TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

RIP Mr. Ebo,

You will always be missed given the great work you have done, artist like him are very important in any community, it is unfortunate that they dont earn what they deserve and never even taken care of. If the Wabungez and Mawaziris are taken to India for only Body check, perhaps he wouldn't have died if was offered such a chance.

Anyway, Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe.
 
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani Amina.
Very shocked!! Huyu jamaa kwa wanaofahamu ndio wasanii wa mwanzo kabisa kuimba R&B tena kwa kiingereza kabla baadae sana kubadilika na kuimba kwa lafudhi ya kimasai! Kwa tuliokuwa Arusha miaka mwanzoni mwa 90s watakuwa wanamkumbuka vizuri sana hasa Deo Rweyunga wa radio one! Miaka hiyo wakati bado anaimba alitoa nyimbo akishirikiana na wakenya(wale walioimba Mpenzi hakuna matata kwa wanaokumbuka) ikatamba sana United radio service (URS) ya arusha moja ya radio za mwanzo za Fm Tz! Naweza kumuweka ktk kundi la Ma legendary wa bongo fleva ingawa watanzania wengi mlimfahamu kuanzia mimmasai bwana! Dah Rest in peace bro!
 
Duh! What a bad news!
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, ampumzike kwa amani. Amen!

"Nikitu najivunia, Masai fahari yangu!"
 
Mungu amuweke mahali pema peponi... Wimbo wa Kamongo umenikaa kichwani baada ya taarifa za msiba wake... Motika Rekodiz... Sisi tunatoa RUBUDANI...
 
Poleni sana wafiwa katika wakati huu mgumu wa kilio cha kumpoteza mpendwa wenu, haijalishi kafariki kwa ugonjwa gani malaria, mafua, kisukari au ukimwi, ajali ya ndege, gari, basi au bajaji. La muhimu ni kukumbuka ni kushikamana na Mungu sana kwakuwa hii ni safari ya wote kwasababu lazima kila mtu airudie ardhi ni wakati gani sio wewe au mimi najua, ni siku gani si wewe au mimi najua, kikubwa tuombeane.
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii aliyejizolea mashabiki wengi hapa nchini kwa staili ya muziki wake aliokuwa akifanya, Mr Ebbo ameaga dunia leo. Mr Ebbo alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani jijini Arusha. Mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wote wa muziki hapa nchini. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
 
This is my favorite Mr. Ebo song Tanzania - Swahili Bongo Flava - Masai Rap (Kamongo) - YouTube, This Video Done by Chapakazi Filmz. I will Miss you my brother Mr. Ebo, I remember the day you invite us on UBARIKIO wa mwanao pale home kwako Tanga, tukala Mbusi kwa visu bila Chumvi, Pia nakumbuka wakati unakuja studio Chapakazi kufuatilia hii video yako tunakaa tunaangalia movie huku tukipiga moja moja.
 
Mwanamuziki nguli wa bongo falaver ametutoka hapa Arusha
inasadikiwa alikua anaumwa kwa muda mrefu na alichoka dawa za
hospitali na kuamua kutumia miti samba

Mungu ampumzishe kwa amaini amina.


Ebboweb.jpg
 
Back
Top Bottom