TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

Hata ukimwi ni ugonjwa jamani, wameletewa wanadamu cha muhimu hawa wanaojiita mastaa ni kuwa makini vinginevyo wataenda sana, maskini ebbo uhandsome wote kwishnee
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ovyo kabisa, hakuna hata aliyewahi kuandika "Mr.Ebbo yu mgonjwa" Huwezi kujua wengine tungepata taarifa mapema, tungejitolea kwa hali na mali kumsaidia mgonjwa...pengine angekuwa bado hai...pengine alikufa kwa kukosa huduma nzuri zaidi..pesa ya matibabu etc.
 
Kweli . Zaidi ya wito huo. Ukigundua umeambukizwa usikimbilie kuokoka maana hutapona kimwili. Ukiamua kuokoka poa tu ila wokovu bila ARV hausadii cho chote zaidi ya kuondoka mapema. Bahati mbaya wachungaji wengine wa kondoo huwadanganya victims wao hata wasitumie dawa za ARV. Na walaaniwe kama wale wanoambukiza ukimwi makusidi. R.I.P Me Ebbo.

The main objective ya kuokoka sio kupona ugonjwa ila ni kukubali msamaha wa dhambi na kuacha njia zetu mbaya kwa kumfuata YESU ambaye hashindwi na jambo lolote.
Ila elewa tu kwamba, MUNGU anaponya ukimwi na ugonjwa mwingine wowote ule unaoweza kuufikiria. Ila sio vizuri kwa watumishi wa MUNGU kuwaachisha watu ARV na dawa nyinginezo bila hiari yao, hii ni sawa na kumlazimisha mtu aamini na wakati imani inatoka moyoni mwa mtu.
Wapo watu waliopona ukimwi kabisa kwa maombi.
 
dah jamani jamani!!nani atabakiiii?mbeya ndo wenye vvu wamefikia 16% nani atabaki

mimi narudi zangu nyumbani mapema...najisomea na kujilinda..mwenzangu huko nje kazidiwa kishawishi au kaamini kondom ikapasuka...ndo basi tena..akija nyumbani baba nakula rojo....!!tayari nshaingia!!

tusimlaumu Ebbo...Mungu ampumzishe

nawaasa wale mlioshaambukizwa....muwahi kuanza dozi mapema...at least utakufa kifo cha kuugua japo kidogo!!

Ebbo umeumwa sanaaaa...u didint deserv the pains.....ARV was there to shorten some of the pains..oooh poor
 
Kweli . Zaidi ya wito huo. Ukigundua umeambukizwa usikimbilie kuokoka maana hutapona kimwili. Ukiamua kuokoka poa tu ila wokovu bila ARV hausadii cho chote zaidi ya kuondoka mapema. Bahati mbaya wachungaji wengine wa kondoo huwadanganya victims wao hata wasitumie dawa za ARV. Na walaaniwe kama wale wanoambukiza ukimwi makusidi. R.I.P Me Ebbo.
ARV ni kama virutubisho au vitamini mwilini, hivyo havina madhara yoyote, ni mchungaji yupi alizuia watu wasitumie hizo ARV, uwe mkweli? Wachungaji ni waelewa vile vile usiwafanye mbumbumbu!!!!!
 
ebbo.jpg

Mr. Ebbo. mia
 
aisee, yani nimekua mdogo kuliko piriton,

yani the guy alivyokua handsome, huwezi amini ugonjwa ule ulivyo mbaya!!!

aisee
 
ndo hivyo na sisi tupo nyuma 100
all we have to do is
kujiweka tayari manake hatujui siku wala
saa!!!1 mda wowote twaweza ondoka

asante kwa picha. dah! ni kweli ametutoka KINEGA WETU. Mungu amuweke mahali pema peponi amina. Mia
 
Asante kwa picha dada, machozi yamenitoka.... jamani kifo kibaya hiki

ulie usilie,upend usipend one day we wil die hiyo ni ahadi na kumbuka kifo kizuri ni cha YESU pekee coz alikufa na thrd day akafufuka
 
dah picha imenitisha sana,maskini mr ebbo.atakua aliugua haswa.nikisoma ktk habari mbalimbali sababu ya ugonjwa wake inachanganywa,mara kansa ya damu mara maradhi ya mapafu haieleweki.mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
 
rip mr Ebbo,hata mie hio picha imenitisha.......
 
Upumzike kwa amani Mr. Ebbo
 
ubinaadam kazi...kuna haja ya kumsimanga marehemu!!!
 
ubinaadam kazi...kuna haja ya kumsimanga marehemu!!!
Nakubaliana na wewe. Kuna kila sababu kwa marehemu kwa kufuata sheria za dini ya kiislamu kusitiriwa na walio hai. Si amini Kama angekubali picha ninayoiona au namna alivyo ionekane/aonekane.
 
Nakubaliana na wewe. Kuna kila sababu kwa marehemu kwa kufuata sheria za dini ya kiislamu kusitiriwa na walio hai. Si amini Kama angekubali picha ninayoiona au namna alivyo ionekane/aonekane.
umenena mkuu, hata mm nilifikiri kitu kama hichi..sidhani kama angependa aonyeshwe katika hali ile...ndio maana waislamu wanasema maiti anaona aibu!
 
Back
Top Bottom