Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Hasa mtu akisema.
Mimi nimesema kwamba stori za Cain na Abel ni za kutunga, ndio chanzo cha haya malumbano.Siamini katika CREATIONISM THEOTY, bali evolution kwa kiasi flani inanishawishi.Sasa wewe wataka nini?
 
Nilisikia walizaa mapacha wa kike na kiume kwa hiyo wakaoana kwa kubadilishana yaani mfano amuoe pacha wa abeli na ukiziangatia zamani hawakuhesabu wanawake. Mi mwenyewe sijui ila nimejibu kutokana na kusoma huhkuhuku JF.
Mbona hawa alihesabiwa? Au hakuwa mwanamke
 
Jibu ni kwamba baada Mungu Kumuumba Adam ,na kuwambia malaika wammsujudie yaani wammpe heshima,m malaika wowote walisujudu isipokuwa huyu Iblis ambayo asili yake alikuwa ni jinni.kumbuka huyu huyu Iblis au ababil au abaa sijda alilelewa mbinguni na mpk akawa kiongozi wa malaika wote.ni kiumbe anajua mambo mengi sana mbingun.Kwa kukataa huko Mungu alimpa laana na kumshusha duniani.

Adam na hawa waliishi peponi walishushwa duniani baada ya kuasi maagizo ya Mungu . Baada ya Adam na hawa Kuletwa duniani Mungu aliweka utaratibu wa wao kuzaa na walizaa kila siku ASUBUHI na jioni -elewa mwanzo wa dunia siku moja haikuwa kama ya Leo ambapo masaa yalikuwa hayakimbii saana kama maisha ya Leo.

so hapo Sheria ya kuoa ilikuwa tofauti na za miaka hii.baada ya kuja mitume na manabii KULETA taratibu za dini.na mambo kama hayo ya kuoa. So ilikuwa hivi .mtoto aliyezaliwa jioni alikuwa ANAOLEWA na MTU aliyezaliwa ASUBUHI.walitoka tumbo moja lkn utaratibu ulikuwa hivyo. Naa kwani watoto walikuwa wanakuwa haraka haraka kuliko maisha yetu.

haya.ya Leo.sasa hao akina kabil walioa ndugu zao wa tumbo moja kilichotenganisha ni Muda tu.Nasisitiza wa ASUBUHI alioa /kuolewa na wa jioni.asante
 
Rejea katika teologia utapata kujua mambo mengi na ufafanuzi mzuri kuhusu hilo na mambo mengine mengi kuhusu biblia
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Nimesoma mjadala wa hoja yako unavyoendelea, nimebaki na mshangao na kujiuliza, hivi swali ni la kidini, kisayansi au kihistoria!

Mwuliza swali "mwembemdogo" sina uhakika wewe ni mwumini wa dini na dini ipi, ila kwa kuwa umegusa maandiko ya dini, kutoka Biblia, nakujibu kwa Biblia hiyo hiyo.

Hivyo basi waumini wa dini na watetezi wa maandiko ya Biblia wanaamini hilo. Ni wazi kwamba mke wa Kaini au Abeli walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa; kitabu cha Biblia "Mwanzo 4:1-2 Adamu akamjua Hawa mkewe; akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanaume kwa BWANA. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.... Mwanzo 5:1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu akimfanya".

Kitabu cha Mwanzo 5 kinatoa orodha ya vivazi vya Adamu na Hawa - ni vizuri kusoma. Ila kabla sijajibu swali la msingi, ni vizuri kuyaeleza maandiko matakatifu ya Biblia.

1) Tunasoma Waraka 1 wa Paulo kwa Wakorintho 15:45: -Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha".

Maana yake Mungu hakuumba kundi la wanadamu bali binadamu wametokana na mwanamme na mwanamke mmoja - Adamu na Hawa.

2) Waraka wa Paulo kwa Warumi 5:12 - "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi".

