TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

Nakumbuka mara ya mwisho nilimuona Kinondoni mkwajuni akielekea Kinondoni Hananasif akiwa ndani ya Harrier yake. Kutokana na kuwa na foleni alishuka ndani ya gari kusaidia kulekeza magari ili kupunguza foleni( kama kawaida akiwa na mavazi yake ya Kimasai). Oooh Mr. Ebbo tutakumbuka kwa nyimbo zako zinazotukuza Utanzania.

Mwanga wa Milele umuangazie ee bwana, apumzike kwa amani Mr. Ebbo. Amen
 
mara ya mwisho kukuona ilikuwa masai camp arusha kipindi hicho unaimba r&b na uliitwa mr.ebbo.RIP
 
Duh, Mungu akupe rehema yake, mateso yako na kuugua kwako yote yamekwisha Abel, twakumbuka sana!!

 
Last edited by a moderator:
sio kwamba sina uhakika, huyu jamaa kafia Arusha maeneo ya Usa, hapa nilipo naishi karibu kabisa na shangazi ake, maeneo ya kimandolu, na chalii aliekuwa ana muuguza ni chalii etu, ambae ni binamu yake. Kwaio nna uhakika na hii habari.

Hatukatai kuwa hafafa. Tatizo ni kuwa kwa celebrity kifo chake kinagusa wengi. Ni sharti taarifa ziiwe na hitimisho. Amefariki lini akiwa na umri gani, sababu za kifo chake(inamiss) na mchango wake kwa jamiii. Mungu awatie nguvu wafiwa wote na washabiki wake.
 
Siku unafiwa na mtu wako wa karibu utauliza source?




Wanakeraga hao kila kitu utawaona "Source plz???"
Ngoja iko siku utamwambia kimbia hapo kuna chatu na atakuuliza "source plz", akishapigwa na chatu ndio atajua ilikuwa source
 
RIP Mr. Ebbo! daima utakumbukwa kwa nyimbo zako zenye mafunzo mengi.


Mr. Ebbo alikuwa kimnya kwa muda mrefu ni kutokana na kusumbuliwa kwa kansa ya damu pamoja na BP ya kushuka ambapo alikuwa kipatiwa matibabu KCMC Hospital ingawa alikuwa akiendelea vizuri ila kilicho muuwa ni BP ya kushuka sana.

Source Kaka wa Marehemu ndani ya familia ya Motika!
 
Hii tabia kwa redio zetu za hapa nchini imekuwa ni sugu pale msanii anapofariki dunia ndipo nyimbo zake zinapigwa kwa wingi sidhani kama ni tabia ni nzuri kwani huongeza hudhuni kwa wafiwa na watu wake wa karibu.mimi binafsi tangu jana nilipokuwa nikisikiliza nyimbo zake kwenye radio huwa natamani kutokwa na machozi kutokana na uzandiki wa watangazaji wetu hawa na mapenzi yangu juu ya Mr.Ebbo.Kwani hata kama mkizipiga nyimbo zake kwa wingi na kuzifanya kuwa hit kwa mara ya pili hakuna faida yoyote kwa kuwa hawezi tena kupiga show kwa hits hizo mlizozitengeneza na watangazaji hawa wanashindwa kutambua kuwa kadri wanavyopiga nyimbo zake ndipo yeye(mr.ebbo) anazidi kupata mateso huko alipo(kwa imani yetu ya kidini).R.I.P MR.EBBO WE WILL ALWAYZ REMEMBER YOU
 
kadri wanavyopiga mziki wake ndivyo anavyozidi kupata mateso duuu hii kali..lakini hii ni kwaimani ya dini ipi maana kama ni mateso basi akina bob, 2pac watakuwa walishakuwa zaidi ya mara 100..
 
Hatukatai kuwa hafafa...Amefariki lini akiwa na umri gani, sababu za kifo chake(inamiss) na mchango wake kwa jamiii
M'bongo hatakiwi kuuliza hayo maswali yako ya marehemu kafa na nini. Mwafrika yuko kwenye edge of existence, saa yoyote anaweza kuanguka, akifa ni kama kawa, hakuna kuulizana sijui alifanya nini na maisha yake. Itoshe kusema Inna li Llahi wa Inna iLlahi Rajiun!

Habari ya sijui amekufa na kansa ya figo, kuulizana eti ule utafiti wetu wa saratani umefikia wapi, hakuna hayo ma complication ya magharibi, ya nini? Mungu ameumba, Mungu ameua. Kwisha. Marijani Rajab aliimba "kula ugali wako ukalale...hakuna rufaa ya kifo."

Abel Loshilaa Motika nitamkumbuka kwa kuenzi utamaduni wangu bila kujali kuwa "mshamba." Alituma ujumbe wa nguvu kwamba "naruhusu kushangaa kwa wageni na wenyeji." Kama ni ushamba kuchukia club soda kwa sababu ni kali basi ni poa tu, nitaongeza sukari vile vile. Na hakusita kusema hajui Kiingereza. Nini Kiingereza, Kiswahili chenyewe hajui, na sio hatari vile vile.

Kama we iko na kosa nakuwa ya Jinai. Jinai mutu ya wapi kila kosa hakatai? Nasingiziwa sana, au ni rushwa hatoi?
Na hapa Saridalama ni wapi naitwa Bise? Ukitafuta mutu naambiwa yuko Bise, huko Bise ni wapi, mbona mimi bado fika?

Ahsante Mr. Ebbo kwa kazi ya maisha yako.
 
Back
Top Bottom