Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Swali jepesi sana.iko hivi
Adam na hawa hawakuwa watu halisi kama tulivyo mimi na wewe bali yalikuwa ni majina ambayo yalitumika kuwakilisha makundi ya watu.so Adam alikuwa anawakilisha wanaume na hawa alikuwa anawakilisha wanawake.lengo la kitabu cha mwanzo ni kuonyesha historia ya binadamu so isingewezekana kuzungumziwa namna kila mtu alivyopatikana so yakachaguliwa majina mawili ili yawe vielelezo au kuwakilisha makundi hayo ya watu.ukisoma vizuri kitabu chenyewe kinajieleza mfano habari ya nyoka kuongea unaona kabisa kwamba No kitu ambacho hakileti maana.so mwandishi wa kitabu kile alitumia majina ya adamu na hawa kwa maana hizo.mfano mzuri ni hadithi za sungura na fisi ambazo hutumia majina hayo kuwakilisha watu halisi.
Unatupoteza mkuu...
 
Zamani na hata katika Biblia wanawake walikua hawahesabiwi hivyo Adam na Hawa walikua na watoto wakike na hawakuandikwa na basi waliolewa na Abel na Kain
Sidhani kama tatizo letu ni kuhesabiwa; tatizo letu mkuu ni kujua hao wake waliowapata walikuwa wapi. Labda useme sasa kuwa Zamani wanawake walikuwa hawatajwi majina yao ; ambapo ntakuuliza kuhusiana na Hawa mbna ametajwa
 
Zamani wanawake walikuwa hawahesabiwi, pia ndugu walioana. Hivyo waliwaoa ndugu zao wa kike na uzao ukaendelea.
Tatizo sio kuhesabiwa ...Tatizo ni walitoka wapi. Sidhanj kama biblia ilishindwa kuandika kulikuwa na ndugu zao kama kweli walikuwepo mana kama kulikuwa na ubaguzi kiasi hicho basi hata tusingesikia Jina la Hawa kabisa...
 
Ukiachana na stori ya Adam na Hawa pia kulikuwa na stori ya watu wengine ambao hawakutajwa majina. Rejea Kaini alivyomuua Abel Mungu alimtia alama asije mtu yeyote akamuua kwa hiyo ni wazi kulikuwa na watu wengine
Nadhani tatizo ni mwandishi...ameipoteza hadhira .
 
Sio kweli kuwa mungu aliumba watu wawili aliumba watu wengi ila walichukuliwa kama sample soma kitabu cha mwanzo chote utaelewa
 
Ndio ubaya wa story za kutunga....mara nyingi zinaishia hewani pasipo na majibu ya maswali yatakayo ibuka....kama Mungu ndiye aliyeumba watu basi angeumba wanawake na wanaume wakutosha ili wasizalishane ndugu kwa ndugu.....na kama aliruhusu ndugu kuzaliana, kwa nini akataze sasa hivi???
Ndo maana kuna torat injili zabur na quran sababu ya nyakati
 
Aliewaumba ndo alieruhusu ndugu wa damu pia waoane. Kuna uwezekano watoto wa Adam walioana wenyewe. Hiyo mila iliendelea hata waebrania walikuwa wanaoana ndugu. Mfano Ibrahim alimwoa sara mdogo wake, baba moja ila mama tofauti. Hivo ni watoto wa mzee Tera walioana. Ndo maana kila anakofika ibrahimu alimtambulisha mkewe ni dadake. Ndugu kuoana kwa waebrania si jambo geni sana ingawa baadae walipunguza mila hizo
 
Ndo maana kuna torat injili zabur na quran sababu ya nyakati
Torat imejaa ukatili wa kutisha,...zaburi inachochea vita....injili imeandikwa kwa utu na kwa kuhimiza upendo.

Ukiangalia Biblia utu, kujali haki za binadamu na upendo kwa watu unaongezeka kutoka vitabu vya mwanzoni kuja vitabu vya mwishoni.

Hapo utagundua kwamba watu walistaharabika kulingana na nyakati, kutoka zamani hadi sasa....waliporekodi historia zao kwenye Bibilia, bibilia iliakisi maisha ya watu.
 
mchina muafrika mzungu mwarabu mjapani walikuaje na asili tofauti na adam na hawa? na kama asili ya mwanadamu ni pale eden, wamarekani wabrazil waargentina wametokea wapi? sababu wapo bara tofauti na bara waliloumbiwa adam na hawa.
Refer the theory of continental drift
 
Mwanzo 5:4 Adamu anazaa wanaume na wanawake,hapo ndipo walipoanza kuzaa.nimelipata baada ya kuisoma biblia....nikapata kasehemu hako....endelea mwenyewe
 
Tatizo sio kuhesabiwa ...Tatizo ni walitoka wapi. Sidhanj kama biblia ilishindwa kuandika kulikuwa na ndugu zao kama kweli walikuwepo mana kama kulikuwa na ubaguzi kiasi hicho basi hata tusingesikia Jina la Hawa kabisa...

Mkuu kama vitu vyote vingeandikwa katika biblia hakika biblia isingetosha. Maana mambo ni mengi sana yaliyofanyika enzi hizo tangu Adamu mpka Yesu.
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?


Hakuna swali gumu hapo, mtoto wa kike na wa kiume anayeendeleza ukoo ni mtoto wa kiume, katika biblia Watoto waliotaji ni wa kiume aimaanishi kuwa adama na hawa walikuwa na watoto wa kiume tu, Watoto wa kike alikuwa nao. Ili ukoo kuendelea unaitaji mtoto wa kiume ndiyo waliopewa nafasi kuelezewa vizuri wanawake walio waoa, fuatilia kuhusu uzao wa yesu kutoka Ibrahim mpaka yoseph watu wote waliotajawa ni wa kiume tu, Je Watoto wa kike hawakuzaliwa , yakobo, yusuph walikuwa na watoto wengi sana chunguza vizuri kuhusu Watoto walio elezewa katika maisha yao utagundua Watoto wa kiume tu.
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Walizaa pia Seth baada ya Abeli kufa (sidhani kama alikua ameoa y Abeli). Kaini akalaaniwa kwa kumuua Abeli akawekwa alama kwenye paji ili 'watu wa mataifa' watakapomuona wamjue.

So Mungu long kabla ya kumuumba adam kulikua na watu wa Mataifa.

Vyovyote vile hiyo hadithi si uhalisia. Ilibidi kuitunga ili kuleta mwafaka wa biblia kuhusu mwanza wa mtu.
 
Back
Top Bottom