Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,176
Aiseee nadhani mh mwakyembe ana hitaji msaada kwenye hii vita?
Hii machine mbona Kama imechakaa ghafla baada ya kukata hicho Chuma au ilifungwa hapo kwanza kisha kikahamishiwa katika machine nyingine! Tazama kwa umakini hizo picha.
Yale yale watu wanaofanya ujambazi huko misitu ya Biharamulo ni Wanyarwanda, wanaofanya uhalifu Arusha ni Wakenya, nk. Wabongo tuna mtazamo mmoja finyu sana wa kujiaminisha kuwa Mtanzania ni malaika, hayo mazagazaga ni watu wengine! Sisi huwa hatufanyi uhalifu! Je wale mabinti wasanii akina Masozange waliokamatwa SA ni Wanyarwanda au Wakenya, Wasomalia?
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.
Ni kweli Yahaya hizo mashine ni tofauti ila haiondoi ukweli wa tukio,cha kuangalia sasa ni uhalali wa wamiliki wa passport zetu maana kuna watu wa mataifa fulani reputation yao ni mbaya abroad na ujanja wanaotumia ni kujificha kwenye uraia wa nchi zinazoaminika na kufanya maovu!
Toka lini kifaa kinunuliwe Tanzania kitumwe China mbona vice-versa
Tanzania hawana mitambo ya kuona madawa yaliyofichwa namna hiyo.
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.
Na alietuloga atakuwa amekufa,kwani angelikuwa hai angelituonea huruma tunavyoadhirika duniani na angetuondolea hii Aibu!Mmmmh
Hivi watanzania tumerogwa na nani? Looh!!!!
Mwakyembe si anakesha hapo kiwanjani..sasa huyu kapitia wapi tena?
kila kukicha wanafichua mbinu mpya
Ndugu ebu tuweke wazi mbona hizo mashine ni tofauti? hiyo nzima hailingani na hiyo iliyokatwa inawezekana kuna udanganyifu wa picha ingawa taarifa inaweza kuwa ya kweli.
Tanzania tunastahili tuzo katika hii biashara!