Adam alimzaa Kaini na Abili, Adam akaishi miaka mia tisa thelathini 930 ndipo akafa, katikati hapo aliwazaa watotot wengi ambao walisambaa kote duniani na hivyo ikawa raisi kumpata mtu wa kuoa, story hii iko vizuri katika kitabu cha mwanzo 5. karibu jisomee dont argue without facts.
Adam na hawa walikwepo eneo gani?
Ilikuwaje akafika America ambapo lazima uwe na boti kufika ukitokea Asia?
Alifikaje Australia? Madagascar? Na kuenea maeneo yote? Kwa sababu mabara hayajaungana.
Pia ilikuwa ni miaka gani?
Utafiti wiki iliuopita unasema jamii ya kale kufika Australia ilifika miaka ya 75,000 mpaka 100,000 kutokana na ushahidi wa mabaki ya mifupa ya kale.
Pia adam na hawa walikuwa races gani ambazo mpaka leo zipo? Na utofauti wa race ulitoka wapi kama walikuwa wapo the sama race (its impossible kusema walikuwa race moja kwa sababu eve alitoka kwenye ubavu wa Adam, its likely walikuwa the same race ).
Ilikuwa miaka gani? Na species gani? Homo sapies huyu wa sasa? Je Homo Erectus, Homo Neanderthals, na Homo ergaster hizi species ambazo zinafanana na mwanadamu lakini zina utofauti kidogo kwenye size ya fuvu, meno, na brain size zilikuwa moja ya vizazi vya Adam au ni kama wanyama wengine?
Je kwenye Biblia tunaweza kuona Stone tools zilitumika kabla ya chuma? Kama stone tools sio za wanadamu wa kale ni viumbe gani vilikuwa vina akili ya kuchonga? Na bushmens mpaka leo wanatumia mawe kuwindia. Kwenye biblia kipindi cha adam ndio hao walikuwa wanatumia mawe?
Nina haya maswali na ninagamani mwenye kujua anifahamishe zaidi maana napenda kujua hizi clues vyema.