Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ficha ujinga wako. Labda kama ni mgeni sana wa siasa za nchii ndo unaweza kuandika huu ujinga.
Inawezekana wewe ndio mjinga kwa kukariri, ulimbukeni au ujuaji wa London-New York -Brussels back to Dar. Ila kichani mwako ni kakariri tu hata hujisubui kutafakar. Totally Western brainwashed low mind. Hiki kitu ndicho kinasumbua sana nchi masikini za kiafrika.
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.
Kuna dalili ya wazi ya Katiba mpya, huyu alikuwa kikwazo
 
Samia ni product ya Kikwete. Sasa team Kikwete akawa mgombea mwenza wa Magufuli na ndiye Rais wa sasa.

Katibu mkuu TISS aliyepita ni team Kikwete.

Kinana ni team Kikwete na ndio katoka umakamu mwenyekiti.

January, Nape, Makamba ni team Kikwete na mawaziri watatu wote walikuwa baraza la Rais Samia.

Mtoto wa Kikwete yupo kwenye baraza la Samia.

Haya tutajie mtandao wa Rostam Aziz na Lowassa uliokuwepo madarakani hata wakati wa Magufuli. Nchimbi kitu gani huyu mweupe hafikii hata nusu ya influence ya Makonda. Kwamba Rostam Aziz anamzidi Kikwete influence? Ndoto za mchana
Bado mtoto sana wa siasa za nchi hii.
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Kwa uma au Kwa ccm? !!!
 
Samia ni product ya Kikwete. Sasa team Kikwete akawa mgombea mwenza wa Magufuli na ndiye Rais wa sasa.

Katibu mkuu TISS aliyepita ni team Kikwete.

Kinana ni team Kikwete na ndio katoka umakamu mwenyekiti.

January, Nape, Makamba ni team Kikwete na mawaziri watatu wote walikuwa baraza la Rais Samia.

Mtoto wa Kikwete yupo kwenye baraza la Samia.

Haya tutajie mtandao wa Rostam Aziz na Lowassa uliokuwepo madarakani hata wakati wa Magufuli. Nchimbi kitu gani huyu mweupe hafikii hata nusu ya influence ya Makonda. Kwamba Rostam Aziz anamzidi Kikwete influence? Ndoto za mchana
Mbona ume panic?
 
Yusuf Makamba
January Makamba
Nape Nnauye
Kinana Abdulrahman

Hawa wanajuana sana ni kundi moja kwenye kupeana chapuo za uongozi

Kama ni mpasuko umetokea CCM kwetu ni habari njema ila kama wamewekwa pembeni kwa kazi maalumu kuelekea uchaguzi kwisha habari yetu
Mpasuko wa wazi kabisa huo
 
Back
Top Bottom