Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Baada ya makala ya uchafu kwenye mabasi ya njia hii iliyofuatiwa na makala ya abiria kusafirishwa kama wafungwa , sasa nimewaletea makala ya vyakula wanavyolishwa abiria hawa wenye uchovu na njaa, na ambao wamepewa dakika 10 tu za kula pamoja na kuchimba dawa.
Natambua kwamba zipo makala zilizochambua bei za vyakula kwenye migahawa ya njiani, mimi nitajikita kwenye chakula chenyewe, ama kwa hakika chakula wanachouziwa abiria hawa ni chakula duni mno!
Kwenye njia hii kuna Hotel kadhaa kuna inayoitwa Bismillah kuna Aljazeera na nyingine inayosuasua inaitwa Kitonga Comfort (zaweza kuwepo zingine pia) kiukweli vyakula vinavyouzwa kwenye hotel hizi ni vibovu, visivyostahili kuliwa na binadamu, wali mbovu kabisa unaofanana na ule wali wa mdundiko (kwa wahenga wamenielewa), hauna ladha hata chembe, kule kwetu Kyela kuna mchele unaitwa Mwangulu, huu ni mchele ambao wali wake hata nguruwe hawapewi, wali unaopikwa kwenye hotel hizi unafanana na Mwangulu, Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba Wali uliobaki kwenye hoteli hizi haujawahi kumwagwa, unapashwa na kuuzwa tena kesho, hii ni hatari sana, abiria aliyepewa dakika 10 hana uwezo wa kukataa chakula hiki atakufa njaa.
Njoo kwenye nyama choma, huku ndio utashangaa hadi uzimie, nyama haieleweki kama ni ya mnyama gani, nyingine hazikuiva lakini tayari zilishawekwa kwenye mifuko ya take away ili kuwahi abiria, hii ni hatari mno kiafya. Wamiliki wa hotel hizi haya wanayajua?
Kuna haja ya mamlaka kuchukua hatua ili kunusuru abiria .