Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Another fool, unafikiri dar tu ndo kuna ushuani? Ushamba mzigo,
Pumbavu kenge wewe mporipori,
Huko maporini kwenu ni makazi yaliyochangamka, narudia hakuna mfano wa Oysterbay, Masaki, Msasani wala Mikocheni, mpaka kesho hata Mbweni ni majengo tu makubwa lakini haitafikia thamani ya kiwanja wala nyumba za hayo maeneo.
Narudia tena hakuna ushuani mikoani na hataikaa itokee,
 
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Hata Mimi sijawahi kula miguu ya kuku na firigisi.
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
Mie nikiona mchuzi au soup ina miguu ya kuku baasss hapo hata hamu ya kula inaniisha. Hivyo ikitokea nimeletewa kuku wa kienyeji ameshatengenezwa kukiwa na miguu ya kuku na kichwa natoa.
Yaani hata ile sight basi mimi inani disturb.
Ila firigisi napiga fresh
 
sahihi mimi nilianza kula matembele nikiwa mkubwa kabisa.
Kigogo nimekuja kukujua nina watoto.
Temeke sijui mbagala nimefika nikiwa mkubwa kabisa chuo sijui.
Jamani kuna watu maisha yalikuwa ni wilaya ya kinondoni tu, tukienda wilaya nyingine ni Upanga.
Nini ajabu sasa ?
Lazima kwani kupajua Mburahati? Hapajui ndio!
lazima kula miguu ya kuku?hajawahi kula ndio!
 
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Mie nipo zanzibar miaka telee na kina sehemu naziskia tu pasi na kuzijua.
Sehemu nyengine ndio naziskia hivi ukubwani na huwa nauuliza hio iko wapi Unguja au Pemba, ipo mjini au shamba!
Inategemea na maisha uliokulia mkuu. Wengine wanakuwa wanajua njia ya kwenda skuli na kurudi tu
 
Hey ndugu mshabiki, naomba niseme kitu kimoja ninachokiona Mimi.

Huyo binti anaweza akawa hayuko sahihi kama ambavyo hao wanamshambulia hawako sahihi na hata nyie watetezi wake pia hamko sahihi kwenye utetezi wenu.

Kwanza kabisa akiwa kama msanii anapaswa kujua watu(watanzania) wanaofuatilia Muziki wake ni watu wa aina gani kwanzia uelewa mpaka zao za kimaisha zikoje na vitu ambavyo mara nyingi vinawafanya kuwa hypersensitive.

Ni jambo ambalo liko wazi hakuna kitu ambacho kinamfanya mtanzania hasa wa Hali ya chini kutoa sensitive reaction kama pale anapohisi unamkebehi kuhusu Hali yake ya kimaisha( naomba unielewe hapa), mtanzania ukiongelea habari za kutokula baadhi ya vyakula ambavyo yeye ndio chakula Chake Cha Kila siku anahisi kama umemdharau sana).

Sasa huyo Abby champis sijui Abby champs kwa aina ya majibu anayotoaga ni obvious lazima wabongo wampopoe maana majibu yake Yana create negative feelings, sio kwamba wako sahihi lakini ndivyo jinsi walivyo.

Kwahiyo Sasa kuliko kuanza kujustify sijui ametoka familia ya kishua mara ooh kakulia nchi za nje inapaswa nyie washauri wake mumfundishe namna nzuri ya kujibu maswali ya aina hiyo yaani ajue kuingea nini na kwa wakati gani...

Mimi binafsi huwa simlaumu kutokana na umri wake. Na pia suala la yeye kukulia ushuani sio sababu ya msingi ya hicho anachokifanya maana yeye sio msanii wa kwanza kutoka familia ya kishua.

Mbona Navy Kenzo wanaotoka familia za kishua lakini hatujawahi kuona wakipopolewa na wabongo kama anavyopopolewa huyu Binti??? Kwani wao hawajaishi nje?

Jibu ni kwamba Envy Kezno wanajua kuishi na mtaa wakati huo huyo binti yenu hajajua kuishi na jamii ya kitanzania kwa namna inavyopaswa, na mbaya zaidi career yake Bado changa sana.

