Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Unamuongelea mkurugenzi wa TRC kirahisi mbona mnamsahau February alietia hasara ya wazi kabisa 3.1 Trillion hapo Wzr ya nishati,hebu tupambanie nchi tusiwe wanafiki muda wote.Majizi yako hapo mawizarani mnaongelea walipa Kodi waliotia hasara ya shillingi 12,000 kwa route na hata ukiangalia hapo hata milioni tano hazifiki,huu ni unafiki wa juu, February atueleze.3.1 trillion ziliko na bado DP 🌎 dirty game
 
Staff nzima ya TRC kuanzia Bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi wake mkuu wapigwe chini au wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi! Hivi inaingia akilini train ya masafa marefu kupakia abiria wa buku? (1,000/=) kweli? Hawa watu wana akili au matope? Kwani daladala za gongolamboto hawazioni? Yaani train inayoenda speed ya 160km/saa iwe inasimama na kushusha abilia kila baada ya akika 5 au 10? Alafu bila aibu wanakuja kwenye hadhira na vyombo vya habari eti hao abilia wa buku wanasafiri hadi Dodoma/Morogoro kwa buku? Real? Mradi wa SGR umegharimu trillions za hela ya walipa kodi na madeni na riba juu alafu wajinga na mapunguani wanataka kuuharibu? Watanzania nani katuloga? Hivi unaweza kwenda Magufuli Bus terminal ukapanda basi la kwenda Dodoma ukawapa buku wakushushe kibaha wakakubali? Mambo mengine yanatia hasira?

Ndo serikali yako hiyo ya ccm mkuu, wamewaachia wananchi nao wajipigie wanavyotaka
 
Nauli 1000???? Wapo serious kweli TRc?
Halafu mapema wanasema shirika limepata hasara .
 
Naskia SGR wanapakia abiria hadi wa buku alafu wanapitiliza hadi dodoma

Juzi hapa kulikuwa na malalamiko abiria wa Doodma wale original na wa moro wanakosa tiketi wanaona online treni imejaa kumbe mmewapa nafasi watu wa pugu na abira wa karibu kwa bei kitonga na hao kitonga ni wahuni wanaopitiliza hadi Morogoro, Dodoma kwa elfu moj hivi hamuoni aibu?

Huu mradi msipikuwa makini mtauuwa mapema tu maana naona hii ni michezo ya wafanyakazi

Ukienda abood pale hakuna nauli ya mlandizi wala nauli ya Chalinze ukipanda gari ya mro kama nuali ni sh 13000 utalipia hiyp hiyo 13000 hakuna masihara

Ukipanda tilisho,kilimanjaro,bm za arusha kama unashukia Tanga au himo wao haiwahusu utalipa 45000 ile ile ya Arusha wanafanya hivyo kuepuka upigaji wa wafanyakazi na abiria wasio waaminifu sasa nyie sgr hamjifunzi kwa wenzenu?

Abiria wa pugu si apande daladala za gongo la mboto pugu kwenye sgr anafuata nini
Yaani umepiga penyewe ila sina hakika kama wahusika watafanyia kazi

Siku niliyosikia kuwa kuna watu wanakata ticket za kushukia Pugu, nilicheka kwa hasira sana. Yaani watu wa panning serikali ndio wanaofelisha hii nchi

Mi naungana na hoja yako, kituoni wasimame na watu wapande na kushuka. Hata hivyo, nauli ibaki ya vituo vikubwa tu kama ulivyotolea mfano wa usafiri wa bus

Kwenye bango lao la nauli wameonyesha nauli za Dar - Moro na Dar - Dom iongezeke na nauli ya Mor - Dar.

