Shushani Ngomeni
Member
- Nov 24, 2014
- 45
- 18
hatujui kiarabu cha dini ya AlahSomeni Quran mtapata majibu ya maswali yenu
Bado hujajibu swali.tufanye walioa na miaka mia nane sasa kijiji kilitokana na kinanani?itakuwa walioana kaka na Dada maana hakukua na shangazi wala mjomba ni baba mama na watoto tu na hapo kwenye miaka zamani hawakuhesabu kama leo ilivyo siku zilikuwa chache tu na dunia ilikuwa ni sehemu wanazojua wao tu.
Bado hujajibu swali.tufanye walioa na miaka mia nane sasa kijiji kilitokana na kinanani?itakuwa walioana kaka na Dada maana hakukua na shangazi wala mjomba ni baba mama na watoto tu na hapo kwenye miaka zamani hawakuhesabu kama leo ilivyo siku zilikuwa chache tu na dunia ilikuwa ni sehemu wanazojua wao tu.
Huo ndio ukweli wa mambo.Nilikwishaeleza humu kitu muhimu katika vitabu vya Agano la Kale na Jipya ni Maudhui.Wapo wahusika wengine hasa katika Agano la Kale wengi ni majina ya kutungwa (kama tunavyofanya leo katika Fasihi Andishi na Simulizi) ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa.Aghalabu Agano Jipya wahusika wengi ni watu halisi.Katika Agano la Kale,vitabu vingine ni hadithi.Swali jepesi sana.iko hivi
Adam na hawa hawakuwa watu halisi kama tulivyo mimi na wewe bali yalikuwa ni majina ambayo yalitumika kuwakilisha makundi ya watu.so Adam alikuwa anawakilisha wanaume na hawa alikuwa anawakilisha wanawake.lengo la kitabu cha mwanzo ni kuonyesha historia ya binadamu so isingewezekana kuzungumziwa namna kila mtu alivyopatikana so yakachaguliwa majina mawili ili yawe vielelezo au kuwakilisha makundi hayo ya watu.ukisoma vizuri kitabu chenyewe kinajieleza mfano habari ya nyoka kuongea unaona kabisa kwamba No kitu ambacho hakileti maana.so mwandishi wa kitabu kile alitumia majina ya adamu na hawa kwa maana hizo.mfano mzuri ni hadithi za sungura na fisi ambazo hutumia majina hayo kuwakilisha watu halisi.
Biblia inazungumzia ukomboz wa mwanadamu ambao story inaanzia kwa adam na hawaBinadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
ukinipa source nyingine manake biblia haina hizi info zaidi ya story ya adam na hawa ambayo haileti maana. unakubali kwamba biblia haijitoshelezi?
Waliwaowa dada zao.
kwa kuwa Mungu ni master scientist, inawezekana uzao wa kwanza kabisa aliujalia genetics za tofauti ili kusiwepo na effect ya back crossing, hata kaka na dada wa tumbo moja wangeweza kuzaliana pasipo changamoto yoyote. Kwa upande wa pili mambo haya ni IMANI so ondoa LOGIC [emoji23][emoji23][emoji23]
Naona wengi tunasoma Biblia kwa mistari michache na kufanya conclusions ambazo hazitusaidii kujibu maswali muhimu. Kwanza tuelewe stori ya Adam na Hawa imewekwa kwa kusudio la kumwelewesha mwanadamu na mahusiano yake na Mungu, na mtiririko wa maisha ya binadamu toka wakati huo hadi sasa. Adam na Hawa walikuwa wanadamu pekee ambao waliishi bustani ya Eden ikimaanisha kuwa wanadamu wengineo waliishi sehemu nyingine mbali mbali.
Ukisoma Mwanzo 1:26-29 wanadamu waliumbwa wengi tu na walikuwepo kila kona ya dunia kabla ya Adam na Hawa.
Adam alimzaa Kaini na Abili, Adam akaishi miaka mia tisa thelathini 930 ndipo akafa, katikati hapo aliwazaa watotot wengi ambao walisambaa kote duniani na hivyo ikawa raisi kumpata mtu wa kuoa, story hii iko vizuri katika kitabu cha mwanzo 5. karibu jisomee dont argue without facts.