Kifungu hicho kinadhihirisha wazi kwamba ni vizazi vya Adamu na Hawa TU ndivyo vinaweza kuondolewa dhambi aliyoitenda Adamu. Dhambi ya mauti, aliyopewa Adamu kwa kuasi amri ya Mungu, pia ilirithiwa na vizazi vyake.
Soma kitabu cha Biblia Mwanzo 3 hasa 17 "Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako"; Mwanzo 3:19 - kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbuni utarudi".

3) Kwa sababu Adamu aliadhibiwa dhambi hiyo kwa mauti, uzao wote wa Adamu hulipa kwa mauti. Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Waraka wa Paulo kwa Warumi 2:23". Je, jibu lake ni lipi?

4)Mtume Paulo kwenye Waraka wake 1 kwa Wakorintho 15 kwamba Mungu alimuumba Adamu mwingine kwa sura yake, Yesu mwana wa Mungu, ambaye hakuwa na dhambi yoyote, soma "1Wakorintho 15:45 - Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha".

Kwa sababu ya dhambi ya Adamu na Hawa, binadamu wamerithi adhabu walizopewa hao watu wa kwanza. Siyo kifo tu bali hata kuzaliana, soma kitabu cha Biblia cha Mwanzo 3:16 - Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto ; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala".

Tuzingatia maandiko, bila chuki yoyote binafsi, kuingiza siasa, au mawazo yoyote ya ziada ya Biblia, tukirudi mwanzo wa uumbaji, wakati kulikuwa na kizazi cha kwanza, ndugu wangeona (dada na kaka)la sivyo kusingekuwapo na vizazi zaidi. Yote haya yamesababishwa na Mtu wa kwanza, Adamu.

Watu wengi hukataa hitimisho kwamba watoto wa Adamu na Hawa walioana, kwa misingi ya sheria ya binadamu inayokataza umbu kuoana. Lakini usipoana na ndugu hutooa binadamu! Wote ni uzao wa Adamu na Hawa, wote ni wa damu moja na Hawa akiwa aneumbwa ubavuni mwa Adamu.

Sheria inayokataza ndoa kati ya ndugu wa karibu haikuwepo hadi wakati wa Nabii Musa (Mambo ya Walawi 18:20 - usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye". Maana yake awali hakukuwa na uasi wa sheria ya Mungu (Kitabu cha Nwanzo 1 na 2) kuhusu ndoa na ndugu wa karibu (hata ndugu na dada).

Lakini leo kwa sababu ya ugunduzi wa vinasaba, kuona ndugu kwa dungu kunaongeza uwezekano wa kuongezeka kwa vizazi vyenye ulemavu. Adamu na hawa waliumbwa bila chembechembe zozote zenye hitilafu. Kila alichoumba Mungu kilikuwa bora na imara (Mwanzo 1:31 - Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita".


Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?

Tatizo lenu hamuwezi kufikiria nje ya boksi,kama alimuumba mmoja atashindwaje kuumba wengi kwa pamoja wakati teknolojia ya kuumba ndio ile ile na yeye ndio mmiliki?
jibu:mungu(ALLAH) ana mipango yake na binadamu tuna mipango yetu,mfano mpango wa mwenyezi mungu(ALLAH) katika dunia ni kwamba nafsi zote zionje umauti.Lakini sisi binadamu mpango wetu ni kuishi milele na kukimbia kifo.Majibu ya maswali yote ambayo ni mnaona ni contradictions yapo katika Aya mbili zifuatazo;

Quran
85:16 Atendaye ayatakayo
13:39 Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake.
NB:majibu ya maswali magumu yanaweza kutoka katika kitabu chochote lakini MAJIBU SAHIHI ya maswali magumu ambayo ni pasua kichwa hayawezi kupatikana nje ya QURAN
 
Hiyo Qur'an yako taja aya inayoleta majibu ya hiki alicholeta mtoa kada
Usilete ujuha mwingine hapa.
Tena ukiweza kopi humu hiyo aya
Pole sana uwezo wako wa kufiri ndio umefika mwisho,swali la mtoa mada majibu yake yapo kwenye hizo aya mbili tu.Hizo aya mbili zina majibu ya maswali zaidi ya milioni mbili

Quran

85:16 Atendaye ayatakayo
13:39 Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake.
 
