Abdul Kareem Popat ndio sababu hasa ya Azam FC Kukosa mafanikio

Abdul Kareem Popat ndio sababu hasa ya Azam FC Kukosa mafanikio

Malengo yao mengine kabisa, tofauti na unavyofikiri wewe. Hiyo ni team ya kampuni siyo kama simba na yanga.

Azzam inajiendesha kibiashara zaidi siyo kishabiki.
bora umemsaidia
 
Swala la Bangala kushuka kiwango na kuwa na utovu wa nidhamu limeripotiwa na mwandishi nguli wa soka nchini Edo Kumwembe.
Siyo kushuka tu kiwango umri pia umemtupa na ni injuries prone
 
Abdul Kareem Popat amekuwa CEO wa Azam FC kwa zaidi ya Miaka 7. Huyu ndio CEO ambae hana presha kabisa ya kupoteza kazi yake kutokana kutopewa presha ya mafanikio pale Chamzi Complex.

Kipindi chote cha uongozi wake Azam FC imeambulia kikombe kimoja tuu cha FA (Azam Confederation Cup) mnamo 2019. Miaka yote ya uongozi wa Popat Azam FC imeshindwa kutwaa Kombe la Ligi na kushindwa kufuzu hatua ya makundi kwenye mashindano ya CAF Champions League au Confederation.

Tukumbuke Namungo imeshiriki mara moja kwenye Kombe la CAF Shirikisho na kupenya hatua ya makundi, na kwa maana hiyo Namungo anahesabika kama timu bora kwa Tanzania baada ya Simba na Yanga pale makao makuu ya CAF.

Popat amekuwa akishindwa hata kutengeneza benchi la ufundi la maana pale Azam FC, ndio maana hakuna kocha aliekuja na kudumu zaidi ya mwaka mmoja.

Popat pia amekuwa akifanya makosa makubwa kwa aina ya wachezaji anaowasajili. Alifanya hivyo kwa kusajili Ibrahim Ajibu mchezaji ambae hakuwa na lolote zaidi ya kuimbwa kwenye miziki ya singeli .

Msimu huu tena licha ya kujitahidi kwenye benchi la ufundi chini ya kocha Yusuf Dabo, lakini anarudia kosa kwa kwenda kumsajili Yanick Bangala kutoka Yanga.

Bangala ambae msimu juzi alikuwa MVP wa Ligi, lakini kiwango chake kimekuwa kikiporomoka na mwisho wa siku kuanza kusugua benchi. Bangala amesugua benchi huku akiwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Inashangaza sana Popat haoni hili. Pili Bangala amehusishwa na migomo ya chini kwa chini ndani ya Klabu ya Yanga. Amekuwa akifanya hivyo kwa kushirikiana na Shaban Djuma. Na wachezaji hao wote wameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jangwani.

Ni mtu mmoja tuu pale Chamazi haoni madhara haya hasi ndani ya uwanja na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo atakayoyaleta Bangala, nae ni Popat.

Kwa rasilimali ambazo Azam FC inazo basi ilikuwa inahitajika itawale soka la bongo na Afrika.

Inawezekana wamiliki wakina Yusuf Bakhresa na wenzio hawaoni haya madhaifu ya CEO wa timu yao. Ni bora wamuweke pembeni na kutafuta CEO mwingine. Nyota ya Azam FC ilikuwa inaanza kuchomoza lakini Popat anaanza kuizimisha kabla hata safari ya msimu ujao haijaanza.
Sawa amekuelewa tatizo ni Yanick Bangala
 
Inashangaza sana Popat haoni hili. Pili Bangala amehusishwa na migomo ya chini kwa chini ndani ya Klabu ya Yanga. Amekuwa akifanya hivyo kwa kushirikiana na Shaban Djuma. Na wachezaji hao wote wameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jangwani.
Ewe uto acha makasiriko kwa Popat kwasabb kachukua wachezaji toka Yanga. Nadhani mlitaka kuwanyanyasa hao wachezaji kama mlivyofanya kwa Feisal Salum
 
Ewe uto acha makasiriko kwa Popat kwasabb kachukua wachezaji toka Yanga. Nadhani mlitaka kuwanyanyasa hao wachezaji kama mlivyofanya kwa Feisal Salum
Mimi sio Uto.
Chamazi Complex moja hii
 
Ungeandika haya maandishi kwa herufi kubwa au ungeyabold kabisa.
Mwekezaji mkubwa Simba ni Mo Dewji, viongozi wengine wakuu ni Kina try Again ambae ni muislam.
Jangwani mwekezaji mkubwa ni GSM na rais hersi na makamu arafat haji ni waislam.
Je napo kuna udini?
 
WeSwala la Bangala kushuka kiwango na kuwa na utovu wa nidhamu limeripotiwa na mwandishi nguli wa soka nchini Edo Kumwembe.
Huyu angeifaa Simba, Azam wameokota dhahabu
 
Mkurugenzi Mkuu wa Azam ni TIDO MUHANDO... Sio Muislam
Azam wanaajiri watu wa dini tofauti na hata wasio na dini na wapo nchi nyingi Afrika na nje ya Afrika.

Hakuna Muislam anaebaguwa asiye Muislam.

Hivi tukianza kuwabaguwa mtaujuwaje uzuri wa Uislam?
 
Ametangazwa lini kuwa amerudishwa uyo bigirimana? Atuwezi kufanyia kazi habari za kwenye vijiwe vya kahawa, kila mtu utayemuona Avic town anapita zake utamuhusisha na yanga?
Dogo rudi hapa utuambie zile habari za vijiweni zimekuwaje tena official
 
Back
Top Bottom