston kupitia kampuni yake anatafuta nyaraka kutakatisha madini yale.

Kisha madini yale yanasafirishwa kuuzwa USA Calfonia.

Mchezo huu ukampatia utajiri mkubwa Juston.

Si yeye pekee

Bali na swahiba wake wakili HIGH MWELI(code)

JUSTON na MWELI wakawa matajiri wa kuogopwa hata na PGO

Wakajenga uswahiba na mkuu wa PGO wakati ule bwana Ngunguri.

PGO gani mwingine angewagusa?

Wakanunua majumba, Mashamba na magari ya kifahari.

Manyamela wao wakaendeleza ukora hata sehemu zingine na wasiguswe.

Nyamela Mjusi alifikia hadi hatua ya kuvamia hospitali ya ITHINASHIR

Akaenda ofisi ya mhasibu na kukwapua Milioni 17 na kutokomea.

Arusha became a real city of gangsters.

Hakika walikuwa wanaelekea kujitangazia Jamuhuri.

Lakini hawakujua...

Kwamba wako mtegoni..

Likapigwa tukio....

Ofisi ya madini ya RIVER GERMS LTD ikamiwa...

Nyamera BANJOO akiwa mstari wa mbele akitumia Toyota Corolla TZL 8500

Banjoo ana kamwili kadogo sana,

Akiwa na mtutu anageuka “Hawafu mwenye nguvu”

Banjoo akapita mapokezi na kumwamuru ROSE MINJA ampeleke ofisi ya Mkurugenzi wa RIVER GERMS LTD ambayo iko ghorofani.

Kule juu ulitembea unyama mwaisa!

Pamoja na kibano Mkurugenzi kagoma kufungua safe

Banjoo akailipusa safe kwa mtutu.

Akakomba Tanzanite na Green ganet akasepa

Kwa kuwa tayari kundi lile lilikuwa linafatiliwa kwa macho makali kutoka kwa namba moja,PM na vipenyo, wala haikutumika nguvu kubwa.

Ni kwamba JUSTON alipigiwa tu simu ya kuitwa polisi.

RPC Arusha wakati ule akiwa ni MBEKO

Inasemekana huu mkasa ulimgharimu MBEKO asipande cheo.

JUSTON alipofika polisi akashamgaa anaambiwa avue viatu.

Yaani Rais wa Arusha avue viatu sentero?

Hakika JUSTON akaona ule ni mzaha.

JUSTON akagoma...


Akasema ngoja awapigie simu “vifaru” wake

Hakuna aliyepokea simu...

Hata Ngunguri..

Wote waliingia mitini.


Yes! Waliingia mitini..

Waliingia mitini kusikia mmachinga ana mkono wake.

Wakamuacha JUSTON kisiwani bila mtumbwi wala kasia.

Kesi ikaunguruma Arusha.

Wakati ule Jaji IRVIN MUGETA akiwa ni Resident Magistrate Arusha.

NYELI akawa anatetewa na mkola mwenzie wakili MWELI

Lakini hakimu Mugeta hakufanya hajizi...

Akawalamba Nyeri na manyamela 30 yrs


Africa Mazonge na Bongo bahati mbaya...

Yes! Bongo bahati mbaya

No! Sio bongo bahati mbaya bali Sheria bahati mbaya

Alianza kutoka JUSTON kwa rufaa baada ya kusota jela karibu miaka mitano

Baadae wakafata kina Banjoo

Nasikia Banjoo baadae aliajiriwa kampuni ya AFGEM

Lakini ukora wao waliendeleza kimya kimya.

Mkwere naye akawavalia njuga.

Akakamatwa wakili Nyeri akiwa na bilioni 17 alizoshindwa kuzitolea Maelezo. Pia akakutwa na magari kibao ya kifahari.

Kwa upande mwingine wale manyamela pale Arusha wakawa wanapelekwa puta na afande SABASITA baba yake na dada mrembo aitwaye TUNDA

Kwa kuwa wakili wao alishakuwa ndani na huku Saba sita anawanyima usingizi, Kuna wakati ilimlazimu Juma Mjusi kujisalimisha bungeni kwa naibu waziri wa usalama wa raia Mohamed Aboud.

Mjusi

Juma Mjusi akamwambia waziri kuwa anahisi maisha yake yapo mashakani kwani polisi wanamsakama.

Ndio ilikuwa pona yake. Kwani SABASITA ilikuwa ukiingia kwenye 18 zake anakupokonya uhai.