Hiyo Qur'an yako taja aya inayoleta majibu ya hiki alicholeta mtoa kada
Usilete ujuha mwingine hapa.
Tena ukiweza kopi humu hiyo aya
Dogo mi nakushauri ukisoma majibu yangu mara moja kama hujaelewa acha usilazimishe kuelewa utazeeka kabla ya umri
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Adam ( mean man) it represents creation of male sex and ( mother of all) wakimanisha kila mtu ata zaliwa na mwanamke basi.

Kwahiyo kuzaliwa kwa Cain na Abel waliwakilisha watu wengine walizaliwa kwa mara ya kwanza kwa watu walioumbwa kwa mara kwanza. Ninacho manisha Mungu kwa mara ya kwanza alimuumba Adam (mwanaume) uhalisia adam anawakilisha jinsia/jinsi ya kiume. Pia EVE ni the same scenario waliumbwa wanawake na Eva anawakilisha wanawake walio umbwa kwa mara ya kwanza.
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?

KWANZA NINI KINAKUSUMA KUULIZA MASWALI KAMA HILI ? UNAFAIDIKA NINI UKIPATA JIBU SAHIHI KAMA SIYO UNATAKA KUHALALISHA KUOANA NA NDUGU AU KUFANYA TENDO LA NDOA NA NDUGU WA DAMU WAKATI MUNGU AMEPIGA MARUFUKU KUONEKANA KWA LAANA YA KUFANYANA TENDO LA NDOA NDUGU !

SOMA BIBLIA KATIKA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI 18:1-19

1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao.
4 Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
5 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA.
6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA.
7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.
10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.
11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake.
12 Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu.
13 Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.
14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako.
15 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.
16 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.
17 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.
18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.
19 Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake.
20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.
 
Kaini alioa dada yake na kujitenga na familia ya Adam kwenda nodi(nchi ya kutangatanga). kumbuka kipindi hicho mwanamke alikuwa hahesabiki na ukiona ametajwa alikuwa kwa tukio maalumu. Mchungaji au padri aliyesoma theology/divinity hawezi shindwa kukuelezea vyema. Tafuta kitabu cha wazee na manabii cha wasabato. Kumbuka kitabu cha mwanzo kimebeba matukio ya zaidi ya milenia moja hivyo yote hayakuandikwa na Musa kwa kitabu hicho. Pia pitia na quran japo nayo imepesti toka kwenye biblia na mgogoro wa Kaini na Abeli uko tofauti kwa vitabu vyote viwili (yaani biblia na quran).
 
Kaini alioa dada yake na kujitenga na familia ya Adam kwenda nodi(nchi ya kutangatanga). kumbuka kipindi hicho mwanamke alikuwa hahesabiki na ukiona ametajwa alikuwa kwa tukio maalumu. Mchungaji au padri aliyesoma theology/divinity hawezi shindwa kukuelezea vyema. Tafuta kitabu cha wazee na manabii cha wasabato. Kumbuka kitabu cha mwanzo kimebeba matukio ya zaidi ya milenia moja hivyo yote hayakuandikwa na Musa kwa kitabu hicho. Pia pitia na quran japo nayo imepesti toka kwenye biblia na mgogoro wa Kaini na Abeli uko tofauti kwa vitabu vyote viwili (yaani biblia na quran).

It seems like you can answer our question vyema kwa sababu unaelewa mkuu.

How about Races and their religions kwa Kaini na Abeli?
 
Mwanzo 6
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Vv
Hao wana wa Mungu bila shaka ni kaka zake Yesu[emoji12]
 
kwa kuwa Mungu ni master scientist, inawezekana uzao wa kwanza kabisa aliujalia genetics za tofauti ili kusiwepo na effect ya back crossing, hata kaka na dada wa tumbo moja wangeweza kuzaliana pasipo changamoto yoyote. Kwa upande wa pili mambo haya ni IMANI so ondoa LOGIC [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom