Miaka ya 80 kuna jambazi aliitwa Nyau, katika mazindiko yake alilishwa moyo wa paka. Akikurukia shingoni alikaba na kurarua kama paka. Huyu jamabazi aliteleza mikononi kwa PGO kama nyoka anavyoteleza mikononi mwa mwanadamu.
Alikua na hirizi hiyo akiivaa risasi zilikua zinapita bila kumdhuru. Alikinukisha Dar na kwenda kujificha Tanga vijijini huko kwa wakwe zake.
Aliuzwa na mke wake, mke wake alikula dili na wajomba kuwa akiwasaidia kumkamata yeye hatakua na hatia. Aliwaambia akiwa amevaa hirizi yake hamuwezi kumkamata.yupo wapi siku hizi
Basi bwana alikaa ndani muda wote, kuna siku mke wake alimwambia si aende nje akapate fresh air, jamaa alitaka kuvaa hirizi mkewe alimwambia unavaa ya nini si unaemda hapo tu. Kumbe nje wajomba wamezunguka nyumba usawa wa vichaka.
Nyau alikamatwa kizembe sana bila hirizi yake.