Abdul Nondo alivyoshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Taifa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Abdul Nondo ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Taifa kufuatia uchaguzi mkuu wa ngome hiyo uliofanyika jana, Alhamisi Februari 29, 2024 kwenye ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo makao makuu ya ACT Wazalendo (Maalim Seif House) Magomeni, Dar es Salaam.

Nondo aliyekuwa anatetea kiti hicho ameibuka kidedea baada ya kupata kura 66 sawa na asilimia 55.4 ya kura zote, akifuatiwa na Julius Masabo aliyepata kura 45 sawa na asilimia 37.8 ya kura zote, nafasi ya tatu ikienda kwa Mhandisi Ndolezi Petro aliyepata kura saba (7) sawa na asilimia 5.8 ya kura zote, huku Ruqayya Nassir akipata kura moja (1) sawa na asilimia 0.8 ya kura zote.

Katika uchaguzi huo idadi ya wapiga kura ilikuwa ni 120 ambapo kura halali zilikuwa ni 119 na kura moja (1) imeharibika.
 
Hongera Nondo ingawa chama chako hakina harakati zozote za kuikomboa Tanganyika na influence yake Tanganyika ni negligible!
Hongera
 
Like father like son, baada ya miaka 5 ya kipindi chake atakuwa kazidi miaka 35 umri sahihi wa mtu kuitwa kijana.
 
Hongera Nondo kali. Umeonyesha ujasiri, Ulikuwa wa wapinzani wakali.

Uwateuwe katika sekretariet zako, watakusidia sana.
 
nimshauri ajikite kwenye siasa za staha
Ccm siasa za staha ni kumsujudia mwenyekiti, na viongozi wengine wa serekali. Yaani uchawa Sasa hivi ni staha ndani ya ccm.
 
ACT imepoteza sana mvuto baada ya kuunga mkono uamuzi wa Samia kuuza bandari zetu kwa DP World.
 
Sasa hii yatuhusu nini , tupo kwenye maombolezo kua na adabu ,pumbavu
 
Hivi saccos ya mzee Mbowe wana uongozi wa vijana?
 
Nondo=Kawaida wote ni ccm
 
Kijana makini na smart na mwenye weledi Wa m hali ya Juu .

I wsh think tank Kama hawa wapate nafasi za juu serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…