Kwa kiasi fulani umetaka kuongelea ukweli ambao upo na watu hawauzingatii kabisa.Mungu hakuumba mtu mzima kama tunavyojiona leo. Alianza na Sperm na Ovum.Kwa hiyo kunapozungumzwa uumbaji wa watu wa kwanza kunamaanisha Mungu kutengeneza structures za Sperm na Ovum.Baadaye ndio zikakutanishwa. Alizikutanishia katika Oviduct na Uterus ya namna gani hakuna ajuaye.Ukweli huu ukitaka kuuona jaribu kuangalia viumbe vyote vya Ulimwengu.Vyote ni Auto(Vinajiendesha).Kwa hiyo kama unavyoona dunia kwa mfano baada ya kuumbwa pengine alii-start ili ianze rotation na baada ya hapo inaendelea yenyewe.Hali kadhalika Binadamu.Baada ya sperm na Ovum kuungana kila kitu baada ya hapo kikawa Auto (kinajiendesha).
Na kwa hiyo tunapozungumza juu ya kuumbwa kwa mwanadamu tunaongelea juu ya genetic programming(coding) aliyoifanya Mungu kwenye hizo single cells za Sperm na Ovum.Gene ndio code zenyewe.Gene kwa watu wa Electronics unaweza kulinganisha na Micro-Controller katika Computer au simu au kifaa chochote cha Electronics.Gene ndio imebeba uhai(information).
Waktisto wanadai biblia iliandikwa kwa muongozo wa roho mtakatifu ambayo pia ni matakwa ya Mungu sasa huyu Mungu anaubaguzi? Kwahiyo aliona hakuna umuhimu wa kuwaregard wanawake? Kama ni ivo anamapungufuZamani na hata katika Biblia wanawake walikua hawahesabiwi hivyo Adam na Hawa walikua na watoto wakike na hawakuandikwa na basi waliolewa na Abel na Kain
Mkuu Apollo kila kitu umeshaweka bayana hapo kwenye mstari wa 27, "male and female he created them" ona kuwa imewekwa kwa wingi (plural) kuonyesha kuwa walikuwa wengi. Sura ya kwanza inazungumzia siku sita za kwanza katika uumbaji, wakati sura ya pili inazungumzia zaidi kuumbwa na kuwekwa kwa mwanadamu ndani ya bustani ya Eden.
Hakuna mahali popote palipoandikwa kwenye Biblia inaposema kuwa Adam ni binadamu wa kwanza duniani. Watu mbali mbali waliotajwa kwenye Biblia ni kwa ajili ya kutujuza sisi mahusiano yetu na Mungu na kutufundisha yaliyotokea kabla yetu.
Nani kasema wanawake walikuwa hawaesabiwi?Zamani wanawake walikuwa hawahesabiwi, pia ndugu walioana. Hivyo waliwaoa ndugu zao wa kike na uzao ukaendelea.
Unapozungumza mambo ya hypothesis kwenye Biblia unaenda nje kidogo na matumizi yake. Biblia ni neno la Mungu lililolengwa kuwapa wanadamu busara,mwongozo,amri na ushauri kuhusu maisha yao ya duniani na baada ya dunia. Biblia imeandikwa kwa lugha ya mafumbo na sio rahisi kuelewa maana ya hayo mafumbo. Ili kuelewa inabidi uwe na upako (Roho Mtakatifu). Wasomi wa Biblia wako wa aina mbili, ukiitizama Biblia kama mtu aliyevishwa kanzu wasomi wa Biblia aina ya kwanza wanaangalia zaidi muonekano wa kanzu na kutafsiri juu juu maana ya Neno, kundi la pili la wasomi wa Biblia ni wale wanaojaribu kutambua na kujaribu kuelewa kilicho ndani ya kanzu hivyo kuelewa maana halisi ya Neno.
Sasa kipindi cha Kaini na Abel ndugu walipatikana wapi???? Tusaidie kiongoziZaman watu walikuwa wanaowana ndugu kwa ndugu