Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Unamuongelea mkurugenzi wa TRC kirahisi mbona mnamsahau February alietia hasara ya wazi kabisa 3.1 Trillion hapo Wzr ya nishati,hebu tupambanie nchi tusiwe wanafiki muda wote.Majizi yako hapo mawizarani mnaongelea walipa Kodi waliotia hasara ya shillingi 12,000 kwa route na hata ukiangalia hapo hata milioni tano hazifiki,huu ni unafiki wa juu, February atueleze.3.1 trillion ziliko na bado DP 🌎 dirty game
 

Ndo serikali yako hiyo ya ccm mkuu, wamewaachia wananchi nao wajipigie wanavyotaka
 
Nauli 1000???? Wapo serious kweli TRc?
Halafu mapema wanasema shirika limepata hasara .
 
Yaani umepiga penyewe ila sina hakika kama wahusika watafanyia kazi

Siku niliyosikia kuwa kuna watu wanakata ticket za kushukia Pugu, nilicheka kwa hasira sana. Yaani watu wa panning serikali ndio wanaofelisha hii nchi

Mi naungana na hoja yako, kituoni wasimame na watu wapande na kushuka. Hata hivyo, nauli ibaki ya vituo vikubwa tu kama ulivyotolea mfano wa usafiri wa bus

Kwenye bango lao la nauli wameonyesha nauli za Dar - Moro na Dar - Dom iongezeke na nauli ya Mor - Dar.

Anayeshuka pugu, ruvu, ngerengere sijui na wapi huko wote walipe nauli za Dar - Moro
 
Usalama wa Taifa au TRC management/board walikuwa wapi muda wote huo. Bila ku-anticipate kuwa kuna risk ya watu kulipa nauli ya pugu akaenda mpaka Dodoma?
Ticketing Software ndo Tatizo- ilitakiwa mtu akishuka Pugu Software ionyeshe kuwa baada ya Pugu Siti ipo wazi.... Software ya TRC Ticketing yeyewe inasoma Dar- Dodoma au Dar - Moro akuna kituo kingine🤣🤣🤣.Jumamos nilikuwa natoka Dodoma to Dar..... 1. System inaonyesha Tren imejaa mpaka kesho Jumanne.....Japo kuna mtu aliingia kwenyr system Jumamos saa tano mchana akapata ticketi...Mimi nilipata Ticket Dodoma- Moro, na kukata ya Jumapili Moro Dar .... tren wakati inatoka Dodoma nilipata siti behewa no 12. Nilipandia Behewa no.6.... kila behewa lilikuwa na siti tupu mengine zaidi ya siti 5 au zaidi. Ata Behewa no 12 pia lilikuwa na siti chache bila watu.... nikiwa ndani ya Treni nilipomuuliza Muhudumu kama ntapata ticket ya Moro- Dar akasema ndo ntapata ila badala ya elfu 13, nimpe 26 elfu🤣Nikakataa... nikashuka Moro , Na jumapili nisafiri to Dar... Ticket yangu ya Dodoma Moro ilikuwa inasomeka Dodoma Dar es salaam Nauli elfu 18.
 
Hii ni hatari... Natumaini wahusika wanafuatilia hata kama walikuwa hawataki kuyajua haya
 
Wanashindwa kuwa wabunifu. Watengeneza mabehewa ya Abiria wa njiani.

Na kwa treni inayoanzia Dar na kituo cha kwanza kiwe Ruvu siyo Pugu.

Shida tumejaza watu wasiofikira katika hizi Taasisi.
Wala hakuna Haja ya kutenga mabehewa, waweke system isiyokuwa na tiketi za njiani kituo cha kwanza kiwe Kingolwira na walipe nauli ya Morogoro. Kwa wale wanaoanzia njiani nako tiketi zisiruhusu mtu anayeishia ndani ya kilomita 50! Vinginevyo warudishe utaratibu wa enzi ya ngongongo, kuwe na ma TT watakaokuwa wanakagua tiketi kila baada ya muda fulani!
 
Juzikati nimetoka Morogoro mjini kwenda Kilosa. Nikapanda gari ya Kilosa nia yangu nikashuke Dumila kisha niendelee baadae. Gari imefika Dumila nimesinzia, nimezinduka Mvumi nikafika Kilosa kwa nauli ya Dumila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…