Abiria wa mabasi ya mikoani hasa Dar - Iringa - Mbeya wanakula chakula kibovu. Mamlaka ziingilie kati

Abiria wa mabasi ya mikoani hasa Dar - Iringa - Mbeya wanakula chakula kibovu. Mamlaka ziingilie kati

Umesema kweli mkuu, hizo hotel zao huwa sigusi kitu ni chafu mno.
Ongezea Arusha to Dodoma
Arusha to Singida
Dodoma to Mwanza.
Barabara yenye msosi bora ni Dar -Arusha
... uko sahihi. Sometimes nikisafiri na vi-kids vyangu, vikikaribia vilima na kona za Korogwe kwanza kama vilikuwa vimeuchapa usingizi vyote vinaamka then vinakuwa na uso wa bashasha simply vimekaribia sehemu ya kula na kupumzika! All the way, restaurant za pale Korogwe ndio their best place to enjoy their safari - kula, kunywa, kujisaidia, kupata hewa safi, na zaidi kupiga picha! Korogwe wanajitahidi kwa kweli japo bei zao sio haba.

Pia umaarufu wa Korogwe umechangiwa na sehemu yenyewe kuwa exactly half-way DAR - MOSHI/ARUSHA. Kwa njia ya DAR - MBEYA "center" ya kueleweka haipo - sijui ni Morogoro? Too far too close kutegemea unatokea wapi. Ni Mikumi? Ni Ruaha? Kitonga? Ilula? Ni Iringa? Mafinga? Hii inachangia wenye hela zao kuto-invest vitu vya maana kwani hata locations hazieleweki ipi ni ipi. Mtazamo wangu anyway.
 
The only route chakula kisafi ni moshi arusha. The rest nchii pwagu na pwaguzi tuuu
 
Ongezea na Njia ya Nyan'goro kutokea Dodoma, hamna Sehemu nzuri ya kupata Chakula hasa pale Migoli, kuna ka mgahawa wanalisha watu vitu vya Ovyo hovyo sana. Wamulikwe hawa watu.
 
The only route chakula kisafi ni moshi arusha. The rest nchii pwagu na pwaguzi tuuu
... tena Korogwe tu. Pana restaurant/hoteli za maana kama 4 hivi ziliibuka baada ya wale waarabu wa Mombo (sikumbuki panaitwaje) kuzingua na vyakula na bei za ajabu ajabu. Waliringa sana wale jamaa enzi zao.
 
Kuna jamaa aliwahi kuuliza kama zile nyama hazijuilikani ni za mnyama gani je ni halal?

Yani kwa waislam ambao huzila wana hakika zimechinjwa kuwafuata taratibu za dini yao?!

Kuna msemo maarufu humu JF, "Njaa haina bouncer" sasa linapokuja swala la kula nadhani wengi tunasukumwa na njaa, ila naamini wapo wachache hula kama sehemu yakujiburudisha.

Wanaojiburudisha wanaweza kuwa waangalifu, ila sisi wenye njaa kwakweli huwa tunakosa choices hivyo kutufanya tule chochote kilichopo, au hovyo hovyo bila kujali.

Binafsi ningeshauri, vituo viwe vingi njiani na hoteli ziwe maeneo yanayosimamiwa na halmashauri au manispaa ili kutoa nafasi mwa wakaguzi wa afya/ Afisa afya kusimamia usalama na afya za hoteli na walaji.

Lakini kuweja hoteli hizi maporini kuna toa loopholes kwa wenye migahawa na mahoteli kutulisha vyakula vya hovyo visivyo jali usalama wetu walaji, kwa sababu hazikaguliwi. Na huko wanapotoa hizo nyama / machinjio pori hakukaguliwi na maafisa afya.

Tuombe mamlaka wapeleke maafisa afya huko na wakague nyama ziletwazo kwenye migahawa hii.
 
Kwakwel umenikumbusha nlikua natoka dar kwenda mwanza tulipo fika singida tuliambiwa tuna dakika 10 za kula na kuchimba dawa so nikashuka kwenye basi chap chap kwenda kutafta chakula nilipo ulizia niliambiwa ni elfu5 so nikaamua kuchukua msosi huku nikiwaza kwa dakika hizo 10 naweza kula na kumalza lakn mda kidogo dakika hizo zilikua zimeisha so nikaenda kuomba wanafungie hicho chakula weeeee nilikatwa jicho sito sahau huku nikiwaongelesha bila kujibiwa ikabid niondoke nakukiacha chakula lakn kimoyo moyo niliumia
Chaajabu ile natoka tu anakuja mdada anakimbilia kile chakula ndo nikapata jibu inawezekana kililud kwenye sufuria kwaajil ya kuwauzia watu wengine
 
Njia uchagani itakosaje vitu vya maana?
Mimi sio mchaga lkn
... uko sahihi. Sometimes nikisafiri na vi-kids vyangu, vikikaribia vilima na kona za Korogwe kwanza kama vilikuwa vimeuchapa usingizi vyote vinaamka then vinakuwa na uso wa bashasha simply vimekaribia sehemu ya kula na kupumzika! All the way, restaurant za pale Korogwe ndio their best place to enjoy their safari - kula, kunywa, kujisaidia, kupata hewa safi, na zaidi kupiga picha! Korogwe wanajitahidi kwa kweli japo bei zao sio haba.

