Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
491
Reaction score
1,907
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
 
Aisee! Huyu celeb ndiyo namskia leo
Ni mtoto wa 2000 huwezi kumjua ni katoto kadogo kalikua mamton kwa hio hata Mbagala anaweza asipajue na kupasikia usishangae ukimwambia Washington DC labda anaweza kukwambia amefika na hatokei Tandale ni kule upande wa Pili wa movie Mlimani City sio Banda Umiza
 
Aisee! Huyu celeb ndiyo namskia leo

Mimi siku moja nilikuwa napitia kwenye ukurasa wa UNICEF TANZANIA, ndio nikakuta kabinti kanaongea kiingereza kizuri sana. Kufuatilia nikajua ndo hako mtoa hoja anaongelea. Ndio nikajua kumbe ni kasanii hapa nchini.

Kwa vile sio muumini wa huu mziki wa vijana, sikufuatilia sana
 
Ni mtoto wa kishua kwa hio habari za uswahilini anazisikia sikia tu uswahilini hajawahi kufika kwa hilo simpingi
 
Hata mimi sijawahi kula miguu ya kuku wala kichwa chake, firigisi nakula kiasi sio mpenzi, sipendi kidari, kwenye kuku napenda paja na shingo,

Je, mimi ni nani?😄
Wewe wa kishua huku uswahilini hivyo ulivyosema huli hatupiwi mbwa ndio vyakula penda mpaka utumbo wa kuku watu wanafakamia safi sana na wananenepa balaa
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
Huyo bint ni level nyingine, Kuna siku aliulizwa hua ananunua nguo za bei gani sijui akajibu hua haangalii wala kuuliza bei, ikimpendeza tu anatoa kadi analipia 😀

Wakati wazee wa pangu pakavu mgahawani tu, kila kitu hii shingapi hii shingapi 😀
 
Umasikini mbaya sana.

Kwa maisha ya watanzania yalivyo magumu,mtu akisika stori kama hizi za mtanzania mwenzao wanaona kama anaigiza.

Huyu Binti ukimsikia tu akiongea accent yake ya kiswahili si ile ya kibantu na anachapia sana maneno ya kiwahili,means either hajakulia bongo au ni wale mboga Saba kupitiliza.

Mtu kama huyu akisema hajawahi kusonga ugali mnamshambulia kwa matusi.

Akisema hapajui mburahati na hajawahi kupasikia mnamshambulia. Kuna Binti niliwahi kuwa nae kwa mahusiano anasema hapajui kabisa mbagala na kazaliwa Dar. Mbagala na umaarufu wote lakini Kuna watu hawapajui kabisa na Wala siyo celebrities,sembuse mburahati au kigogo.

Akisema hajawahi kula miguu ya kuku na firigisi mnaona ana pretend,sasa miguu ya kuku nayo ya kujisifia na kuanza kumshambulia mtu akisema hajawahi kula? Kwa nyama Gani iliyonayo mtu ukitafuna utadhani unatafuna peni ya speedo.

Huyu Binti anashambuliwa sana mitandaoni na wabongo ,ila yote hii ni kwa sababu ya kuona vitu kama tulivyo(umasikini) badala ya kuona vitu kama vilivyo.
 
Huyo bint ni level nyingine, Kuna siku aliulizwa hua ananunua nguo za bei gani sijui akajibu hua haangalii wala kuuliza bei, ikimpendeza tu anatoa kadi analipia 😀

Wakati wazee wa pangu pakavu mgahawani tu, kila kitu hii shingapi hii shingapi 😀
Ushua ushua mwingi mwanangu na wewe mjazie mwanao vibunda ili asiulize sana bei
 
Huyo bint ni level nyingine, Kuna siku aliulizwa hua ananunua nguo za bei gani sijui akajibu hua haangalii wala kuuliza bei, ikimpendeza tu anatoa kadi analipia 😀

Wakati wazee wa pangu pakavu mgahawani tu, kila kitu hii shingapi hii shingapi 😀
Na anachosema ni sahihi. Suala la kupunguziwa bei ni letu sisi makapuku. Wenye ukwasi wao huwa wanasoma tu price tag wanatoa kadi wanalipa na kuondoka.
 
Umasikini mbaya sana.

Kwa maisha ya watanzania yalivyo magumu,mtu akisika stori kama hizi za mtanzania mwenzao wanaona kama anaigiza.

Huyu Binti ukimsikia tu akiongea accent yake ya kiswahili si ile ya kibantu na anachapia sana maneno ya kiwahili,means either hajakulia bongo au ni wale mboga Saba kupitiliza.

Mtu kama huyu akisema hajawahi kusonga ugali mnamshambulia kwa matusi.

Akisema hapajui mburahati na hajawahi kupasikia mnamshambulia. Kuna Binti niliwahi kuwa nae kwa mahusiano anasema hapajui kabisa mbagala na akazaliwa Dar. Mbagala na umaarudu wote lakini Kuna watu hawapajui kabisa na Wala siyo celebrities,sembuse mburahati au kigogo.

Akisema hajawahi kula miguu ya kuku na firigisi mnaona ana pretend,sasa miguu ya kuku nayo ya kujisifia na kuanza kumshambulia mtu akisema hajawahi kula? Kwa nyama Gani iliyonayo mtu ukitafuna utadhani unatafuna peni ya speedo.

Huyu Binti anashambuliwa sana mitandaoni na wabongo ,ila yote hii ni kwa sababu ya kuona vitu kama tulivyo(umasikini) badala ya kuona vitu kama vilivyo.
Tunaangalia kipaji hayo mengine ni udaku usio na maana kiufupi ana kipaji itoshe kusema hivyo mengine ni kuchimbana ovyo tu
 
Back
Top Bottom