TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

Wengi tunaishia kumtakia kheri kwa mola, hatuuchambua wimbo wake. Au hauna maana?
 
Ntamaholo nakuunga mkono;

Threda ya rambi rambi ipo hapo juu...............hapa tujadili kazi yake kama msanii!

Nimeupiga mara 6 huu wimbo nikijaribu kutafakari kazi hii

Fumbo kubwa ni mambo mengi yaliyo kinyume ambayo jamii yetu hivi sasa imeyakumbatia

Mfano..........Nyoka mwenye hereni............ni jinsi jamii inavyoabudu wenye pesa na hali ni watu wanayoiumiza jamii kwa kiu yao ya kujilimbikzia mali
Ngombe jike karembua...........nawafananisha na masoga na wwasagaji .............nk

Kiujumla ametanabahisha mambo yote yaliyo kinyume lakini jamii inayafumbia macho hasa yale maovu......mfano anapowaambia wasambaa na neno she..........anawalenga watu wote kuwa tumemkaribisha shetani na kumgeuza rafiki yetu..................

Mr Ebbo naweza kuthubutu kumwita ni genious in his own way! Tutamkumbuka
 
Hakika tumempoteza mwanamuziki anayejali asili ya Tanzania hususan jamii ya Wamasai.

R. I. P Mr. Ebo
 
Mr Ebbp (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda kidogo huko mkoani Tanga alikokuwa anaishi. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea jijini Arusha kwa mazishi inafanywa. Katika uhai wake alitamba na nyimbo kama Mimi mmasai, Kamongo, Boda Boda na nyingine nyingi.
 
polen sana ndg zangu huko mliko najua hali ni ngumu pia wakati mgumu sana hata sisi wananchi wa tunduma mana hali ni ngumu tokea soko liungue.R.I.p mr ebo upumzike kwa amani kazi yake mola haina makosa
 
Back
Top Bottom