Mr Ebbp (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda kidogo huko mkoani Tanga alikokuwa anaishi. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea jijini Arusha kwa mazishi inafanywa. Katika uhai wake alitamba na nyimbo kama Mimi mmasai, Kamongo, Boda Boda na nyingine nyingi.