Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mnamkuza sana Kikwete ilhali ni mwepesi kuliko karatasi! Kikwete na mtandao wake ulimalizwa haraka sana na Magufuli akabaki hoi bin taabani.

Mtandao pekee ambao haukufa na Magufuli aliamua kusalimu amri kwao na kuungana nao ni Lowassa na Rostam Aziz ambao kijana wao mtiifu na mpendwa ndo huyo Nchimbi kwa sasa!

Huyo JK hana lolote mnalotaka kuaminisha watu zaidi ya mvizia fadhila tuu.
Wewe utakuwa kijana wa 2000 hii nchi hakuna kama kikwete ata 1995 alikuwa amemshinda Mkapa kama sio busara za Mwalimu Nyerere. In short kikwete Nchi anaifahamu kama kiganja cha mkono wake.
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.
Naiona nafasi ya urais kwa makonda kama bado yu hai...
 
Hoja Iko hapa: Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika...

Upinzani sijui kama wanaelewa!
Hata upinzani nao wanaweza kutumia Uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana, ni namna wanavyoweza kujipanga.
Umoja ndani ya CCM unapungua taratibu
Kazi kwao wapinzani
 
Ni Hekima na Busara Mh.Rais akalivunja Bunge tukafanya uchaguzi Mkuu kwa pamoja na ule wa Serikali za mitaa ili kuokoa fedha lakini pia kutengeneza Serikali yake kupitia watu wapya wenye maono ya kuijenga Nchi.
 
Back
Top Bottom