Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Pamoja na "shenanigans" za CCM, ukweli unabaki kuwa ukweli.

Wasaidizi wengi sana wa Rais Samia hawamkubali tokana na uwezo wake, na kwa kweli hili sio dhambi wala sio jinai.

Viongozi hawa ni ndugu zetu, wanaongea nasi ukweli toka mioyoni mwao mara kwa mara tunapokuwa kwenye mazungumzo nao.

Unafiki wetu mkubwa ndio unatufanya tuendelee na kazi na kumsifia.
Marope pia aliyasema hayo live
 
Who knows, usishangae Lukas Mwashambwa au FaizFoxy anauramba umakomo Mwenyekiti wa CCM, maana siku hizi UCHAWA unalipa sana.
Aaah siyo mambo yangu hayo kabisa. Hata ukatibu kata siuwezi.
hata raisi atapumzika pia na kumkabidhi P.Mpango (PhD) muda si mrefu, kila kitu kimepangwa wana-check boxes tu …
Mafao ya kufa mtu.

Raha mustarehe.
 
Ficha ujinga wako. Labda kama ni mgeni sana wa siasa za nchii ndo unaweza kuandika huu ujinga.
Mjinga ni wewe, huyo JK alishakata pumzi kabisa..... JK hana nguvu yoyote ndani ya CCM sana sana ni samaki tu asiyeweza ishi nje ya maji.
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Kuna yule pastor alitabiri mpasuko mkubwa ndani ya ccm naona yametimia
 
Back
Top Bottom