TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

What? Siku yangu imeharibika. Mr. Ebbo alikuwa anaimba nyimbo zenye mafundisho hutachoka kumsikiliza. Poleni sana mliofikwa na msiba huu Mungu azidi kuwatia nguvu tupo pamoja. Tutakukumbuka daima. Umpumzike kwa amani.
 
Rest in peace bro. We umetangulia na sisi tutafata siku moja
 


Ndugu wenzangu usiku wa jana, kuna ujumbe wa kusikitisha sana ya kwamba Abel Motika a.k.a Mr. Ebbo ambae ni msanii na pia ni producer wa muziki katika studio yake ya Motika Records mjini Tanga ameaga duniani,taarifa zilizopatikana kwa jirani yake wa Mr.Ebbo amesema kuwa alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa hospitali ya Mount Meru na usiku ndipo alifunga ukrasa wake wa maisha na safari yake ya kuishia ndio ulifika mwishoni mwa jana saa 5 usiku.
 
he we si ulikuwa unaulizia source
kwa maana ya kwamba hujui
kama kafariki imekuwaje tena umegeuka doctor?

acha unyanyapaa
kwani ukimwi si jambo la kumcheka
au kumnyooshea mwenzio
vidole wkt afya yako wewe na doc wako ndo mwaijua


rip abel loshilaa motika
uwe umekufa kwa ajali
maradhi
ama lolote
we are behind you
Mkuu umekosea!!!angalia vizuri post,aliyekuwa anadai source na kuzusha kwamba kafariki kwa UKIMWI ni mwingine!!!!!Just make careful follow up rather than making skimming/scanning reading:spy:
 
Nini kimemtanguliza mwenzetu. Its so ghafla eee!
 
Mungu amlaze mahali panapostahili..
 
Mr. Ebbo hatunaye tena duniani! Ni masikitiko makubwa sana kumpoteza mwanaharakati wa muziki kama Mr Ebbo. MuzikI wake ulivutia, kufundisha, kuonya, kudumisha mila na utamaduni. Ni mwakilishi wa wamasai kwenye uwanja wa muziki lakini pia hata Tanzania nzima hasa pale tunapozungumzia muziki nje ya mipaka ya Tanzania. Mr. Ebbo namkumbuka sana kwa ujasiri wake wa kuenzi mila na desturi za kabila lake. Ni wasanii wachache wanaoweza na kuthubutu kudumisha mila na desturi za kabila wanazotoka. Tunashuhudia wasanii wengi wakifanya sanaa ndani ya DSM na kujiinua kuwa wao ndio watoto wa jiji. Huwezi kuwaona wasanii hasa wa muziki wakitukuza na kujivunia desturi za kwao. Hii nadhani ibaki kama kumbukumbu kwa wasanii wote wa muziki Tanzania na hata wale wa sanaa nyingine kuwa na "homage arts".
Ikumbukwe kuwa Mungu alivyotuumba muda wetu wa kuishi duniani hatuna dhamana nao; dhamana hii ipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu aliyetuumba. Hivyo hatuna budi kuwa makini na wakati, na kufanya kila kitu na mipango yetu kana kwamba tunakufa kesho. Mr. Ebbo alikuwa sana serious na kazi zake bila haya usiku na mchana.
Mr. Ebbo hatunaye tena, basi tubaki na yale yote mema aliyoyatenda angali hai kwa manufaa yetu na kwa wale watakaobaki baada ya maisha yetu kukoma duniani kama ilivyompata Mr. Ebbo.
Natoa pole sana kwa familia ya mzee Motika, ndugu jamaa na marafiki wa mbali na wa karibu wa familia ya mzee Motika; pia kwa wapenzi wote wa kazi za marehemu Mr. Ebbo. Mwenyezi Mungu atujalie wote mioyo ya subira, uvumilivu na faraja kwa wakati huu wa majonzi mazito sana. Mungu atusaidie sana kuzienzi kazi zote nzuri alizoziacha mwenzetu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE! AMEN!
 
Kwa taarifa ya redio Clouds....... Mimi Mmasai bana....hatunaye tena.
 
Mkuu umekosea!!!angalia vizuri post,aliyekuwa anadai source na kuzusha kwamba kafariki kwa UKIMWI ni mwingine!!!!!Just make careful follow up rather than making skimming/scanning reading:spy:

Nimeipenda hyo skimming and scanning
 
Back
Top Bottom