Mfahamishe tu kuwa hao Wala miguu ya kuku na firigisi wanaotoka Mburahati na maeneo mengine yenye hadhi ya Mburahati ndio mashabiki wakubwa wa Muziki wa bongo flavor na wao ndio wanaweza kuamua kupush Muziki wake au kumu hold back, hivyo haepuke kuwakwaza kwa namna yoyote ile hata bila kukusudia na pia vile vile ajifunze kiundani kuhusu uhalisia wa maisha ya watanzania wengi yakoje.
Wewe sasa ndo umesema.
 
Ni mfano tu, Mtu anayeishi mbagala, sio rahaisi kuifahamu Kimara Bonyokwa, au kuifahamu Kilungule.

Huyo binti yuko sahihi, kuna maeneo sio rahisi kuyafahamu kama huyatembelei au katika cycle yako hakuna mwenye interest nayo.
 
Miguu ya kuku na kichwa huwa napenda, bahati mbaya kabisa huwa hapa home akiandaliwa vinakatwa na kutupwa pia naona noma kusema nitengee miguu ya kuku au kichwa. Bahati mbaya nyingine ni kuwa siwezi kununua ile ya uswazi, hitimisho najikuta sijala miaka mingi
 
sahihi mimi nilianza kula matembele nikiwa mkubwa kabisa.
Kigogo nimekuja kukujua nina watoto.
Temeke sijui mbagala nimefika nikiwa mkubwa kabisa chuo sijui.
Jamani kuna watu maisha yalikuwa ni wilaya ya kinondoni tu, tukienda wilaya nyingine ni Upanga.
Nini ajabu sasa ?
Lazima kwani kupajua Mburahati? Hapajui ndio!
lazima kula miguu ya kuku?hajawahi kula ndio!
Upanga imekuwa wilaya lini?
 
umemaliza mkuu, ni suala la huyo binti aelekezwe tu kitu gani cha kusema in public kwa hadhira yake ambao 99% ni watz. Management yake wawe proffesional, azingatie nini cha,kusema mbele ya media.

hao waandishi wanamuuliza maswalivya hivyo ili wapate content tu, but management iwe inawapa limitation ya maswali cas mashabiki watamchukia kwa kuona kama anawadharau.
Sahihi kabisa mkuu, naona hiyo management yake imejikita zaidi kwenye kudeal na kipaji Chake atoe Muziki mzuri tu basi, na Wala hawajali kabisa mahusiano na audience yake yako vipi.

Muziki ni Zaid ya kipaji, mashabiki wana sehemu kubwa sana ya kuukuza Muziki wako hasa kwa bongo hapa, hivyo ni muhimu sana kujua behavior patterns pamoja na akili zao zikoje hili ujue namna ya kuishi nao.

Na namna nzuri ya kuishi au kuteka mashabiki ni kujifananisha na wao hata kama ni kiongo uongo, na sio kujitofautisha na wao.

Sasa wewe huwezi leo hii ukaropoka eti wewe hujawahi kula ugali na Wala kwenu hampikagi ugali, halafu utegemee positive reactions kutoka kwa watanzania wakati zaidi ya 96% wamekuzwa na huo huo ugali ambao wewe unaona si chakula Cha kula mtu.

Huyu Binti washauri wake wanapaswa kumjenga kwenye suala Zima la public relation, na wasikae tu kujustify majibu yake ya ajabu ajabu mara sijui kakulia masaki, yeye sio celebrity wa kwanza kukulia masaki walikuwepo akina king crazy Gk walikulia Oysterbay sijui Upanga lakini walijua kuishi vizuri na adhira ya bongo.
 
Upanga imekuwa wilaya lini?
Sehemu ikiwa ndani ya wilaya nyingine inaitwa jina la wilaya hiyo au jina la sehemu husika?
suala lilikuwa, ni kutaja eneo lililopo ndani ya wilaya tofauti na nilipozoea kufika
 
Back
Top Bottom