Sina mashaka hata kidogo na kazi pamoja na kipaji chako na mtindo wako ulioamua kutoka nao miaka hiyo ladha iliyowaburudisha nayo Watanzania wa rika, jinsi na umri mbali mbali, ulifahamika katika ulimwengu wa wasanii kwa jitihada na uwezo wako. Hakika ulikofikia kwa wakati ule si pabaya.
Uliugua kama Binadamu mwingine yeyote na sasa Mungu kaamua kukuita Ulale salama ndugu yetu; inauma sana kupoteza nguvu kazi na mwalimu wa Watanzania wenye kupenda kuwa Wasanii kama wewe ila hatukuwa na jinsi manake aliyekuumba ndiye mwenye mamlaka na pumzi yako yeye akishasema hakuna wa kupinga wala wa kukata rufaa umetangulia nasi twaja kwa kupitia njia hiyo hiyo Watanzania tutakukumbuka daima.
rest in peace brother..............