Hey ndugu mshabiki, naomba niseme kitu kimoja ninachokiona Mimi.Umasikini mbaya sana.
Kwa maisha ya watanzania yalivyo magumu,mtu akisika stori kama hizi za mtanzania mwenzao wanaona kama anaigiza.
Huyu Binti ukimsikia tu akiongea accent yake ya kiswahili si ile ya kibantu na anachapia sana maneno ya kiwahili,means either hajakulia bongo au ni wale mboga Saba kupitiliza.
Mtu kama huyu akisema hajawahi kusonga ugali mnamshambulia kwa matusi.
Akisema hapajui mburahati na hajawahi kupasikia mnamshambulia. Kuna Binti niliwahi kuwa nae kwa mahusiano anasema hapajui kabisa mbagala na kazaliwa Dar. Mbagala na umaarufu wote lakini Kuna watu hawapajui kabisa na Wala siyo celebrities,sembuse mburahati au kigogo.
Akisema hajawahi kula miguu ya kuku na firigisi mnaona ana pretend,sasa miguu ya kuku nayo ya kujisifia na kuanza kumshambulia mtu akisema hajawahi kula? Kwa nyama Gani iliyonayo mtu ukitafuna utadhani unatafuna peni ya speedo.
Huyu Binti anashambuliwa sana mitandaoni na wabongo ,ila yote hii ni kwa sababu ya kuona vitu kama tulivyo(umasikini) badala ya kuona vitu kama vilivyo.
Huyo binti anaweza akawa hayuko sahihi kama ambavyo hao wanamshambulia hawako sahihi na hata nyie watetezi wake pia hamko sahihi kwenye utetezi wenu.
Kwanza kabisa akiwa kama msanii anapaswa kujua watu(watanzania) wanaofuatilia Muziki wake ni watu wa aina gani kwanzia uelewa mpaka zao za kimaisha zikoje na vitu ambavyo mara nyingi vinawafanya kuwa hypersensitive.
Ni jambo ambalo liko wazi hakuna kitu ambacho kinamfanya mtanzania hasa wa Hali ya chini kutoa sensitive reaction kama pale anapohisi unamkebehi kuhusu Hali yake ya kimaisha( naomba unielewe hapa), mtanzania ukiongelea habari za kutokula baadhi ya vyakula ambavyo yeye ndio chakula Chake Cha Kila siku anahisi kama umemdharau sana).
Sasa huyo Abby champis sijui Abby champs kwa aina ya majibu anayotoaga ni obvious lazima wabongo wampopoe maana majibu yake Yana create negative feelings, sio kwamba wako sahihi lakini ndivyo jinsi walivyo.
Kwahiyo Sasa kuliko kuanza kujustify sijui ametoka familia ya kishua mara ooh kakulia nchi za nje inapaswa nyie washauri wake mumfundishe namna nzuri ya kujibu maswali ya aina hiyo yaani ajue kuingea nini na kwa wakati gani...
Mimi binafsi huwa simlaumu kutokana na umri wake. Na pia suala la yeye kukulia ushuani sio sababu ya msingi ya hicho anachokifanya maana yeye sio msanii wa kwanza kutoka familia ya kishua.
Mbona Navy Kenzo wanaotoka familia za kishua lakini hatujawahi kuona wakipopolewa na wabongo kama anavyopopolewa huyu Binti??? Kwani wao hawajaishi nje?
Jibu ni kwamba Envy Kezno wanajua kuishi na mtaa wakati huo huyo binti yenu hajajua kuishi na jamii ya kitanzania kwa namna inavyopaswa, na mbaya zaidi career yake Bado changa sana.
Mfahamishe tu kuwa hao Wala miguu ya kuku na firigisi wanaotoka Mburahati na maeneo mengine yenye hadhi ya Mburahati ndio mashabiki wakubwa wa Muziki wa bongo flavor na wao ndio wanaweza kuamua kupush Muziki wake au kumu hold back, hivyo haepuke kuwakwaza kwa namna yoyote ile hata bila kukusudia na pia vile vile ajifunze kiundani kuhusu uhalisia wa maisha ya watanzania wengi yakoje.