KERO Abiria tunaoenda hadi Intel kupitia kwa Morombo jioni tunateseka kwani magari huishia Morombo

KERO Abiria tunaoenda hadi Intel kupitia kwa Morombo jioni tunateseka kwani magari huishia Morombo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wanaotegemea magari ya Intel yanayopita Morombo wanakumbana na changamoto kubwa nyakati za jioni kuanzia saa 12. Magari mengi hukataa kuendelea na safari hadi Intel na huishia kupakia abiria wanaokwenda Morombo pekee.

Hali hii imewasababishia usumbufu mkubwa wasafiri, wakiwemo wanafunzi, ambao hulazimika kusubiri kwa muda mrefu au kutegemea magari ya Costa ili kufika wanakoenda.

Tunaomba mamlaka husika na wasimamizi wa usafiri wachukue hatua kutatua tatizo hili, kwani kila jioni wananchi wanaendelea kupata usumbufu mkubwa.
 
Back
Top Bottom