Pia umaarufu wa Korogwe umechangiwa na sehemu yenyewe kuwa exactly half-way DAR - MOSHI/ARUSHA. Kwa njia ya DAR - MBEYA "center" ya kueleweka haipo - sijui ni Morogoro? Too far too close kutegemea unatokea wapi. Ni Mikumi? Ni Ruaha? Kitonga? Ilula? Ni Iringa? Mafinga? Hii inachangia wenye hela zao kuto-invest vitu vya maana kwani hata locations hazieleweki ipi ni ipi. Mtazamo wangu anyway.
 
Kuna jamaa aliwahi kuuliza kama zile nyama hazijuilikani ni za mnyama gani je ni halal?

Yani kwa waislam ambao huzila wana hakika zimechinjwa kuwafuata taratibu za dini yao?!

Kuna msemo maarufu humu JF, "Njaa haina bouncer" sasa linapokuja swala la kula nadhani wengi tunasukumwa na njaa, ila naamini wapo wachache hula kama sehemu yakujiburudisha.

Wanaojiburudisha wanaweza kuwa waangalifu, ila sisi wenye njaa kwakweli huwa tunakosa choices hivyo kutufanya tule chochote kilichopo, au hovyo hovyo bila kujali.

Binafsi ningeshauri, vituo viwe vingi njiani na hoteli ziwe maeneo yanayosimamiwa na halmashauri au manispaa ili kutoa nafasi mwa wakaguzi wa afya/ Afisa afya kusimamia usalama na afya za hoteli na walaji.

Lakini kuweja hoteli hizi maporini kuna toa loopholes kwa wenye migahawa na mahoteli kutulisha vyakula vya hovyo visivyo jali usalama wetu walaji, kwa sababu hazikaguliwi. Na huko wanapotoa hizo nyama / machinjio pori hakukaguliwi na maafisa afya.

Tuombe mamlaka wapeleke maafisa afya huko na wakague nyama ziletwazo kwenye migahawa hii.
Hotel kujengwa porini inachangia sana wasafiri kudhulumiwa
 
Ujinga ni kampuni za mabasi kutulisha kwenye hoteli hizo..
Madreva, wakiingiza gari tu hotelini wanasaini sh 10000 , sasa unadhani ni rahisi kukataa hiyo pesa wakati hatumii nguvu zaidi ya kukata kona?
 
Kuna mdau katika ule uzi wa Bei za Vyakula Alishauri:

1, tujitahidi sisi wasafiri kutopenda kulakula sana. Mfano mtu unatoka Dar to Iringa, masaa 8 kuna ulazima gani kula hayo Masaa kama wewe ni mzima wa afya?

2, panapokua na uhitaji kama una mtoto, mgonjwa, unanyonyesha, au una njaa, basi either beba msosi ulipotoka au kula zile fast foods kama juice, maji, biskuit.
Ushauri mbovu huu. Binadamu anatakiwa kutatua matatizo yaliyo ndani ya uwezo wake na siyo kuyakimbia. Kufuata huu ushauri itakuwa ni kama serikali imeogopa na kusalimu amri.
1. Masaa manane ni mengi na mtu hata kama ni mzima wa afya anatakiwa kula kama anajisikia. Kwa nini unataka watu wajitese kwa vitu ambavyo vina utatuzi? Na isitoshe msafiri anaweza kuwa ametoka kwenye mazingira yaliyomfanya asile kabla ya kuanza safari. Si kila msafiri anatoka nyumbani huku akiwa ameshakula. Wengine wanaunganisha safari na hawana muda wa kula kwanza. Pili kuna magari kuharibika au safari kuchelewa. Zipo sababu nyingi sana.
2. Na suala la kubeba chakula nalo ni pendekezo lisilo na mashiko. Sababu ni ile ile, siyo kila msafiri amepanga na kuanza safari kwa kujiandaa.
Mbona zamani mabasi yalikuwa yanasimama stendi za jumuia na watu wanachagua wale nini na waingie hoteli gani? Hoteli zilikuwa zinafanya ushindani na walijitahidi kupika vizuri na kuweka bei ya kuvutia. Mambo yalianza kuharibika baada ya mafisadi wachache kubuni mtindo wa kwenda kujenga hotel maporini na kuwahonga madereva ili wawe wanasimama kwenye hoteli zao ambazo wanapika na kuuza chakula kwa bei wanayotaka. Ushindani ukirudi kila kitu kitakuwa shwari.
 
Back
Top Bottom