arabianfalcon
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 2,285
- 584
Iko wapi hiyo picha?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iko wapi hiyo picha?
HA! Hao wamasai wa mtwara si wa ArushaMiguu juu kichwa chini.
mmmh! ni kweli huyu ni mr.ebo???? ooh! jamani jamani! nimeogopa!! mungu mpumzishe kwa amani!! wapendwa tumrudie mungu.Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi. R.I.P. Mr Ebbo!![]()
kweli mkuu! kumuonyesha mara kwa mara mtu aliyekufa sio haki..mm naamini hata yeye angepata fursa ya kuchagua asingependa picha hii isambazwe hv mtandaoni...tumsitiri marehemu wajameni..Mods ondoa hii picha kwa heshima ya Mr.Ebbo..wengine tunapatwa huzuni sana kumuona ndugu yetu vile.jamani kwann hii picha mnaiwekaweka tena?acheni izo kwani si tayari ipo kwenye thread ya kifo chake,mnachorudia kuiweka tena na kuianzishia thread mpya ni nn?ivi ingekua ni ndugu yako ungefanya ivo?acha kudhihaki marehemu hata wewe utakufa..
stress nyingi siku hizi hasa huu mwisho wa mwaka.Miguu juu kichwa chini.
PAMOJA na kifo cha msanii, Mr. Ebbo, kuwasikitisha maelfu ya wapenda muziki nchini, hali ya kutoelewana ‘bifu' kati ya wasanii wa Arusha na Dar es Salaam, imetanda kama vita baridi.
Mr. Ebbo, ambaye jina lake halisi ni Abel Motika Loshlaa, alifariki dunia wiki iliyopita katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Baadhi ya wasanii wa miondoko ya hip hop, wamezungumza na gazeti hili na kuonyesha kukerwa na namna wenzao wa Dar es Salaam walivyoshindwa kujitokeza kwenye mazishi yake yaliyofanyika juzi huko Moshono mjini Arusha.
"Sidhani kama kunitaja jina ndiyo ishu, pointi yangu ya msingi ni hivi, Dar es Salaam wameonyesha ni wabaguzi na watu wasiojali," alisema msanii ambaye anatokea Arusha lakini mara nyingi amekuwa jijini Dar.
Msanii mwingine maarufu anayetokea Arusha naye alisema hivi: "Kaka huwezi kuamini, wasanii kutoka Dar es Salaam utafikiri wamefanya mgomo. Kama huja Arusha kwa ajili ya shoo, vipi wanashindwa kuja kumzika mwenzao? Tena mtu kama Mr. Ebbo, ambaye hakuwa na makundi wala makuu, imetuuma sana."
Mara baada ya mazishi yake juzi, mitandao mbalimbali ikiwemo ya kijamii kama Facebook ilisambaza taarifa za wasanii wa Dar es Salaam kutojitokeza.
Hali hiyo ilizua hisia tofauti, huku baadhi ya wachangiaji wakiwaponda wasanii kutoka Dar es Salaam na wengine wakitaka watu kutolikuza suala hilo kupitia U-arusha na U-dar es Salaam, kwa kuwa kwenda msibani ni hiari ya mtu.mia