Kwenye simulizi yako umeweka too general ngoja na mimi nielezee kwa ufahamu wangu kuhusu chuga gangsters:
Sadick Mkindi ni legend mtoto wa mzee Mkindi familia maarufu na tajiri Arusha huyo ni mdingi alifanya uhalifu in late 80’s na early 90’s
Majambazi walikuwa kina Chonjo maarufu kwa wizi wa magari, Bob Sambeke, Alex Massawe, Nyari....
Ila kuna hawa magangster wezi na wababe wa mitaani
Alikuwepo Hamis Mtotoo alikuwa anaibia sana wazungu aliuliwa na polisi relini watoto wa Pangani na Bondeni tunamjua vizuri.
Alikuwepo nyokaa alikuwa mwizi hatari katesa sana mianzini, sakina, ilboru na sanawari aliuliwa na polisi sakina
Alikuwepo Tumboniiii alitesa ngulelo, kimandolu kijenge nafkir na yeye aliuliwa na polisi ngulelo
Ngarenaro alikuwepo Mbalulaa alikuwa na mbio hatari akikwapua humshiki
Kuna kundi la wababe hawa hawakuwa wezi ila wababe hatari waliwakosesha raha watu sehemu za starehe kama mawingu club kijenge,roasters garden uzunguni, crystal club, metropole, sabasaba nk miaka ya mwishoni 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000
1. Iddi Mkuluuu (RIP) na kundi lake la Kaloleni gym,huyu bro alikuwa baunsa bonge la mtu mbabe hatari
2. Farijala Athumani(Papaaa) mtoto wa Ngarenaro bdae kijenge alikuwa anapiga kick boxer hatari alikuwa akikupiga kichwa lazima uanguke aliuliwa kwa kuchinjwa pale mtaa wa Jaluo
3.Fredi Jebi na Kabelo walikuwa watoto wa line police fire wababe walikuwa wanapiga gujuruu sio za nchi hii waliwatesa mno watoto wa kishua mjini kina Soican, Yusuph Mirambo, Valee Tango, Alkesh etc. Fredi Jebi alikufa kifo cha ajabu mguu uliota tende na ndio ukawa mwisho wa ubabe wa Kabelo
4.Baba Kisioki “babaaa” alkuwaga bondia na mbabe huko sinoni, lemara, njiro na kijenge ckumbuki nini kilimuua
5.Kingkola alikuwa mbabe hatari alikuwa anchezea timu ya Ngarenaro inaitwa “wayamkali” mpira hauishi kama kingkola hajapiga tiktatka
Wengine ni kina Omary manjiwaa, sele kishugaa pia kulkuwa na dogo aliitwa Regaa au Julius mambwaa alikuwa kapurwa lkn mbabe hatari alikuwa anatembea na mbwa zaidi ya 20.
Makundi maarufu yalikuwepo ka Kossovo chini ya Festo watoto wa Kambi ya fisi, maghoro na makao. Nako2Nako watoto wa kaloleni “Ololoo”, wakudisi watoto wa bongonyoo na Ungaltd kulikuwa na watoto wa blood ring Esso, watoto wa cheka ung’atwe Sombetini. kuna watoto wa Sing’isi walikuwa wanakaa sana tengeru walikuwa ni kwikwi tesa sana watu waliokuwa wnaenda beach party Duluti
Siku hizi haya magenge yamekufa ila waliobaki hatari ni vijana wa “tatu mzuka” wako kokote omba Mungu usikutane nao