Abdul Nondo ashinda nafasi ya Uenyekiti Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo

Abdul Nondo ashinda nafasi ya Uenyekiti Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
UCHAGUZI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO


MWENYEKITI
Mgombea aliyeshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa ni Abdul Omar Nondo.

1.jpg

Mnamo mwaka 2018 Nondo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania wakati akiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam kwa kipindi hicho, aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa

Baada ya kupatikana alifunguliwa keshi yenye mashtaka mawili ambapo moja lilikuwa ni kutoa taarifa ya uongo kwa Afisa wa Polisi wa Kituo Mafinga akidai alitekwa na watu wasiojulikana na la pili ni kutoa taarifa za uongo mtandanoni kuhusu kutekwa kwake

Mnamo Agosti 2018, alikutwa na kesi ya kujibu dhidi ya mashtaka hayo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa. Novemba 2018 Mahakama hiyo ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia


MAKAMU MWENYEKITI
Seleman Misango ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara) wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo.

Khadija Anwary Mohammed ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Ngome ya Vijana ACT wazalendo (Zanzibar)


Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu kupitia Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo:
1. Monalisa Joseph Ndala
2. Salim Mohamed Shafi
3. Mbaraka Chilumba

Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu kupitia Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo:
1. Charles Paul Lowenge
2. Gora Shambuli Hamad
3. Hassan Abdallah Omar
4. Sharifa Mohamed Ali
5. Juma Haji Mmanga
 
Yes,

Alijijenga kupitia TSNP. He deserves !

Let's wait and see what he has to offer
 
Hongera kwake!! Ajipange ili October apate angalau kata (udiwani) au jimbo (ubunge) kabisa.
 
Wiston Mogha kwa hiyo amepigwa chini 🤣🤣🤣🤣🤣, anatumiwa kama toilet paper na Zitto
 
Hakuna mpiga kura atakaye ruhusu kikundi cha mtu kutawala, ni CCM tu imekuwa na inclusiveness ktk uongozi, CCM iko ki taasisi zaidi.

Tuwekee hapa majina ya mawaziri,makatibu wakuu wa wizara,wakuu wa mikoa,maras,wakuu wa wilaya,maded na wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya serikali. Pia tuwekee wajumbe wa halimashauri kuu ya CCM.

Vinginevyo dhana yako ya udini ni Uislam.
 
Back
Top Bottom