TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

381334_323773357633297_100000019058462_1321065_1933741141_n.jpg
Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi. R.I.P. Mr Ebbo!
mmmh! ni kweli huyu ni mr.ebo???? ooh! jamani jamani! nimeogopa!! mungu mpumzishe kwa amani!! wapendwa tumrudie mungu.
 
jamani kwann hii picha mnaiwekaweka tena?acheni izo kwani si tayari ipo kwenye thread ya kifo chake,mnachorudia kuiweka tena na kuianzishia thread mpya ni nn?ivi ingekua ni ndugu yako ungefanya ivo?acha kudhihaki marehemu hata wewe utakufa..
 
kweli mkuu! kumuonyesha mara kwa mara mtu aliyekufa sio haki..mm naamini hata yeye angepata fursa ya kuchagua asingependa picha hii isambazwe hv mtandaoni...tumsitiri marehemu wajameni..Mods ondoa hii picha kwa heshima ya Mr.Ebbo..wengine tunapatwa huzuni sana kumuona ndugu yetu vile.
 
Waswahili Bwana, utafikiri wao hawatakufa. Mwingine anasema hajaiona picha ya marehemu. Lakini tujue kuwa hujafa hujaumbika. Wengine twaweza kufa kifo kibaya hata tukashindwa kuwekwa kwenye hilo jeneza.

All in all nawapa big up sana Waislamu ambao marehemu haonyeshwi. Kuna vitu vya kujifunza katika hilo kwani siyo kila maiti ni ya kuionyesha, wakati mwingine unaidhalilisha tukichukulia wengine wanaichukulia kama habari ya kuitangaza. Mimi hapa najipanga kuwaambia ndugu zangu nikiugua, nikabadilika sitaki kuonekana kwa watu. Kama kutoa heshima za mwisho watazunguka jeneza ambalo litakuwa na picha kama nilivyokjuwa hapo awali, inatosha.
 
Gaddafi mbona alionyeshwa? Au yeye hakuwahi kuhiji licha ya kujenga misikiti?
 
PAMOJA na kifo cha msanii, Mr. Ebbo, kuwasikitisha maelfu ya wapenda muziki nchini, hali ya kutoelewana ‘bifu' kati ya wasanii wa Arusha na Dar es Salaam, imetanda kama vita baridi.

Mr. Ebbo, ambaye jina lake halisi ni Abel Motika Loshlaa, alifariki dunia wiki iliyopita katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Baadhi ya wasanii wa miondoko ya hip hop, wamezungumza na gazeti hili na kuonyesha kukerwa na namna wenzao wa Dar es Salaam walivyoshindwa kujitokeza kwenye mazishi yake yaliyofanyika juzi huko Moshono mjini Arusha.

"Sidhani kama kunitaja jina ndiyo ishu, pointi yangu ya msingi ni hivi, Dar es Salaam wameonyesha ni wabaguzi na watu wasiojali," alisema msanii ambaye anatokea Arusha lakini mara nyingi amekuwa jijini Dar.

Msanii mwingine maarufu anayetokea Arusha naye alisema hivi: "Kaka huwezi kuamini, wasanii kutoka Dar es Salaam utafikiri wamefanya mgomo. Kama huja Arusha kwa ajili ya shoo, vipi wanashindwa kuja kumzika mwenzao? Tena mtu kama Mr. Ebbo, ambaye hakuwa na makundi wala makuu, imetuuma sana."

Mara baada ya mazishi yake juzi, mitandao mbalimbali ikiwemo ya kijamii kama Facebook ilisambaza taarifa za wasanii wa Dar es Salaam kutojitokeza.

Hali hiyo ilizua hisia tofauti, huku baadhi ya wachangiaji wakiwaponda wasanii kutoka Dar es Salaam na wengine wakitaka watu kutolikuza suala hilo kupitia U-arusha na U-dar es Salaam, kwa kuwa kwenda msibani ni hiari ya mtu.mia
 
kama lilikuwepo gari la bure na mimi ningeenda. Wasiwe magwiji tu wa kulaumu
 
Wasanii wenyewe hawa wa Ruge Mutahaba watapata wapi nauli ya kuja Arusha??
mpaka Ruge aandae Show huko waletwe na Bwana wao.
 
Kwani hakuna hata mmoja aliyekwenda? Bonge wa Clouds FM sio Msanii? Maana yeye alikuwepo.
 
Back
Top Bottom