Juma Mjusi akawekwa chini ya ulinzi na kusafirishwa hadi Arusha kwa kamanda Basilo Matei akakaakaa ndani kwa muda na nasikia sasa hivi ni mwanaCCM kindakindaki akiwa green guard. Sabaya kamtumia sana kwenye mishe zake.

Mjusi

JUSTON naye alijaribu kugombea ubunge kwa CCM lakini jina likakatwa.

Arusha ya sasa imepoa sana kwa kweli.


Ongeza wengine unaowakumbuka
Kuna vitu umeongea vya uwongo sana chusa hajawahi kua kibaka au nyamera,mwale hajawahi kuua mtu wa karibu wa nyari zaidi ya kua mwanasheria wake alipopata kesi...kesi ya mwale ni pesa zilitoka nje ya nchi na kuingia kwenye acc yake.
Banjoi hajawahi kua muajiriwa wa tanzaniteone kaja mererani 2013 kuzama kwenye mgodi wa manjulu.
Moja ni fala tu wala hana ujanja zaidi ya huko mtaani kwao daraja mbili
 
Kuna george (kindei)huyu siku moja aliitwa na baba yake mdogo pale crocodile bar,baba yake akawa anajaribu kumuonya kuhusu vitendo vyake vya kihalifu,kindei akamsikiliza mzee wake halafu mwisho akamwambia,poa mzee nimekusikia ila ndio umeshachelewa hivyo,mimi siyo tena yule wa zamani" baada ya kumwambia hivyo akainua koti lake refu akimuonyesha mzee "jembe" short gun imetulia hapo,mzee akatoka kama mkuki, mwingine aliitwa spider,huyu alikuwa malaika kimwonekano,ila ukikutana na majambazi wenzake wanamheshimu na kumwogopa kwa ukatili wake huyu aliuwawa kikatili kabisa!alishindiliwa mkuki shingoni ukanasa kwenye tairi ya lori,mwingine alishindiliwa tumboni,akapitishwa katikati ya tairi mbili kubwa na kupigwa kiberiti,alibaki mguu mmoja tu na raba yake ya new balance,kindei alitulazimu kuchangishana hela mtaa mzima ili kununua bunduki ambayo kweli ilikuja kufanikiwa kumuua,majizi yalikuwa mengi sana arusha enzi hizo,inshaallah sasa hivi tunaishi kwa amani.
Mitaa gani hiyo
 
Tulia dada huko daslam mmelegea sana huko daslam alijitokeza mtu anaitwa scorpion akamtoboa mtu macho hadharani lakin hakuna msaada wowote alioupata huyo mtobolewa macho sasa ndo ajitokeze mtu na shortgun mtamfanya nini?
Sasa unashangaa hii... Mbona arusha mwanaume kaolewa na hakuna kitu mlifanya..... Au mliunga mkono hoja.!?

Au wanaoibiwa madini mbona hakuna kitu mlifanya;?


Arusha hakuna kitu... Pengine ni ufala wa kutotembea ukajifunza we ni kujifungia arusha tu... Utaelewa nin.

Usela mavi tu.
 
Kuna vitu umeongea vya uwongo sana chusa hajawahi kua kibaka au nyamera,mwale hajawahi kuua mtu wa karibu wa nyari zaidi ya kua mwanasheria wake alipopata kesi...kesi ya mwale ni pesa zilitoka nje ya nchi na kuingia kwenye acc yake.
Banjoi hajawahi kua muajiriwa wa tanzaniteone kaja mererani 2013 kuzama kwenye mgodi wa manjulu.
Moja ni fala tu wala hana ujanja zaidi ya huko mtaani kwao daraja mbili
Safi man..... Elekeza madogo.. wanasikiliza story za chindo na donii wanakuja kusimulia
 
Aisee hii dunia ina watu, mimi nikimuona mtu anatumia kisu tu kupora namkwepa mita mia sipiti nae njia moja,
INSHORT SINA HISTORIA YA WAHARIFU .
 
JUSTIN NYARI,tushawahi kwenda ofisini kwake kitambo sana tulimpelekea rhodelite aliwaka sana,pesa sasa ikawa mtihani
Akataka tumwachie mzigo,alikuwa dhuluma
Anaweza kupa hela na badaye akakutumia watu wakupore wanarudisha kwake...
Nakumbuka tulipotoka ofisini kwake watu tulinyoosha Nairobi moja kwa moja....
Alibaki nyuma kablow tu


Ova
 
Back
Top Bottom