Anayeshuka pugu, ruvu, ngerengere sijui na wapi huko wote walipe nauli za Dar - Moro
 
Usalama wa Taifa au TRC management/board walikuwa wapi muda wote huo. Bila ku-anticipate kuwa kuna risk ya watu kulipa nauli ya pugu akaenda mpaka Dodoma?
Ticketing Software ndo Tatizo- ilitakiwa mtu akishuka Pugu Software ionyeshe kuwa baada ya Pugu Siti ipo wazi.... Software ya TRC Ticketing yeyewe inasoma Dar- Dodoma au Dar - Moro akuna kituo kingine🤣🤣🤣.Jumamos nilikuwa natoka Dodoma to Dar..... 1. System inaonyesha Tren imejaa mpaka kesho Jumanne.....Japo kuna mtu aliingia kwenyr system Jumamos saa tano mchana akapata ticketi...Mimi nilipata Ticket Dodoma- Moro, na kukata ya Jumapili Moro Dar .... tren wakati inatoka Dodoma nilipata siti behewa no 12. Nilipandia Behewa no.6.... kila behewa lilikuwa na siti tupu mengine zaidi ya siti 5 au zaidi. Ata Behewa no 12 pia lilikuwa na siti chache bila watu.... nikiwa ndani ya Treni nilipomuuliza Muhudumu kama ntapata ticket ya Moro- Dar akasema ndo ntapata ila badala ya elfu 13, nimpe 26 elfu🤣Nikakataa... nikashuka Moro , Na jumapili nisafiri to Dar... Ticket yangu ya Dodoma Moro ilikuwa inasomeka Dodoma Dar es salaam Nauli elfu 18.
 
Hii ni hatari... Natumaini wahusika wanafuatilia hata kama walikuwa hawataki kuyajua haya
 
Wanashindwa kuwa wabunifu. Watengeneza mabehewa ya Abiria wa njiani.

Na kwa treni inayoanzia Dar na kituo cha kwanza kiwe Ruvu siyo Pugu.

Shida tumejaza watu wasiofikira katika hizi Taasisi.
Wala hakuna Haja ya kutenga mabehewa, waweke system isiyokuwa na tiketi za njiani kituo cha kwanza kiwe Kingolwira na walipe nauli ya Morogoro. Kwa wale wanaoanzia njiani nako tiketi zisiruhusu mtu anayeishia ndani ya kilomita 50! Vinginevyo warudishe utaratibu wa enzi ya ngongongo, kuwe na ma TT watakaokuwa wanakagua tiketi kila baada ya muda fulani!
 
Naskia SGR wanapakia abiria hadi wa buku alafu wanapitiliza hadi dodoma

Juzi hapa kulikuwa na malalamiko abiria wa Doodma wale original na wa moro wanakosa tiketi wanaona online treni imejaa kumbe mmewapa nafasi watu wa pugu na abira wa karibu kwa bei kitonga na hao kitonga ni wahuni wanaopitiliza hadi Morogoro, Dodoma kwa elfu moj hivi hamuoni aibu?

Huu mradi msipikuwa makini mtauuwa mapema tu maana naona hii ni michezo ya wafanyakazi

Ukienda abood pale hakuna nauli ya mlandizi wala nauli ya Chalinze ukipanda gari ya mro kama nuali ni sh 13000 utalipia hiyp hiyo 13000 hakuna masihara

Ukipanda tilisho,kilimanjaro,bm za arusha kama unashukia Tanga au himo wao haiwahusu utalipa 45000 ile ile ya Arusha wanafanya hivyo kuepuka upigaji wa wafanyakazi na abiria wasio waaminifu sasa nyie sgr hamjifunzi kwa wenzenu?

Abiria wa pugu si apande daladala za gongo la mboto pugu kwenye sgr anafuata nini
Juzikati nimetoka Morogoro mjini kwenda Kilosa. Nikapanda gari ya Kilosa nia yangu nikashuke Dumila kisha niendelee baadae. Gari imefika Dumila nimesinzia, nimezinduka Mvumi nikafika Kilosa kwa nauli ya Dumila.
 
Back
Top Bottom