Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Wabongo kwa kutukuza umaskini.! cha ajabu nini mtu kutokula miguu ya kuku? mi mwenyewe pangu pakavu lakini miguu ya kuku, utumbo na kichwa hunilishi na sijawahi kula hii tangu utoto nyumbani wanajua.

sasa hapo ukisema public wabongo wataanza kukuponda.
 
Huyu dogo mnaweza dhani anaongopa ila ndo ukweli ulivyo kulingana na maisha aliyoishi...

Nakumbuka nikiwa chuo kuna jamaa wa kishua tulifahamiana hapohapo chuo kwa kuwa tulikuwa tunasoma kozi moja tukajikuta ni marafiki... Mi nilikuwa napenda sana kupiga misele maeneo ya uswazi nikamwambia twende nikakuoneshe maisha tuliyokulia sisi. Nikampitisha sinza, manzese mpka tandale

Kila chocho tuliyokuwa tunapita akawa anashangaa mpaka unahc km jamaa anawehuka... Alikuwa hajawahi ona watu wakifua kwenye vijito, kuchota maji ya kupikia mtoni, jinsi nyumba zilivyopangika hovyo na namna watu wanavyoishi

Mpaka tunamaliza mizunguko yetu mwamba alikuwa anatoa chozi. Namuulza vp anasema alikuwa anasikia watu ni masikini lakini hajawahi ona live na alichokiona kimemsikitisha sana kuona kumbe kuna watu wana maisha mabaya kuliko hata mbwa koko
 
Mbona hakuna cha ajabu hapo, miguu ya kuku wengi tu hatujawahi kula!
Huko mburahati akujue anaenda kufanya nini?
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
Hata mi sijawahi kula miguu ya kuku.
 
cha ajabu nini hapo sasa, kuto kula miguu ya kuku ni cha kushangaza, Dar wa salaam ina maeneo mengi huwezi kuyajua yote
 
Kawaida
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Kawaida alafu huyo ni mdogo bado na kwao mboga saba kweli..kwanza amesoma nje mwanzo mwisho.

Hajui vitu vingi hata boloyanki pia hajui mwacheni bhana.
 
Sijakula hiki, sijakula kile.

Ukila sausage tu ushakula kila kitu 🤣🤣🤣
 
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Ukiisha shiba miguu ya kuku, unaanza kusifu mama kwa kukuza uchumi.
 
Kwanza mtu uende Mburahati unafuata nini kwa mfano?
Kuna mwanangu kwao Mburahati alikuwa ananizimia sana stories zangu shuleni Tambaza.

Mimi kwetu Oysterbay nilikuwa sina ndugu Mburahati wala sababu ya kwenda huko.

Siku moja alinichukua shule Tambaza akanipeleka mpaka Manzese huko tukapita border mpaka Mburahati akanionesha kwao huko, tukafika shule moja ya primary jamaa alikuwa anafundisha tuition. Yani jamaa mwanafunzi Tambaza kumbe kule Mburahati na yeye anafundisha tuition watoto wa Primary.

Na jamaa wale watoto walikuwa wanamkubali sana na alikuwa anawachangisha kiasi kizuri tu, mpaka nikashangaa.

Ndiyo mara ya kwanza nafika Mburahati nilikuwa napasikia tu lakini nikasema huu mji wangu ni muhimu kujua sehemu mbalimbali na watu wanavyoishi.

Sio kila siku na hang out na kina Cool Moe Cee tu.
 
Huyu bila kiki hasikiki hata nyimbo zake hazifatiliwi alianza bifu na mario, akat bila yeye nyimbo isingeenda mjini akaja kwa paula, akaja yeye bikra sijui akaja kuhusu ugali,,,tid akamjib akahamia kwa tid now huku kwakifupi bongo bila kiki mziki hauend mjin zuchu mwenyew tu na kiki zake za Mond bila hivo taarab zake hazisikiki 🚮
 
Mkuu ndio leo nimeona umeandika comment, always we mzee wa kutoa like na kuscroll
images (1).jpeg
 
Mimi nina sio mpenzi wa nyama hivyo kwa hakika kitu ambacho sili na sijawahi kula kwenye kuku ni MIGUU, FILIGISI, SHINGO, KILE KIPANDE CHA MGONGO KUELEKEA NYUMA, mimi ni KIDARI TU na PAJA ( kama italazimika nile )
 
Sio lazima jamani wamuache mtoto
Kwani wamekosa vya kuhoji au ndo media zinakosa content wanaulizauliza vitu vya ajabu
Mimi na kuishi kote dar hiyo mburahati sijawahi kwenda, mtu kama huna kazi inayokupeleka huko unaenda kufanya nini..
 
Back
Top Bottom